< Yohana 12 >

1 Siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alikwenda Bethania mahali ambako Lazaro aliyekuwa amefufuliwa na Yesu alikuwa anaishi.
Jesus, however, six days before the Passover, came to Bethany, where Lazarus was whom He had raised from the dead.
2 Wakaandaa karamu kwa heshima ya Yesu. Martha akawahudumia wakati Lazaro alikuwa miongoni mwa waliokaa mezani pamoja na Yesu.
So they gave a dinner there in honour of Jesus, at which Martha waited at table, but Lazarus was one of the guests who were with Him.
3 Kisha Maria akachukua chupa ya painti moja yenye manukato ya nardo safi ya thamani kubwa, akayamimina miguuni mwa Yesu na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato.
Availing herself of the opportunity, Mary took a pound weight of pure spikenard, very costly, and poured it over His feet, and wiped His feet with her hair, so that the house was filled with the fragrance of the perfume.
4 Ndipo Yuda Iskariote mwana wa Simoni, mmoja wa wale wanafunzi ambaye ndiye angemsaliti Yesu, akasema,
Then said Judas (the Iscariot, one of the Twelve--the one who afterwards betrayed Jesus),
5 “Kwa nini manukato haya hayakuuzwa kwa dinari 300 na fedha hizo wakapewa maskini?”
"Why was not that perfume sold for 300 shillings and the money given to the poor?"
6 Yuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali maskini, bali kwa kuwa alikuwa mwizi, kwani ndiye alikuwa akitunza mfuko wa fedha akawa anaiba kile kilichowekwa humo.
The reason he said this was not that he cared for the poor, but that he was a thief, and that being in charge of the money-box, he used to steal what was put into it.
7 Yesu akasema, “Mwacheni. Aliyanunua manukato hayo ili ayaweke kwa ajili ya siku ya maziko yangu.
But Jesus interposed. "Do not blame her," He said, "allow her to have kept it for the time of my preparation for burial.
8 Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.”
For the poor you always have with you, but you have not me always."
9 Umati mkubwa wa Wayahudi walipojua kwamba Yesu alikuwa huko Bethania, walikuja si tu kwa ajili ya Yesu, lakini pia kumwona Lazaro ambaye Yesu alikuwa amemfufua.
Now it became widely known among the Jews that Jesus was there; but they came not only on His account, but also in order to see Lazarus whom He had brought back to life.
10 Kwa hiyo viongozi wa makuhani wakafanya mpango wa kumuua Lazaro pia,
The High Priests, however, consulted together to put Lazarus also to death,
11 kwa kuwa kutokana na habari za kufufuliwa kwake Wayahudi wengi walikuwa wanamwendea Yesu na kumwamini.
for because of him many of the Jews left them and became believers in Jesus.
12 Siku iliyofuata umati mkubwa uliokuwa umekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Yesu angekuja Yerusalemu.
The next day a great crowd of those who had come to the Festival, hearing that Jesus was coming to Jerusalem,
13 Basi wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema, “Hosana!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!” “Amebarikiwa Mfalme wa Israeli!”
took branches of the palm trees and went out to meet Him, shouting as they went, "God save him! Blessings on him who comes in the name of the Lord--even on the King of Israel!"
14 Yesu akamkuta mwana-punda akampanda, kama ilivyoandikwa,
And Jesus, having procured a young ass, sat upon it, just as the Scripture says,
15 “Usiogope, Ewe binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda!”
"Fear not, Daughter of Zion! See, thy King is coming riding on an ass's colt."
16 Wanafunzi wake Yesu mwanzoni hawakuelewa mambo haya, lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka kuwa mambo haya yalikuwa yameandikwa kwa ajili yake na alitendewa yeye.
The meaning of this His disciples did not understand at the time; but after Jesus was glorified they recollected that this was written about Him, and that they had done this to Him.
17 Wale waliokuwepo wakati Yesu alipomwita Lazaro kutoka kaburini na kumfufua kutoka kwa wafu, waliendelea kushuhudia.
The large number of people, however, who had been present when He called Lazarus out of the tomb and brought him back to life, related what they had witnessed.
18 Ni kwa sababu pia walikuwa wamesikia kwamba alikuwa ametenda muujiza huu ndiyo maana umati wa watu ukaenda kumlaki.
This was also why the crowd came to meet Him, because they had heard of His having performed that miracle.
19 Hivyo Mafarisayo walipoona hayo wakaambiana, “Mnaona, hamwezi kufanya lolote. Angalieni, ulimwengu wote unamfuata yeye!”
The result was that the Pharisees said among themselves, "Observe how idle all your efforts are! The world is gone after him!"
20 Basi palikuwa Wayunani fulani miongoni mwa wale waliokuwa wamekwenda kuabudu wakati wa Sikukuu.
Now some of those who used to come up to worship at the Festival were Greeks.
21 Hawa wakamjia Filipo, ambaye alikuwa mwenyeji wa Bethsaida huko Galilaya, wakiwa na ombi. Wakamwambia, “Tungependa kumwona Yesu.”
They came to Philip, of Bethsaida in Galilee, with the request, "Sir, we wish to see Jesus."
22 Filipo akaenda akamweleza Andrea, nao wote wawili wakamwambia Yesu.
Philip came and told Andrew: Andrew and Philip told Jesus.
23 Yesu akawajibu, “Saa imewadia ya Mwana wa Adamu kutukuzwa.
His answer was, "The time has come for the Son of Man to be glorified.
24 Amin, amin nawaambia, mbegu ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, hubakia kama mbegu peke yake. Lakini ikifa huzaa mbegu nyingi.
In most solemn truth I tell you that unless the grain of wheat falls into the ground and dies, it remains what it was--a single grain; but that if it dies, it yields a rich harvest.
25 Mtu yeyote anayependa maisha yake atayapoteza, naye ayachukiaye maisha yake katika ulimwengu huu atayaokoa hata kwa uzima wa milele. (aiōnios g166)
He who holds his life dear, is destroying it; and he who makes his life of no account in this world shall keep it to the Life of the Ages. (aiōnios g166)
26 Mtu yeyote akinitumikia lazima anifuate, nami mahali nilipo ndipo mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu akinitumikia, Baba yangu atamheshimu.
If a man wishes to be my servant, let him follow me; and where I am, there too shall my servant be. If a man wishes to be my servant, the Father will honour him.
27 “Sasa roho yangu imefadhaika sana. Niseme nini? ‘Baba, niokoe katika saa hii.’ Lakini ni kwa kusudi hili nimeufikia wakati huu.
Now is my soul full of trouble; and what shall I say? Father, save me from this hour. But for this purpose I have come to this hour.
28 Baba, litukuze jina lako.” Ndipo ikaja sauti kutoka mbinguni, “Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.”
Father, glorify Thy name." Thereupon there came a voice from the sky, "I have glorified it and will also glorify it again."
29 Ule umati wa watu uliokuwa mahali pale uliisikia nao ukasema, “Hiyo ni sauti ya radi,” wengine wakasema, “Malaika ameongea naye.”
The crowd that stood by and heard it, said that there had been thunder. Others said, "An angel spoke to him."
30 Yesu akawaambia, “Sauti hii imesikika kwa faida yenu, wala si kwa faida yangu.
"It is not for my sake," said Jesus, "that that voice came, but for your sakes.
31 Sasa ni saa ya hukumu kwa ajili ya ulimwengu huu, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje.
Now is a judgement of this world: now will the Prince of this world be driven out.
32 Lakini mimi, nikiinuliwa kutoka nchi, nitawavuta watu wote waje kwangu.”
And I-- if I am lifted up from the earth--will draw all men to me."
33 Yesu aliyasema haya akionyesha ni kifo gani atakachokufa.
He said this to indicate the kind of death He would die.
34 Ule umati wa watu ukapiga kelele ukasema, “Tumesikia kutoka Sheria kwamba ‘Kristo adumu milele,’ wewe wawezaje kusema, ‘Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu’? Huyu ‘Mwana wa Adamu’ ni nani?” (aiōn g165)
The crowd answered Him, "We have heard out of the Law that the Christ remains for ever. In what sense do you say that the Son of Man must be lifted up? Who is that Son of Man?" (aiōn g165)
35 Ndipo Yesu akawaambia, “Bado kitambo kidogo nuru ingalipo pamoja nanyi. Enendeni maadamu mna nuru, msije mkakumbwa na giza. Mtu anayetembea gizani hajui anakokwenda.
"Yet a little while," He replied, "the light is among you. Be faithful to the light that you have, for fear darkness should overtake you; for a man who walks in the dark does not know where he is going.
36 Wekeni tumaini lenu katika nuru hiyo ili mpate kuwa wana wa nuru.” Baada ya kusema haya, Yesu aliondoka, akajificha wasimwone.
In the degree that you have light, believe in the Light, so that you may become sons of Light." Jesus said this, and went away and hid Himself from them.
37 Hata baada ya Yesu kufanya miujiza hii yote mbele yao, bado hawakumwamini.
But though He had performed such great miracles in their presence, they did not believe in Him--
38 Hili lilikuwa ili kutimiza lile neno la nabii Isaya lililosema: “Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu, na mkono wa Bwana umefunuliwa kwa nani?”
in order that the words of Isaiah the Prophet might be fulfilled, "Lord, who has believed our preaching? And the arm of the Lord--to whom has it been unveiled?"
39 Kwa hivyo hawakuamini, kwa sababu Isaya anasema mahali pengine:
For this reason they were unable to believe--because Isaiah said again,
40 “Amewafanya vipofu, na kuifanya mioyo yao kuwa migumu, ili wasiweze kuona kwa macho yao, wala kuelewa kwa mioyo yao, wasije wakageuka nami nikawaponya.”
"He has blinded their eyes and made their minds callous, lest they should see with their eyes and perceive with their minds, and should turn, and I should heal them."
41 Isaya alisema haya alipoona utukufu wa Yesu na kunena habari zake.
Isaiah uttered these words because he saw His glory; and he spoke of Him.
42 Lakini wengi miongoni mwa viongozi wa Wayahudi walimwamini, lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakukiri waziwazi kwa maana waliogopa kufukuzwa katika masinagogi.
Nevertheless even from among the Rulers many believed in Him. But because of the Pharisees they did not avow their belief, for fear they should be shut out from the synagogue.
43 Wao walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu.
For they loved the glory that comes from men rather than the glory that comes from God.
44 Yesu akapaza sauti akasema, “Yeyote aniaminiye, haniamini mimi peke yangu, bali yeye aliyenituma.
But Jesus cried aloud, "He who believes in me, believes not so much in me, as in Him who sent me;
45 Yeyote anionaye mimi, amemwona yeye aliyenituma.
and he who sees me sees Him who sent me.
46 Mimi nimekuja kama nuru ulimwenguni, ili kwamba kila mtu aniaminiye asibaki gizani.
I have come like light into the world, in order that no one who believes in me may remain in the dark.
47 “Mimi simhukumu mtu yeyote anayesikia maneno yangu na asiyatii, kwa maana sikuja kuuhukumu ulimwengu, bali kuuokoa.
And if any one hears my teachings and regards them not, I do not judge him; for I did not come to judge the world, but to save the world.
48 Yuko amhukumuye yeye anikataaye mimi na kutokuyapokea maneno yangu, yaani, yale maneno niliyosema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho.
He who sets me at naught and does not receive my teachings is not left without a judge: the Message which I have spoken will judge him on the last day.
49 Kwa maana sisemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba aliyenituma aliniamuru ni nini cha kusema na jinsi ya kukisema.
Because I have not spoken on my own authority; but the Father who sent me, Himself gave me a command what to say and in what words to speak.
50 Nami ninajua amri zake huongoza hadi kwenye uzima wa milele. Hivyo lolote nisemalo, ndilo lile Baba aliloniambia niseme.” (aiōnios g166)
And I know that His command is the Life of the Ages. What therefore I speak, I speak just as the Father has bidden me." (aiōnios g166)

< Yohana 12 >