< 1 Akoritho 1 >

1 Paulo ywakemilwe ni Kristo pangika Mtume kwa mapenzi ga Nnongo, ni Sosthene nnuna witu.
Paulo, aliyeitwa na Kristo Yesu kuwa mtume kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu,
2 Kwa likanisa lya Nnongo lyalibile Korintho, kwa balo ambabo babekilwe wakfu mu Yesu Kristo, babakemilwe panga bandu atakatifu twaandikya kae balo boti babakema lina lya Ngwana witu Yesu Kristo mahali palo, Ngwana wabe ni witu.
kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, kwa wale ambao wamewekwa wakfu katika Yesu Kristo, ambao wameitwa kuwa watu watakatifu. Tunawaandikia pia wale wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo katika mahali pote, Bwana wao na wetu.
3 Neema na amani ibe kwinu buka kwa Nnongo tate bitu ni Ngwana witu Yesu Kristo.
Neema na amani iwe kwenu kutoka kwa Mungu baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo.
4 Masoba gote nimsukuru Nnongo wango kwa ajili yinu, kwa sababu ya neema ya Nnongo ywabile awapeile Yesu Kristo.
Siku zote namshukru Mungu wangu kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu ambayo Kristo Yesu aliwapa.
5 Abapangite kuwa matajiri mu'kila ndela, katika longela pamope maarifa gake.
Amewafanya kuwa matajiri katika kila njia, katika usemi na pamoja maarifa yote.
6 Abapangite matajiri, kati ushuhuda kuhusu Kristo wautithibitisha kuwa kweli nkati yinu.
Amewafanya matajiri, kama ushuhuda kuhusu Kristo ya kwamba amethibitishwa kuwa kweli miongoni mwenu.
7 Kwa eyo ipungwa kwaa karama ya kiroho, kati samubile na kilulu so kuulinda ufunuo wa Ngwana witu Yesu Kristo.
Kwa hiyo hampungukiwi karama za kiroho, kama mlivyo na hamu ya kusubiri ufunuo wa Bwana wetu Yesu Kristo.
8 Alowa kumwimarisha mwenga mpaka mwisho, ili kana mukaumilwe lisoba lya Ngwana witu Yesu Kristo.
Atawaimarisha ninyi pia hadi mwisho, ili msilaumiwe siku ya Bwana wetu Yesu Kristo.
9 Nnongo ni mwaminifu ywabile abakemile mwenga mu'ushirika wa mwana wake, Yesu Kristo Ngwana witu.
Mungu ni mwaminifu ambaye aliwaita ninyi katika ushirika wa mwana wake, Yesu Kristo Bwana wetu.
10 Nambeambe niasihi mwainja ni numbwango, pitya lina lya Ngwana witu Yesu Kristo, panga mwabote muyikityange, ni panga kana kube ni banganika nkati yinu. Niasihi muungane pamope mu'nia jimo.
Sasa nawasihi kaka na dada zangu, kupitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba wote mkubali, na kwamba kusiwe na migawanyiko miongoni mwenu. Nawasihi kwamba muungane pamoja katika nia moja na katika kusudi moja.
11 Mana bandu ba nyumba ya Kloe batumakiye kuwa kubile ni banganika nkati yinu.
Kwani watu wa nyumba ya Kloe wamenitaarifu kuwa kuna mgawanyiko unaoendelea miongoni mwenu.
12 Nibile na mana yee: Kila yumo abaya “nenga na ywaa Paulo”, au “nenga ni ywaa Apolo,” au nenga nI ba Kefa” au “nenga ni wa Kristo.”
Nina maana hii: Kila mmoja wenu husema, “Mimi ni wa Paulo,” au “Mimi ni wa Apolo”, au “Mimi ni wa Kefa” au “Mimi ni wa Kristo”.
13 Je! Kristo atebanganika? Je Paulo atisulubilwa kwaajili yinu? Je! mwatibatizwa kwa lina lya Paulo?
Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulubiwa kwa ajili yenu? Je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?
14 Nenda kumshukuru Nnongo kuwa nimbatiliza kwaa yeyete, ila Krispo ni Gayo.
Namshukuru Mungu kuwa sikumbatiza yeyote, isipokuwa Krispo na Gayo.
15 Yee yabile panga ntopo ywoywoti aweza baya mwabatizwa kwa lina lyango.
Hii ilikuwa kwamba hakuna yeyote angesema mlibatizwa kwa jina langu.
16 (Pia natekuabatiza ba nyumba ya Sephania. Zaidi ya palo, nitangite kwaa kati nambatiza mundu ywenge yeyote).
(Pia niliwabatiza wa nyumba ya Stephania. Zaidi ya hapo, sijui kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote).
17 Kwa kuwa, Kristo antumile kwaa batiza ila ubili injili. Antumile longela kwa maneno ga ekima ya kimundu, ili panga ngupu ya msalaba wa Kristo kana ubuke.
Kwa kuwa, Kristo hakunituma kubatiza bali kuhubiri injili. Hakunituma kuhubiri kwa maneno ya hekima ya kibinadamu, ili kwamba nguvu ya msalaba wa Kristo isiondolewe.
18 Kwa kuwa ujumbe wa msalaba ni upuuzi kwa balo batiwaa. Lakini kwa balo ambabo Nnongo atikwalopwa, ni ngupu ya Nnongo.
Kwa kuwa ujumbe wa msalaba ni upuuzi kwa wale wanaokufa. Lakini kwa wale ambao Mungu anawaokoa, ni nguvu ya Mungu.
19 Kwa kuwa iandikilwe, “Nalowa kuiharibu hekima ya ywabile ni busara. Nalowa kuuharibu ufahamu wa babile ni malango.”
Kwa kuwa imeandikwa, “Nitaiharibu hekima ya wenye busara. Nitauharibu ufahamu wa wenye akili.”
20 Abile kwako mundu ywabile ni busara? ywabile kwako ywabile ni elimu? ywabile kwako ywabaya nga mshawishi wa dunia yee? Je Nnongo aigalambwile kwaa hekima ya dunia yee no pangika ulalo? (aiōn g165)
Yuko wapi mtu mwenye busara? Yuko wapi mwenye elimu? Yuko wapi msemaji mshawishi wa dunia hii? Je, Mungu hakuigeuza hekima ya dunia hii kuwa ujinga? (aiōn g165)
21 Buka dunia ipangika mu'hekima yake intangite kwaa Nnongo, impendeza kwaa Nnongo mu'ulalo wabe wa hubiri ili kubalopwa balo baaminiya.
Tangu dunia imekuwa katika hekima yake haikumjua Mungu, ilimpendeza Mungu katika ujinga wao wa kuhubiri ili kuokoa wale wanaoamini.
22 Kwa Ayahudi kulokiya ishara ya miujiza ni kwa Ayunani upala hekima.
Kwa Wayahudi huuliza ishara za miujiza na kwa Wayunani hutafuta hekima.
23 Lakini tumuhubiri Kristo ywaatisulubilwa, ywabile kikwazo kwa Ayahudi na nga ulalo kwa Ayunani.
Lakini tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa, aliye kikwazo kwa Wayahudi na ni ujinga kwa Wayunani.
24 Lakini kwa balo babakemile ni Nnongo, Ayahudi ni Ayunani, twamuhubiri Kristo kati ngupu ni hekima ya Nnongo.
Lakini kwa wale ambao waliitwa na Mungu, Wayahudi na Wayunani, tunamhubiri Kristo kama nguvu na hekima ya Mungu.
25 Kwa kuwa ulalo wa Nnongo wabile ni hekima kuliko ya bandu, ni udhaifu wa Nnongo wabile ni ngupu kuliko ya bandu.
Kwa kuwa ujinga wa Mungu una hekima kuliko ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.
26 Lola wito wa Nnongo nnani yinu, ainja ni nnumbwa ngo. Ni baingi kwaa nkati yinu mwabile ni hekima mu'viwango vya bandu. Ni baingi kwa nkati yinu mwabile ni ngupu. baingi kwaa nkati yinu mubelekwi mu ukolo.
Angalia wito wa Mungu juu yenu, kaka na dada zangu. Si wengi wenu mlikuwa na hekima katika viwango vya kibinadamu. Si wengi wenu mlikuwa na nguvu. Si wengi wenu mlizaliwa katika ukuu.
27 Lakini Nnongo asawile ile ya kilalo ya dunia ili kwiaibisha yabile ni hekima. Nnongo asawile sa'kinyatike mu'dunia kukiabisha sa kibile ni ngupu.
Lakini Mungu alichagua vitu vijinga vya dunia ili kuviaibisha vyenye hekima. Mungu alichagua kilicho dhaifu katika dunia kukiaibisha chenye nguvu.
28 Nnongo asawile chelo cha hali ya pae ni chabile chakisalaulilwe mu'dunia. Asawile ata ilebe ambayo yabalangilwe kwaa pangika ilebe, kwa kuipanga ilebe kwaa yabile ni yhamani.
Mungu alichagua kile kilicho cha hali ya chini na kilichodharauliwa katika dunia. Alichagua hata vitu ambavyo havikuhesabiwa kuwa kitu, kwa kuvifanya si kitu vitu vilivyo na thamani.
29 Apangite nyoo ili kana abe yeyote ywabile ni sababu ya kuipunia nnonge yake.
Alifanya hivi ili asiwepo yeyote aliye na sababu ya kujivuna mbele zake.
30 Kwa sababu ya chelo chaakipangite Nnongo, nambeambe mubile nkati ya Kristo Yesu, ywabile apangike hekima kwa ajili yinu kuoma kwa Nnongo. Abile nga haki yitu, utakatifu ni ukombozi.
Kwa sababu ya kile Mungu alichofanya, sasa mko ndani ya Kristo Yesu, ambaye amefanyika hekima kwa ajili yetu kutoka kwa Mungu. Alikuwa haki yetu, utakatifu na ukombozi.
31 Kati matokeo, kati liandiko lyatibaya, “Ywaisipu, aisipu mu'Nngwana.”
Kama matokeo, kama andiko lisemavyo, “Anayejisifu, ajisifu katika Bwana.”

< 1 Akoritho 1 >