< 2 Petro 2 >

1 Manabii ba ubocho walowa bokanga kwa Baisraeli, na balimu wa uongo walowa isa kae kwinu. Kwa siri balowa kuapeya mapundisho ga ubocho nabo walowa kunkengama Ngwana ywaabapemeya. Wajiletya uharibifu ba haraka nnani yabe bene.
Manabii wa uongo walijitokeza kwa Waisraeli, na walimu wa uongo watakuja pia kwenu. Kwa siri wataleta mafundisho ya uongo nao watamkana Bwana aliyewanunua. Wanajiletea uharibifu wa haraka juu yao wenyewe.
2 Bingi wapala ndela yabe ya oni na pitya bembe waikufuru ndela ya ukweli.
Wengi watafuata njia zao za aibu na kupitia wao wataikufuru njia ya ukweli.
3 Kwa uchoyo walowa kubanyonya bandu pitya maneno ga ubocho. Hukumu yabe ichelewa kwaa, uharibifu walowa kubakengama.
Kwa uchoyo watawanyonya watu wakitumia maneno ya uongo Hukumu yao haitachelewa, uharibifu utawafuata.
4 Maana Nnongo abaleka kwaa malaika balo batikengeuka. Ila abatombwile kuzimu ili batabilwe ni minyororo mpaka hukumu paiisile nnani yabe. (Tartaroō g5020)
Maana Mungu hakuwaacha malaika waliokengeuka. Bali aliwatupa kuzimu ili wafungwe minyororo mpaka hukumu itakapowajilia. (Tartaroō g5020)
5 Wala Nnongo ativumiliya kwaa ulimwengu wa kunchogo. Ila, atimuhifadhi Nuhu, ywabile ni wito wa haki, pamope ni benge saba, muda wailekite garika nnani ya ulimwengu wabaasi.
Wala Mungu hakuuvumilia ulimwengu wa zamani. Bali, alimhifadhi Nuhu, mwenye wito wa haki, pamoja na wengine saba, wakati alipoachila gharika juu ya ulimwengu ulioasi.
6 Nnongo atiihukumu miji ya Sodoma na Gomora kiasi cha kupangika majivu na uharibifu ili ibe mpwano kwa ajili ya baovu katika masoba gaisa.
Mungu aliihukumu miji ya Sodoma na Gomora kiasi cha kuwa majivu na uharibifu ili iwe mfano kwa ajili ya waovu katika siku za usoni
7 Lakini paapangite lee, atinlopwa Lutu mundu ywa haki ywabile atihuzinishwa na tabia chafu za bakengamite kwaa sheria ya Nnongo.
Lakini alipofanya hilo, alimwokoa Lutu mtu wa haki, aliyekuwa amehuzunishwa na tabia chafu za wasiofuata sheria za Mungu.
8 Kwa mana yolo mundu wa haki, ywatama nabo masoba gatiitesa nafsi yake kwa ajili ya yalo yaagayowine na kugabona.
Kwa kuwa huyo mtu wa haki, aliyeishi nao siku kwa siku akiitesa nafsi yake kwa ajili ya yale aliyoyasikia na kuyaona.
9 Kwa eyo Ngwana atangite jinsi ya kubalopwa bandu bake wakati wa mateso na namna ya kubavumilia baovu kwa ajili ya hukumu katika lisoba lya mwisho.
Kwa hiyo Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa watu wake wakati wa mateso na jinsi ya kuwavumilia waovu kwa ajili ya hukumu katika siku ya mwisho.
10 Hakika woo nga ukweli kwa balo bayendelya tama katika tamaa ya yega yee na kugadharau mamlaka. Bandu ba jinsi yee babile ni ujasiri katika dhamiri yabe. Batiyogopa kwaa kubakufuru atukufu.
Kwa hakika huu ndio ukweli kwa wale wanoendelea kuishi katika tamaa za mwili huu na kuyadharau mamlaka. Watu wa jinsi hii wana ujasiri katika dhamiri zao, Hawaogopi kuwakufuru watukufu.
11 Ingawa malaika babile ni uwezo na ngupu kuliko bandu, lakini baweza kwaa letya hukumu dhidi yabe kwa Ngwana.
Ingawa malaika wana uwezo na nguvu kuliko wanadamu, lakini hawawezi kuleta hukumu dhidi yao kwa Bwana
12 Lakini aba banyama babile kwaa na akili batichengwa kwa asili ya kukamwa na kuangamizwa.
Lakini hawa wanyama wasio na akili wametengenezwa kwa asili ya kukamatwa na kuangamizwa.
13 Baumizwa kwa ujira ba mabou gabe. Mutwekati wote utama kwa anasa. Batijaa ubou na maovu. Upuraikia anasa za ubocho batisherehekea ni wenga.
Wanaumizwa kwa ujira wa maovu yao. Mchana kutwa huishi kwa anasa. Wamejaa uchafu na maovu. Hufurahia anasa za udanganyifu wanaposherehekea na wewe.
14 Minyo gabe yatipunikwa na umalaya; batosheka kwaa panga sambi. Ubalaghai na kubatombwa baumini achunu katika sambi. Babile na mioyo yatijaa tamaa, ni bana balaanilwe.
Macho yao yamefunikwa na uzinzi; hawatosheki kutenda dhambi. Huwalaghai na kuwaangusha waumini wachanga katika dhambi. Wana mioyo iliyojaa tamaa, ni watoto waliolaaniwa.
15 Bailekite ndela ya ukweli. Batitomboka na kuikengama ndela ya Balaam mwana wa Beori, ywapenda kupata malipo ga udhalimu.
Wameiacha njia ya kweli. wamepotoka na wameifuata njia ya Balaam mwana wa Beori, aliyependa kupata malipo ya udhalimu.
16 Lakini ywakanikiwa kwa ajili ya ukosaji wake. Mbonda ywabile bubu alongela kwa lilobe lya bandu, atiukenga uchizi ba nabii.
Lakini alikemewa kwa ajili ya ukosai wake. Punda aliyekuwa bubu akiongea katika sauti ya binadamu, alizuia wazimu wa nabii.
17 Bandu aba ni kati chemichemi ibile kwaa na mase. Ni kati maunde galowa tolwa ni mbepo. Liunde zito lyatihifadhiwa kwa ajili yabe. (questioned)
Watu hawa ni kama chemichemi zisizo na maji. Ni kama mawingu yanayotoweshwa na upepo. Wingu zito limehifadhiwa kwa ajili yao.
18 Ulongela kwa majipuno matupu. Ubatombwa bandu kwa tamaa ya yega. Ubalaghai bandu bajaribia kutila babo batama katika ukosaji.
Huongea kwa majivuno matupu. Huwaangusha watu kwa tamaa ya mwili. Huwalaghai watu wanaojaribu kuwakimbia wale waishio katika ukosaji.
19 Ubaahidi bandu uhuru muda wabe bene ni amanda ba sambi ya ufisadi. Mana mundu upangwa kuba mmanda wa chelo chamtawala.
Huwaahidi watu uhuru wakati wao wenyewe ni watumwa wa dhambi ya ufisadi. Maana mwanadamu hufanywa kuwa mtumwa wa kile kinachomtawala.
20 Ywembe ywajiepushae ni uchafu ba ulimwengu kwa kutumia maarifa ga Ngwana na mkochopoli Yesu Kristo, na boka po atikerebukia uchapu woo kae, hali yake upangika inoite kwaa kuliko yelo ya mwanzo.
Yeye ajiepushaye na uchafu wa ulimwengu kwa kutumia maarifa ya Bwana na mwokozi Yesu Kristo, na kisha akarudia uchafu huo tena, hali yake huwa mbaya kuliko ile ya mwanzo.
21 Inoite bandu kati abo baitangite kwaa ndela ya haki kuliko kuitanga na boka po kuzileka kae amri takatifu zabapeilwe.
Ingefaa watu hao kama wasingeifahamu njia ya haki kuliko kuifahamu na kisha tena kuziacha amri takatifu walizopewa.
22 Mithali yee huwa na ukweli kwabe.”mapwa ukulebukiya matapishi gabe. Ngobe ywatioshwa ukerebuka kae mu'matope.
Mithali hii huwa na ukweli kwao. “mbwa huyarudia matapishi yake. Na nguruwe aliyeoshwa hurudi tena kwenye matope.”

< 2 Petro 2 >