< Luka 15 >

1 Siku moja, watoza ushuru na wahalifu wengi walikwenda kumsikiliza Yesu.
Then drew near to him all the tax collectors and sinners to hear him.
2 Mafarisayo na walimu wa Sheria wakaanza kunung'unika: “Mtazameni mtu huyu! Anawakaribisha wenye dhambi, na tena anakula nao.”
And the Pharisees and scribes murmured, saying, This man receiveth sinners, and eateth with them.
3 Yesu akawajibu kwa mfano:
And he spoke this parable to them, saying,
4 “Hivi, mtu akiwa na kondoo mia, akigundua kwamba mmoja wao amepotea, atafanya nini? Atawaacha wale tisini na tisa mbugani, na kwenda kumtafuta yule aliyepotea mpaka ampate.
What man of you, having an hundred sheep, if he loseth one of them, doth not leave the ninety and nine in the wilderness, and go after that which is lost, until he findeth it?
5 Akimpata, atambeba mabegani kwa furaha.
And when he hath found it, he layeth it on his shoulders, rejoicing.
6 Anapofika nyumbani, atawaita rafiki zake akiwaambia, Furahini pamoja nami, kwa sababu nimempata yule kondoo wangu aliyepotea.
And when he cometh home, he calleth together his friends and neighbours, saying to them, Rejoice with me; for I have found my sheep which was lost.
7 Kadhalika nawaambieni, ndivyo kutakavyokuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya kutubu kwa mwenye dhambi mmoja, kuliko kwa ajili ya watu tisini na tisa wanaojiona kuwa wema, wasiohitaji kutubu.
I say to you, that likewise joy shall be in heaven over one sinner that repenteth, more than over ninety and nine righteous persons, who need no repentance.
8 “Au mwaonaje? Tuseme mwanamke fulani ana sarafu kumi za fedha, akipoteza moja, atafanya nini? Atawasha taa, aifagie nyumba na kuitafuta kwa uangalifu mpaka aipate.
Either what woman having ten pieces of silver, if she loseth one piece, doth not light a lamp, and sweep the house, and seek diligently till she findeth it?
9 Akiipata, atawaita rafiki na jirani zake akisema, Furahini pamoja nami, kwa sababu nimeipata ile sarafu yangu iliyopotea.
And when she hath found it, she calleth her friends and her neighbours together, saying, Rejoice with me; for I have found the piece which I had lost.
10 Kadhalika nawaambieni, ndivyo watakavyofurahi malaika wa Mungu kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja anayetubu.”
Likewise, I say to you, there is joy in the presence of the angels of God over one sinner that repenteth.
11 Yesu akaendelea kusema, “Kulikuwa na mtu mmoja mwenye wana wawili.
And he said, A certain man had two sons:
12 Yule mdogo, alimwambia baba yake: Baba, nipe urithi wangu. Naye akawagawia mali yake.
And the younger of them said to his father, Father, give me the portion of goods that falleth to me. And he divided to them his living.
13 Baada ya siku chache, yule mdogo aliuza urithi wake, akasafiri na fedha aliyopata, akaenda nchi ya mbali ambako aliitumia ovyo.
And not many days after the younger son gathered all together, and took his journey into a far country, and there wasted his substance with riotous living.
14 Alipomaliza kutumia kila kitu, kukatokea njaa kali katika nchi ile, naye akaanza kuhangaika.
And when he had spent all, there arose a mighty famine in that land; and he began to be in want.
15 Akaomba kazi kwa mwananchi mtu mmoja wa huko naye akampeleka shambani mwake kulisha nguruwe.
And he went and joined himself to a citizen of that country; and he sent him into his fields to feed swine.
16 Alitamani kula maganda waliyokula wale nguruwe, ila hakuna mtu aliyempa kitu.
And he was longing to fill his belly with the husks that the swine ate: and no man gave to him.
17 Alipoanza kupata akili akafikiri: Mbona kuna wafanyakazi wengi wa baba yangu wanaokula na kusaza, nami ninakufa njaa?
And when he came to himself, he said, How many hired servants of my father have bread enough and to spare, and I am perishing with hunger!
18 Nitarudi kwa baba yangu na kumwambia: Baba, nimemkosea Mungu, na nimekukosea wewe pia.
I will arise and go to my father, and will say to him, Father, I have sinned against heaven, and before thee,
19 Sistahili hata kuitwa mwanao. Nifanye kama mmoja wa wafanyakazi wako.
And am no more worthy to be called thy son: make me as one of thy hired servants.
20 Basi, akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Alipokuwa bado yu mbali, baba yake alimwona, na kwa moyo wa huruma alimkimbilia, akamkumbatia na kumbusu.
And he arose, and came to his father. But when he was yet a great way off, his father saw him, and had compassion, and ran, and fell on his neck, and kissed him.
21 “Mwanawe akamwambia: Baba, nimemkosea Mungu, na nimekukosea wewe pia. Sistahili hata kuitwa mwanao.
And the son said to him, Father, I have sinned against heaven, and in thy sight, and am no more worthy to be called thy son.
22 Lakini baba yake akawaambia watumishi wake: Haraka! Leteni nguo nzuri mkamvike! Mvisheni pete na viatu!
But the father said to his servants, Bring forth the best robe, and put it on him; and put a ring on his hand, and shoes on his feet:
23 Mchinjeni ndama mnono; tule kusherehekea!
And bring here the fatted calf, and kill it; and let us eat, and be merry:
24 Kwa sababu huyu mwanangu alikuwa amekufa, kumbe yu mzima alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana. Wakaanza kufanya sherehe.
For this my son was dead, and is alive again; he was lost, and is found. And they began to be merry.
25 “Wakati huo kaka yake alikuwa bado shambani. Alipokuwa akirudi na kukaribia nyumbani akasikia vifijo na ngoma.
Now his elder son was in the field: and as he came and drew near to the house, he heard music and dancing.
26 Akamwita mmoja wa watumishi, akamwuliza: Kuna nini?
And he called one of the servants, and asked what these things meant.
27 Huyo mtumishi akamwambia: Ndugu yako amerudi nyumbani, na baba yako amemchinjia ndama mnono kwa kuwa amempata akiwa salama salimini.
And he said to him, Thy brother is come; and thy father hath killed the fatted calf, because he hath received him safe and sound.
28 Huyo kijana mkubwa akawaka hasira hata akakataa kuingia nyumbani. Baba yake akatoka nje na kumsihi aingie.
And he was angry, and would not go in: therefore his father came out, and entreated him.
29 Lakini yeye akamjibu: Kumbuka! Miaka yote nimekutumikia, sijavunja amri yako hata mara moja. Umenipa nini? Hujanipa hata mwana mbuzi mmoja nikafanye sherehe pamoja na rafiki zangu!
And he answering said to his father, Lo, these many years do I serve thee, neither have I at any time transgressed thy commandment: and yet thou never gavest me a kid, that I might make merry with my friends:
30 Lakini mtoto wako huyu aliyekula mali yako pamoja na makahaba, mara tu alipokuja umemchinjia yule ndama mnono.
But as soon as this thy son had come, who hath devoured thy living with harlots, thou hast killed for him the fatted calf.
31 Baba yake akamjibu: Mwanangu, wewe uko pamoja nami siku zote, na kila nilicho nacho ni chako.
And he said to him, Son, thou art ever with me, and all that I have is thine.
32 Ilitubidi kufanya sherehe na kufurahi, kwa sababu huyu ndugu yako alikuwa amekufa, kumbe yu mzima; alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana.”
It was right that we should make merry, and be glad: for this thy brother was dead, and is alive again; and was lost, and is found.

< Luka 15 >