< 1 Petro 2 >

1 Kwa njo mubike pabwega ubovu winu woti na konga, unafiki, bwigu na kashifa.
Kwa hiyo wekeni pembeni uovu wote, udanganyifu, unafiki, wivu na kashifa.
2 Kati bana alele mupale mabele supiga pamwoyo ili kwamba muwesekula nkati ya wokovu.
Kama watoto wachanga, mtamani maziwa safi ya kiroho, ili kwamba mweze kukua ndani ya wokovu,
3 Kwa njo mubweni Bwana na mwema.
kama mmeonja kwamba Bwana ni mwema.
4 Mwise kwa bile ywembe liwe likoti lyalitama ambalo litikani lwa na bandu, lakini litisaulikwa na Nn”ungu nanilya thamani kwake.
Njoni kwake aliye jiwe hai linaloishi ambalo limekataliwa na watu, lakini hilo limechaguliwa na Mungu na ni la thamani kwake.
5 Na mwenga kati maliwe gagabile makoti gaga senge lwa kunani panga nyumba ya mwoyo ili panga ukuwani mtakatifu ambao ubuya sambi ya mwoyo, yai yekitilwa na Nn”ungu pitya Yesu Kristo.
Ninyi pia ni kama mawe yaliyo hai yanayojengwa juu kuwa nyumba ya kiroho, ili kuwa ukuhani mtakatifu ambao hutoa dhabihu za kiroho zinazokubaliwa kwa Mungu kupitia Yesu Kristo.
6 Lyandiko libaya nyanya, mm”lole nibii Sayuni liwe lya pabwega, likulo lya lisaulikwe na lya thamani. Ywoywoti ywamwobilya ywembe abona oni.
Andiko husema hivi, “Tazama, nimeweka katika Sayuni jiwe la pembeni, kuu na lililochaguliwa na la thamani. Yeyote aaminiye katika yeye hataona aibu”.
7 Kwa njo ishima yinu mwenga mwamuamini lakini liwe lyabalikani Babasenga leno lipangite liwe likulu lya pabwega.
Hivyo heshima ni yenu kwenu ninyi mnaoamini. Lakini, “jiwe lililokataliwa na wajenzi, hili limekuwa jiwe kuu la pembeni”-
8 Na “liwelyo kubala na mwamba wokubali” Bembe kubala, Babalikana neno kwa lilu lyalibile kai Batesauli kwa Bembe.
na, “jiwe la kujikwaa na mwamba wa kujikwaa.”Wao hujikwaa, wanaolikataa neno, kwa lile ambalo pia walikuwa wameteuliwa kwalo.
9 Kwa njo mwenga ni lukolo lwalu saulikwe na mpendo wa Kifalme, taifa, takatifu bandu ba miliki ya Nn”ungu ili pange muwese tangaza matendo ga ajabu ga yulu ywankemite buka mulubindu isa kwene mweya wa ajabu.
Lakini ninyi ni ukoo uliochaguliwa, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa miliki ya Mungu, ili kwamba mweze kutangaza matendo ya ajabu ya yule aliyewaita kutoka gizani kuja kwenye nuru yake ya ajabu.
10 Mwenga mwabile li mwa Bandu ba Nn”ungu li mwenga mupakile rehema.
Ninyi kwanza hamkuwa watu, lakini sasa ninyi ni watu wa Mungu. Ninyi hamkupokea rehema, lakini sasa mmepokea rehema.
11 Mwolongo nitekunkema kati mwageni mwaz bakwijima buka mwo jiga tamaa mbaya ya sambi, ambayo yendakubwana na ngodo ya mwoyo winu.
Wapendwa, nimewaita kama wageni na wazurujaji kujinyima kutoka kwenye tamaa mbaya za dhambi, ambazo zinapigana vita na roho zenu.
12 Mupalikwa mube na tabia safi buka mataifa ili kae mwana babalongela kita mupangite ikowe njapu, Buluwa bulanga kasi yinu sapi na kunumba Nn”ungu katika masoba go isa kwake.
Mnapaswa kuwa na tabia njema kati ya mataifa, ili kwamba, kama watawasema kama kwamba mmefanya mambo maovu, wataziangalia kazi zenu njema na kumsifu Mungu katika siku ya kuja kwake.
13 Muyikiti kila kilebe sa mundu kwa ajili ya Bwana abile kati mfalme nkulu,
Tii kila mamlaka ya mwanadamu kwa ajili ya Bwana, ikiwa mfalme kama mkuu,
14 ikapanga atawala babatumilwe kwa nkubwa baba panga ma chapu na kwapulaikya balu baba panga sapi.
ikiwa watawala waliotumwa kuwaadhibu watenda mabaya na kuwasifu wale wanaotenda mema.
15 Kwa njo mapenzi ya Nn”ungu, kwa panga sapi mwankanikiaya longela makowo ga kilalo kwa mandu achochi.
Kwa kuwa ni mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kufanya mema mwanyamazisha mazungumzo ya kipuuzi ya watu wapumbavu.
16 Mwana bandu bubile hunu, kwane matumihuru winu kati kiwikilyo cha ubou, basi mube kati mwabanda ba Nn”ungu.
Kama watu huru, msiutumie uhuru wenu kama kifuniko kwa maovu, bali muwe kama watumishi wa Mungu.
17 Mwaeshimu bandu boti, mwapende alongo, munjogope Nn”ungu, mumwesimu mfalme
Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mwogopeni Mungu. Mweshimuni mfalme.
18 Mwabanda mwayogofe mabwana binu kwa heshima yoti, siyo tu bwana yu sapi, mpole, lakini kai nanabile asapu.
Watumwa, watiini bwana zenu kwa heshima yote, siyo tu bwana walio wazuri na wapole, lakini pia walio waovu.
19 Kwa njo sifa kati yoyoti ywa vumilia lumya waka wateseka bila kilebe kwa sababu ya kumpala Nn”ungu.
Kwa kuwa ni sifa kama yeyote atavumilia maumivu wakati anapoteseka pasipo haki kwa sababu ya dhamiri yake kwa Mungu.
20 Kwina kilibe gani mwana mwenda dumu pamupanga sambi buka po mwendelipata azabu? Kwa njo mwana mupangile sapi naywa pata tabu kwo hukumiwa, yino ni sifa sapi kwa Nn”ungu.
Ni faida gani iliyopo kama mwadumu kutenda dhambi kisha mwendelee kuadhibiwa? Lakini kama mmefanya mema na ndipo mteseke kwa kuhukumiwa, hii ni sifa njema kwa Mungu.
21 Kwa lino mwatikemelwa kwa Kristo ywa tesike kwa ajili yitu, anekile mfano kwa ajili yinu kingama njayo yake.
Kwa hili mliitwa, kwa sababu Kristo pia aliteswa kwa ajili yenu, amewaachia mfano kwa ajili yenu kufuata nyayo zake.
22 Ywembe apangiteli sambi wala abone kineli konga munkano wake.
Yeye hakufanya dhambi, wala haukuonekana udanganyifu wowote kinywani mwake.
23 Wakati ywembe patukanilwe, akilibukieli tukana, hatishikeli ila atikwipaye mwene kwake ywembe ywa ukumu kwa haki.
Wakati yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano, alipoteseka, hakutisha bali alijitoa mwenyewe kwake Yeye ahukumuye kwa haki.
24 Ywembe mwene atiputwa sambi yitu payiga yake munkongo, ili kwamba kwane tube na pandu kai katika sambi na tutame kwa ajili ya haki. Kwo kumbulwa kwake twenga tuponi.
Yeye mwenyewe alizibeba dhambi zetu katika mwili wake kwenye mti, ili kwamba tusiwe na sehemu tena katika dhambi, na kwamba tuishi kwa ajili ya haki. Kwa kupigwa kwake ninyi mmepona.
25 Mwaboti mwamwabile kamuangaika kati ngondolo ywaobite, lakini sayino abuite kwa mchungaji na mlinzi wa mweyo winu.
Wote mliokuwa mkitangatanga kama kondoo aliyepotea, lakini sasa mmerudi kwa mchungaji na mlinzi wa roho zenu.

< 1 Petro 2 >