< Yakobo 1 >

1 Yakobo mmanda ba Nnongo ni Ngwana witu Yesu Kristu, kwa makabila komi ni ibele gagatawanyike, salaam.
Yakobo, mtumwa wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo, kwa makabila kumi na mbili yaliyotawanyika, salaam.
2 Mubalange kwamba pulaika muno, alongo bango mwanakamupeta mumatatizo ga kila aina.
Hesabuni kuwa ni furaha zaidi, ndugu zangu, mnapopita katika matatizo mbali mbali,
3 mutange panga ipalilwa imani yinu ipalae pumiliya.
mkijua kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huwapa uvumilivu.
4 Muleke pumilia ili mwikamilishe kasi yake, ili muweze komala kikamilipu, bila pungukiwa ni loloti.
Acheni uvumilivu uikamilishe kazi yake, kwamba muweze kukomaa kikamilifu, bila kupungukiwa katika lolote.
5 Lelo mana mundu kati yinu apala hekima ailobe kuoma kwa Nnongo, ywembe piya kwa wakati ni bila benda kwa boti babannoba, na apala kwapeya kwa hekima.
Lakini kama mtu kati yenu anahitaji hekima, aiombe kutoka kwa Mungu, ambaye hutoa kwa ukarimu na pasipo kukemea kwa wote wamwombao, na atawapa hekima.
6 Lakini mulobe kwa imani, bila shaka, kwa mana ywembe ywabile ni shaka ni kati mawimbi mubahari, tolelwa na upepo notaikuilwa kuno ni kuno.
Lakini omba kwa imani, bila shaka, kwa kuwa mwenye kutia shaka ni kama mawimbi katika bahari, huchukuliwa na upepo na kutupwa huku na huko.
7 Kwa hakika mundu ywoo kana aweze panga apala pokelelwa likowe lyake mboka kwa Ngwana;
Kwa hakika mtu huyu asifikirie kwamba atapokelewa ombi lake kutoka kwa Bwana;
8 Mundu yoo ai'na nia ibele, imara kwaa mundela yake yoti.
mtu huyu ana nia mbili, si imara katika njia zake zote.
9 Mwalongo maskini apalikwa kwipuna kwa yima kwake kunani,
Ndugu maskini anapaswa kujivuna katika kusimama kwake juu,
10 Muda wowo mwalongo tajiri kwo nyenyekea kwake, kwa mana alwambokeka kati liloba lya mmende lya mung'unda mwapetaa.
wakati huo huo ndugu tajiri katika unyenyekevu wake, kwa sababu atatoweka kama ua la kondeni katika shamba analopita.
11 Lisoba lilwapita na lyoto liyotinia yumea michee, na lisoba tomboka n goloka kwake waha. Nganyonyo bandu matajiri bapilya muliyengo lyabe.
Jua huchomoza na joto la kuunguza kukausha mimea, na maua huanguka na uzuri wake hufa. Vivyo hivyo watu matajiri watachakaa katikati ya kazi zao.
12 Atibarikiwa mundu yolo ywapumilia majaribu, na mwana baada ya shinda jaribu lee, apala pokya taji ya ukoto, yaibile itiahidiwa kwa balo babampindile Nnongo.
Amebarikiwa mtu yule anayevumilia majaribu, kwa kuwa baada ya kushinda jaribu hilo, atapokea taji ya uzima, ambayo imeahidiwa kwa wale wampendao Mungu.
13 Mundu ywoywoti apalikwa kwaa baya paajaribiwa, “Jaribu leni liboka kwa Nnongo,” kwa mana Nnongo ajaribiwa kwaa ni ubou, ni Nnongo mwene amjaribu kwaa yeyoti.
Mtu yeyote hapaswi kusema anapojaribiwa, “Jaribu hili linatoka kwa Mungu,” kwa sababu Mungu hajaribiwi na uovu, na Mungu mwenyewe hamjaribu yeyote.
14 Kila mundu ujaribiwa ni tamaa yake mbaya yaimshawishi ni kummuta kunanipa.
Kila mtu hujaribiwa na tamaa zake mbaya zinazomshawishi na kumvuta mbali.
15 Baada ya sambi potwa ndumbo sambi loelekwa, ni yolo sambi komala muno muno, yomokya kwake ni kiwo.
Ndipo baada ya tamaa ya dhambi kubeba mimba, dhambi huzaliwa, na baada ya dhambi kukomaa sawasawa, huishia katika mauti.
16 mwalongo bango mwapendwa, kana mukongelwe.
Ndugu zangu wapendwa, msidanganyike.
17 Kila zawadi inoyite ni kila zawadi yabile kamilifu iboka kunani, iuluka pae kuoma kwa Tate ba nuru, Habadilika kwaa kamwe kati kiwili mwakibadilika.
Kila zawadi iliyo nzuri na kila zawadi iliyokamilika hutoka juu, hushuka chini kutoka kwa Baba wa nuru. Kamwe habadiliki kama kivuli kibadilikavyo.
18 Nnongo atikuchawa kutupeya twenga ukoti pitya Neno lya ukweli, ili tuwese kuba ubelekwi wa kwanza nkati ya iumbe yake.
Mungu alichagua kutupa sisi uzima kwa Neno la kweli, ili kwamba tuweze kuwa kama uzao wa kwanza miongoni mwa viumbe vyake.
19 Mutangite lee, mwalongo bango, Kila yumo apalikwa abe mwepesi wo yowa, nga mwepesi kwaa longela wala kasilika.
Mnajua hili, ndugu zangu wapendwa. Kila mmoja anapaswa kuwa mwepesi wa kusikia, siyo mwepesi wa kuongea wala kukasirika,
20 Kwa mana hasira ya mundu yaweza kwaa kupanga haki ya Nnongo.
kwa kuwa hasira ya mwanadamu haiwezi kutenda haki ya Mungu.
21 kwa nyo mubeke kutalu uchapu wa sambi ni ubaya woti wabile sehemu yoyoti, na kwa nyenyekea mulipoki likowe lyalipendilwe nkati yinu, ambalo libile ni uwezo wokoa roho yinu.
Kwa hiyo wekeni mbali uchafu wa dhambi na ubaya wote ulio mahali popote, na kwa unyenyekevu lipokeeni neno lililopandwa ndani yenu, ambalo lina uwezo wa kuokoa roho zenu.
22 Mulikengame likowe kana muliyowe bai. mwikonga nafsi yinu mwabene.
Litiini neno, msilisikie tu, mkijidanganya nafsi zenu wenyewe.
23 Kwa mana kati yoyoti ywaliyowa likowe bila kulipangya kazi ni sawa ni
Kwa kuwa kama yeyote alisikiaye neno bila kulitendea kazi ni sawa na mtu ajiangaliaye uso wake halisi katika kioo.
24 mundu ywailola kuminyo yake halisi mu'kilolo. Aitasimini kuminyo yake, na kuboka na baada ya muda mwipi libalya mwaabile.
Hujitathimini uso wake, na huenda zake na baada ya muda mfupi husahau anavyofanana.
25 Lelo mundu yoo ywailola kwo uangalifu saliya toti, saliya huru no yendelya kuiheshimu, kana iakamwi kwa sababu ywembe ywa mundu wo'sahau, mundu yoo alowa barikiwa mana aipangite.
Bali mtu yule anayeiangalia kwa uangalifu sheria kamili, sheria ya uhuru, na kuendelea kuitii, si kwa sababu yeye ni msikilizaji anayesahau, huyu mtu atabarikiwa anapoitenda.
26 Mana mundu yeyoti alwawasa mwene panga ni mundu wa dini, lakini awesa kwaa kuutawala lulemi lwake, haukonga mwoyo wake ni dini yake ni yabule.
Ikiwa mtu yeyote atafikiri mwenyewe kuwa ni mtu wa dini, lakini hawezi kuutawala ulimi wake, huudanganya moyo wake na dini yake ni bure.
27 Dini yaibile safi ni iharibike kwaa nnonge ya Nnongo witu ni Tate nga yee: kuasaidia yatima ni ajane mu'mateso yabe, no kuilinda mwene ni ufisadi wa dunia.
Dini iliyo safi na isiyoharibiwa mbele za Mungu wetu na Baba ni hii: kuwasaidia yatima na wajane katika mateso yao, na kujilinda wenyewe na ufisadi wa dunia.

< Yakobo 1 >