< 2 Petro 1 >

1 Simoni Petro, Mmanda na mtume wa Yesu Kristo, kwa balo baipokile imani yeyelo ya thamani kati twaipokile twenga, imani yaibile nkati ya haki ya Nnongo na mwokozi witu Yesu Kristo.
Simon Petro, Mtumwa na Mtume wa Yesu Kristo, Kwa wale walioipokea imani ile ile ya thamani kama tulivyoipokea sisi, imani iliyo ndani ya haki ya Mungu na mwokozi wetu Yesu Kristo.
2 Neema ibe kwinu, amani iyongeyekeye pitya maarifa ga Nnongo na Ngwana witu Yesu.
Neema iwe kwenu; amani iongezeke kupitia maarifa ya Mungu na Bwana wetu Yesu.
3 Pitya maarifa ga Nnongo tupatike makowe gake yote kwa ajili ya uchaji wa maisha. Boka kwa Nnongo ywatukemile kwa ajili ya uzuru wa utukufu wake.
Kupitia maarifa ya Mungu tumepata mambo yake yote kwa ajili ya uchaji wamaisha, Toka kwa Mungu aliyetuita kwa ajili ya uzuri wa utukufu wake.
4 Kwa ndela yee atitutumanisha ahadi ngolo ya thamani. Apangite nyoo ili kutupanga barithi ba asili ya Nnongo, kwa kadiri tuyendelya kuuleka ubou wa dunia yee.
Kwa njia hii alitutumainishia ahadi kuu za thamani. Alifanya hili ili kutufanya warith wa asili ya Mungu, kwa kadiri tunavyoendelea kuuacha uovu wa dunia hii.
5 Kwa sababu yee, mupange bidii kuongeza uzuri kwa ndela ya imani yinu, kwa sababu ya uzuri, maarifa.
Kwa sababu hii, fanyeni bidii kuongeza uzuri kwa njia ya imani yenu, kwa sababu ya uzuri, maarifa.
6 Pitya maarifa, kiasi, pitya kiasi saburi, na pitya saburi utauwa.
Kupitia maarifa, kiasi, na kupitia kiasi saburi, na kupitia saburi, utauwa.
7 Pitya utuwa upendo wa alongo na pitya upendo wa alongo, upendo.
Kupitia utauwa upendo wa ndugu na kupitia upendo wa ndugu, upendo.
8 Mana makowe aga gabile nkati yinu, yayendelya kukua nkati yinu, bai mwenga mwapangika kwaa tasa au bandu babeleka kwaa matunda katika maarifa ga Ngwana witu Yesu Kristo.
Kama mambo haya yamo ndani yenu, yakiendelea kukua ndani yenu, basi ninyi hamtakuwa tasa au watu msiozaa matunda katika maarifa ya Bwana wetu Yesu Kristo.
9 Lakini yeyote ywabile kwaa na makowe aga, ugabona makowe ga papipi kae; ywembe nga ipofu, atisahau utakaso ba sambi yake ya kale.
Lakini yeyote asiyekuwa na mambo haya, huyaona mambo ya karibu tu; yeye ni kipofu. amesahau utakaso wa dhambi zake za kale.
10 Kwa eyo, alongo bango, mupange juhudi ili kujihakikishia uteule na wito kwa ajili yinu. Kati mugapanga aga, mwalowa kuikwaa.
Kwa hiyo, ndugu zangu, fanyeni juhudi ili kujihakikishia uteule na wito kwa ajili yenu. Kama mtayafanya haya, hamtajikwaa.
11 Nga nyoo mwaipatia bingi ba nnango wa jingya katika upwalume wangayomoka wa Ngwana witu na nkochopoli Yesu Kristo. (aiōnios g166)
Hivyo mtajipatia wingi wa lango la kuingilia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu na mwokozi Yesu Kristo. (aiōnios g166)
12 Kwa eyo nenga nalowa pangika tayari kuwakombokya makowe aga kila mara, hata kama mwayatanga, nambeambe mubile imara katika kweli.
Kwa hiyo mimi nitakuwa tayari kuwakumbusha mambo haya kila mara, hata kama mnayafahamu, na sasa mmekuwa imara katika kweli.
13 Nawaza kuwa nibile sahihi kubaamsha na kuwakombokya nnani ya makowe aga, ningali nibile nkati ya hema lee.
Nafikiria kuwa niko sahihi kuwaamsha na kuwakumbusha juu ya mambo haya, ningali nimo katika hema hii.
14 Kwa mana nitangite kuwa muda kwaa mrefu nalowa liondoa lihema lyango, kati Ngwana Yesu Kristo atubonekeya.
Kwa maana najua kuwa si muda mrefu nitaiondoa hema yangu, kama Bwana Yesu Kristo alivyonionyesha.
15 Nalowa jitahidi kwa bidii kwa ajili yinu ili mkombokeye makowe aga baada ya nenga kuboka.
Nitajitahidi kwa bidii kwa ajili yenu ili mkumbuke mambo haya baada ya mimi kuondoka.
16 Kwa mana twenga twafata kwaa hadithi zatijingya kwa ustadi palo patulongela nnani ya ngupu na kujidhihirisha kwa Ngwana witu Yesu Kristo, ila twenga tubile mashahidi ba utukufu wake.
Kwa kuwa sisi hatukufuata hadthi zilizoingizwa kwa ustadi pale tulipowaeleza juu ya nguvu na kujidhihirisha kwa Bwana wetu Yesu Kristo, bali sisi tulikuwa mashahidi wa utukufu wake.
17 Ywembe ywapokile utukufu na heshima boka kwa Nnongo tate palo lilobe liyowanike boka katika utukufu nkolo yatibaya.”Ayoo nga mwana wango, mpendwa wango ambaye ywatipendezwa niywembe.”
Yeye alipokea Utukufu na heshima toka kwa Mungu baba pale sauti iliposikika toka katika utukufu mkuu ikisema, “Huyu ndiye mwanangu, mpendwa wangu ambaye nimependezwa naye.”
18 Tuyowine lilobe lee iboka kumaunde palo tubile niywembe katika chelo kitombe kitakatifu.
Tuliisikia sauti hii ikitokea mbinguni pale tulipokuwa naye kwenye ule mlima mtakatifu.
19 Tubile ni lee neno lya unabii lyalithibitike, ambalo kwa lee mwapanga vyema kuliteketeza. Kati taa ya'ing'ara mulibendo mpaka bwamba na ndondwa ga mawio zatibonekana katika mioyo yinu.
Tunalo hili neno la unabii lililothibitika, ambalo kwalo mwafanya vyema kulitekeleza. Ni kama taa ing'aayo gizani mpaka kuchapo na nyota za mawio zionekanazo katika mioyo yenu.
20 Mutangite aga panga, ntopo unabii wauandikilwe kwa sababu ya kuwaza mwabene kwa nabii mwene.
Tambueni haya ya kwamba, hakuna unabii unaoandikwa kwa sababu ya kujifikirisha kwa nabii mwenyewe.
21 Kwa mana ntopo unabii wabile kwa mapenzi ga bandu, ila bandu bapangilwe na Roho mtakatifu ywalongela boka kwa Nnongo.
Kwa kuwa hakuna unabii uliokuja kwa mapenzi ya mwanadamu, isipokuwa wanadamu waliwezeshwa na Roho Mtakatifu aliyeongea toka kwa Mungu.

< 2 Petro 1 >