< 1 Petro 3 >

1 Kwa ndila yii, mwenga mwabubile mwalwawa mupalikwa kwipiya kwa akinasengo binu mwabena, ili ata baadhi yabe banaliyikitya li neno, pitya tabia ya akinajumbo babe baweza utilwa bila neno.
Kwa njia hii, ninyi ambao ni wake mnapaswa kujitoa kwa waume zenu wenyewe, ili, hata kama baadhi yao hawajalitii neno, kupitia tabia za wake zao wanaweza kuvutwa pasipo neno,
2 kwa sababu balu bene baluwa bona tabia yinu njema pamope na heshima.
kwa sababu wao wenyewe watakuwa wameiona tabia yenu njema pamoja na heshima.
3 Yino ipangike siyo kwa mapambo ga panja suka njwili, vito vya dhahabu, au ngubo ya mitindo.
Hii ifanyike siyo kwa mapambo ya nje—kusuka nywele, vito vya dhahabu, au mavazi ya mtindo.
4 Lakini badala yake mupange kwa utu wa nkati ya mwoyo, na zidi katika goloka ma unyenyekevu na utulivu wa mwoyo ambani wa thamani mbele ya Nn”ungu
Lakini badala yake ifanyike kwa utu wa ndani wa moyo, na kuzidi katika uzuri wa unyenyekevu na utulivu wa moyo, ambao ni wa thamani mbele za Mungu.
5 Kwa njo alwawo atakatifu bate kwi pamba bene kwa ajili yino. Bibile na imani katika Nn”ungu na bate kawatii akina sengo babe bene.
Kwa kuwa wanawake watakatifu walijipamba wenyewe kwa njia hii. Walikuwa na imani katika Mungu na waliwatii waume zao wenyewe.
6 Kwa ndila yino, sana atikujuawa Ibrahamu na kunkema ywembe “mchengowe” mwenga lelo ni mwabana bake mana mwapanga ganang'oloka na mwana nyogopali mabaya.
Kwa njia hii Sara alimtii Ibrahamu na kumwita yeye “bwana” wake. Ninyi sasa ni watoto wake kama mtafanya yaliyo mazuri na kama hamwogopi mabaya.
7 Kwa ndila yoyoyo mwenga mwanalume mupalikwa tamaa na akinajumbo binu mutangite panga ni ainu alwawani dhaifu, mwatangite bembe kasi yabe pokya ainu zawadi ya ukoti. Mupange nya ili kwamba luba kwinu kwane mukotoke.
Kwa njia hiyo hiyo, ninyi wanaume mnapaswa kuishi na wake zenu mkijua kuwa wao ni wenzi wa kike dhaifu, mkiwatambua wao kama wapokeaji wenzenu wa zawadi ya uzima. Fanyeni hivi ili kwamba maombi yenu yasizuiliwe.
8 Hatimaye, mwenga mwaboti, mube na ndelajimo, mwabene huruma, upendo kati mwalongo mwanyenyekevu, na mwapole.
Hatimaye, ninyi nyote, muwe na nia moja, wenye huruma, upendo kama ndugu, wanyenyekevu, na wapole.
9 Kwane mulipe kwa mbisi tukana kwa tukana. Nungi yake muyendeli bariki, kwa sababu yino mwatekimelwa, ili kwamba muwese kwipata baraka.
Msilipe ovu kwa ovu, au tusi kwa tusi. Kinyume chake, mwendelee kubariki, kwa sababu hii mliitwa, ili kwamba muweze kurithi baraka.
10 Nyembe ywapala kuoenda maisha no bona lisuba sapi lazima alukilibuye lulime lwake kwa mabaya na mikano yake baya hila.
“Yeye atakaye kupenda maisha na kuona siku njema lazima auzuie ulimi wake kwa mabaya na midomo yake kusema hila.
11 Na agalabuke na aleke masapuino panga gagabile mazuri.
Na ageuke na kuacha mabaya na kufanya yaliyo mazuri. Atafute amani na kuifuata.
12 Mijo ya bwana umona mwene haki na masikio gake kugayuwa maombi gake. Lakini kuminyo ya Bwana kubile kinyume na balu babapanga maovu.
Macho ya Bwana humwona mwenye haki na masikio yake husikia maombi yake. Lakini uso wa Bwana uko kinyume cha wale watendao uovu.”
13 Nyai ywapala kudhuru mwe, kanpala tamani lyalibile lizuri.
Ni nani atakayewadhuru ninyi, ikiwa mwatamani lililo zuri?
14 Lakini mwana mwateseka kwa haki mubarikiwe, Kwane muyogope galu ambapo bembe banda gayogapa. Kwane mube na sukala.
Lakini kama mkiteseka kwa haki, mmebarikiwa. Msiogope yale ambayo wao wanayaogopa. Msiwe na wasiwasi.
15 Badala yake mumeke Kristo Bwana katika mwoyo winu kati mtakatifu kila saa mupetayari kunyangwa kila munduywa nokiya mwenga kwa namari mumwobilya Nn”ungu.
Badala yake, mmuweke Kristo Bwana katika mioyo yenu kama mtakatifu. Kila mara muwe tayari kumjibu kila mtu anayewauliza ninyi kwa nini mna tumaini katika Mungu. Fanyeni hivi kwa upole na heshima.
16 Mube na dhamini sapi ili panga bandu babatukana maisha ginu mema katika Kristo bawesa aibika lwa sababu balongela kinyume dhidi yinu panga mwabile mwamupanga maovu.
Muwe na dhamiri njema ili kwamba watu wanaotukana maisha yenu mema katika Kristo waweze kuaibika kwa sababu wanaongea kinyume dhidi yenu kama kwamba mlikuwa watenda maovu.
17 Ni vizuri zaidi mwanaipangite Nn”ungu andapala, kwamba muteseka kwo panga mema kuliko kwo panga mabaya.
Ni vizuri zaidi, ikiwa Mungu anatamani, kwamba mwateseka kwa kufanya mema kuliko kwa kufanya mabaya.
18 Kristo na ywembe atiteseka mara jima kwa ajili ya sambi. Ywembe ambaye ni mwene haki atiteseka kwa ajili yetu ambao twabile twabene haki ili kwamba atulete twenga kwa Nn”ungu.
Kristo pia aliteseka mara moja kwa ajili ya dhambi. Yeye ambaye ni mwenye haki aliteseka kwa ajili yetu, ambao hatukuwa wenye haki, ili kwamba atulete sisi kwa Mungu. Alikufa katika mwili, lakini alifanywa mzima katika roho.
19 Atiwa katika yiga lakini apangilwa nkoti katika mwoyo. Katika mwoyo atinda no kwa bakiya mwoyo ambao sasa utitabilwa.
Katika roho, alikwenda na kuzihubiri roho ambazo sasa ziko kifungoni.
20 Yubile sapili wakati uvumilivu wa Nn”ungu pawabile kaulinda wakatiwa nuhu, lichuba lyabarengesage safina na Nn”ungu atekwaokoa bandu asene nafsi nane buka katika masi.
Hazikuwa tiifu wakati uvumilivu wa Mungu ulipokuwa unasubiri wakati wa Nuhu, siku za ujenzi wa safina, na Mungu aliokoa watu wachache—nafsi nane—kutoka katika maji.
21 Yino n alama you batizo wawakombwa mwenga sasa, sio leka usapu buka muyiga, lakini kwo luba dhamini sapi kwa Nn”ungu pitya yuka Yesu Kristo.
Hii ni alama ya ubatizo unaowaokoa ninyi sasa, siyo kama kuosha uchafu kutoka mwilini, lakini kama ombi la dhamiri njema kwa Mungu, kupitia ufufuo wa Yesu Kristo.
22 Nywemba abile luboko lwa nungi kwa Nn”ungu ayei mbinguni. Malaika na ngupu lazima inyue yewmbe.
Yeye yuko mkono wa kuume wa Mungu. Alikwenda mbinguni. Malaika, mamlaka, na nguvu lazima vimtii yeye.

< 1 Petro 3 >