< 1 Yohana 5 >

1 Yeyoteb ywaaminiya kuwa Kristo abelekwile na Nnongo. Na yeyote ywampenda ywembe ambaye aboka kwa Tate ubapenda bana bake.
Yeyote anayeamini kuwa Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na yeyote ampendaye yeye ambaye ametoka kwa Baba pia huwapenda watoto wake.
2 Kwa lee tutangite panga twawapenda bana ba Nnongo-patumpendile Nnongo na kuipanga amri yake.
Kwa hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu — tunapompenda Mungu na kutekeleza amri zake.
3 Ayee nga namna ya kumpenda Nnongo panga twazikamwa amri zake. Na amri zake ni nyepesi.
Hivi ndivyo tunavyompenda Mungu kwamba twazishika amri zake. Na amri zake ni nyepesi.
4 Kwa kuwa kila ywabelekilwe na Nnongo huushinda ulimwengu. Na wolo nga ushindi wa kuushinda ulimwengu, imani yitu.
Kwa kuwa kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Na huu ndio ushindi wa kuushinda ulimwengu, imani yetu.
5 Ni nyai ywaushinda ulimwengu? Na yolo ywaaminiye panga Yesu ni Mwana wa Nnongo.
Ni nani aliyeushinda ulimwengu? Ni yule aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.
6 Ayee nga ywaisile kwa mase na myai-Yesu Kristo. Aisa kwaa tu kwa mase ila kwa mase na myai.
Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu- Yesu Kristo. Hakuja tu kwa maji bali kwa maji na damu.
7 Kwa mana babile atatu bashuhudiao:
Kwa kuwa kuna watatu washuhudiao:
8 Roho, mase na myai. Haba atatu uyeketyana. Zingatia: Maneno aga “Tate, Neno, na Roho Mtakatifu” yabonekania kwaa katika nakala bora za kale)
Roho, maji na damu. Hawa watatu hukubaliana. (Zingatia: Maneno haya “Baba, Neno, na Roho Mtakatifu” hayaonekani katika nakala bora za kale).
9 Mana twapokya ushuhuda wa bandu ba Nnongo ni nkolo kuliko wolo. Kwa mana ushuhuda wa Nnongo ni wolo-panga abile na ushuhuda kuhusiana na mwana wake.
Kama tunaupokea ushuhuda wa wanadamu ushuhuda wa Mungu ni mkuu kuliko huo. Kwa kuwa ushuhuda wa Mungu ni huu- kwamba anao ushuhuda kuhusiana na Mwanawe.
10 Ywembe ywamwaminiye mwana wa Nnongo abile na ushuhuda nkati yake mwene. Na yeyote ywaamwiniya kwaa Nnongo ampangite kuwa mbocho, kwa mana aaminiya kwaa ushuhuda ambao Nnongo atiuleta kuhusu mwana wake.
Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu ana ushuhuda ndani yake mwenyewe. Na yeyote asiye mwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini ushuhuda ambao Mungu ameuleta kuhusu Mwanawe.
11 Na ushuhuda nga wolo-panga Nnongo atupeile ukoto wa milele, na ukoto ubile nkati ya mwana wake. (aiōnios g166)
Na ushuhuda ndio huu — kwamba Mungu alitupa uzima wa milele, na uzima huu umo ndani ya Mwanawe. (aiōnios g166)
12 Ywabile nae mwana abile na ukoto. Ywabile kwaa naywembe Mwana wa Nnongo abile nkoto.
Aliye naye Mwana ana uzima. Asiyekuwa naye Mwana wa Mungu hana uzima.
13 Natiwaandikia aga muweze kutanga panga mubile na ukoto wa milele-mwenga mwamuaminiya katika lina lya Mwana wa Nnongo. (aiōnios g166)
Nimewaandikia haya mweze kujua kwamba mnao uzima wa milele — ninyi mnaoamini katika jina la Mwana wa Mungu. (aiōnios g166)
14 Na wolo nga ujasiri tubile nao nnongi yake, panga mana tukiloba kilebe chochote sawa sawa na mapenzi gake, hutusikia-
Na huu ndio ujasiri tulionao mbele zake, kwamba kama tukiomba kitu chochote sawa sawa na mapenzi yake, hutusikia.
15 Na mana tutangite panga hutupekania-chochote cha tukiloba kwake tutangite panga hutupekania panga tubile nacho hicho chatumlobite.
Na kama tunajua kwamba hutusikia — chochote tumwombacho tunajua kwamba tunacho hicho tulichomwomba.
16 Mana mundu ywanloba nongowe atenda sambi yapelekea kwa kiwo, apalikwa kuloba na Nnongo alowa kumpeya ukoto. Nalongela kwa balo ambao sambi yabe ni yelo yaipelekea kwaa kiwo-pabile na sambi yaipelekea kiwo-nilongela kwaa panga apalikwa kuloba kwa ajili ya sambi yee.
Kama mtu amwonaye ndugu yake anatenda dhambi isiyopelekea kifo, yampasa kuomba na Mungu atampa uzima. Ninasema kwa wale ambao dhambi yao ni ile isiyopelekea kifo — Kuna dhambi ipelekeayo kifo — sisemi kwamba anapaswa kuomba kwa ajilli ya dhambi hiyo.
17 Uasi wote ni sambi-lakini pabile na sambi yaipelekea kwaa kiwo.
Uasi wote ni dhambi — lakini kuna dhambi isiyopelekea kifo.
18 Tutangite ya kuwa ywabelekilwe na Nnongo apanga kwaa sambi. Ila ywabelekilwe na Nnongo hutunzwa naywembe salama daima, na yolo nchela aweza kwaa kumdhuru.
Tunajua ya kuwa aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi. Bali aliyezaliwa na Mungu hutunzwa naye salama daima, na yule mwovu hawezi kumdhuru.
19 Tutangite panga twenga ni wa Nnongo na tutangite panga ulimwengu wote ubile pae ya utawala wa yolo nchela.
Tunajua kuwa sisi ni wa Mungu na tunajua kwamba ulimwengu wote uko chini ya utawala wa yule mwovu.
20 Lakini tutangite panga Mwana wa Nnongo aisile na atupeya ujuzi, panga tuntangite ywembe ywabile mu kweli na panga tubile nkati yake ywembe ywabile kweli, hata katika mwana wake Yesu Kristo. Ni Nnongo wa kweli na ukoto wa milele. (aiōnios g166)
Lakini twajua kwamba Mwana wa Mungu amekuja na ametupatia ujuzi, kwamba tunamjua yeye aliye kweli na kwamba tumo ndani yake yeye aliye kweli, hata katika Mwanawe Yesu Kristo. Ni Mungu wa kweli na uzima wa milele. (aiōnios g166)
21 Bana apenzi, mujiepushe na sanamu.
Watoto wapenzi, jiepusheni na sanamu.

< 1 Yohana 5 >