< Galatians 4 >

1 Now I say, [That] the heir, as long as he is a child, differeth nothing from a servant, though he is lord of all;
Ninasema kwamba maadamu mrithi ni mtoto, hana tofauti na mtumwa, hata ingawa ni mmiliki wa mali yote.
2 But is under tutors and governors until the time appointed by the father.
Badala yake, yuko chini ya waangalizi na wadhamini mpaka wakati uliowekwa na baba yake.
3 Even so we, when we were children, were in bondage under the elements of the world:
Kadhalika pia na sisi, tulipokuwa watoto, tulishikiliwa katika utumwa wa kanuni za kwanza za ulimwengu.
4 But when the fullness of the time was come, God sent forth his Son, born of a woman, born under the law,
Lakini wakati sahihi ulipofika, Mungu alimtuma mwanawe, mzaliwa wa mwanamke, mzaliwa chini ya sheria.
5 To redeem them that were under the law, that we might receive the adoption of sons.
Alifanya hivi ili kuwakomboa wale waliokuwa chini ya sheria, ili kwamba tupokee hali ya kuwa kama wana.
6 And because ye are sons, God hath sent forth the Spirit of his Son into your hearts, crying, Abba, Father.
Kwa sababu ninyi ni wana, Mungu alimtuma Roho wa mwanawe ndani ya mioyo yetu, Roho aitaye, “Abba, Baba.”
7 Wherefore thou art no more a servant, but a son; and if a son, then an heir of God through Christ.
Kwa sababu hii wewe si mtumwa tena bali mwana. Kama ni mwana, basi wewe pia ni mrithi kupitia Mungu.
8 However then, when ye knew not God, ye did service to them which by nature are no gods.
Hata kabla, wakati hamkumjua Mungu, mlikuwa watumwa kwa wale ambao kwa asili si miungu kabisa.
9 But now, after ye have known God, or rather are known by God, how turn ye again to the weak and beggarly elements, to which ye desire again to be in bondage?
Lakini sasa kwamba mnamjua Mungu, au kwamba mnajulikana na Mungu, kwa nini mnarudi tena kwenye kanuni dhaifu za kwanza na zisizo za thamani? Je mnataka kuwa watumwa tena?
10 Ye observe days, and months, and times, and years.
Mnashika kwa uangalifu siku maalumu, miandamo ya miezi, majira, na miaka. Ninaogopa kwa ajili yenu.
11 I am afraid of you, lest I have bestowed upon you labor in vain.
Ninaogopa kwamba kwa namna fulani nimejitaabisha bure.
12 Brethren, I beseech you, be as I am; for I [am] as ye [are]: ye have not injured me at all.
Ninawasihi, ndugu, muwe kama nilivyo, kwa kuwa pia nimekuwa kama mlivyo. Hamkunikosea.
13 Ye know that in infirmity of the flesh I preached the gospel to you at the first.
Bali mnajua kwamba ilikuwa ni kwa sababu ya ugonjwa wa mwili kwamba nilihubiri injili kwenu kwa mara ya kwanza.
14 And my temptation which was in my flesh ye despised not, nor rejected; but received me as an angel of God, [even] as Christ Jesus.
Ingawa hali yangu ya mwili iliwaweka katika jaribu, hamkunidharau au kunikataa. Badala yake mlinipokea kama malaika wa Mungu, kana kwamba nilikuwa Kristo Yesu mwenyewe.
15 What then was the blessedness ye spoke of; for I bear you testimony, that, if [it had been] possible, ye would have plucked out your own eyes, and have given them to me.
Kwa hiyo, iko wapi sasa furaha yenu? kwa kuwa ninashuhudia kwenu kwamba, ikiwezekana, mungelin'goa macho yenu na kunipa mimi.
16 Am I therefore become your enemy because I tell you the truth?
Hivyo sasa, je nimekuwa adui yenu kwa sababu ninawaambia ukweli?
17 They zealously affect you, [but] not well; for, they would exclude you, that ye may affect them.
Wanawatafuta kwa shauku, bali si kwa mema. Wanataka kuwatenganisha ninyi na mimi ili muwafuate.
18 But [it is] good to be zealously affected always in [a] good [thing], and not only when I am present with you.
Ni vyema daima kuwa na shauku kwa sababu zilizo njema, na si tu wakati ninapokuwa pamoja nanyi.
19 My little children, of whom I travail in birth again, until Christ be formed in you,
Wanangu wadogo, ninaumwa uchungu kwa ajili yenu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu.
20 I desire to be present with you now, and to change my voice; for I stand in doubt of you.
Ningependa kuwepo pale pamoja nanyi sasa na kugeuza sauti yangu, kwa sababu ninamashaka juu yenu.
21 Tell me, ye that desire to be under the law, do ye not hear the law?
Niambieni, ninyi ambao mnatamani kuwa chini ya sheria, hamsikii sheria isemavyo?
22 For it is written, that Abraham had two sons; the one by a bond-maid, the other by a free-woman.
Kwa kuwa imeandikwa kwamba Abrahamu alikuwa na wana wa kiume wawili, mmoja kwa yule mwanamke mtumwa na mwingine kwa mwanamke huru.
23 But he [who was] of the bond-woman, was born according to the flesh; but he of the free-woman [was] by promise.
Hata hivyo, yule wa mtumwa alizaliwa kwa mwili tu, bali yule wa mwanamke huru alizaliwa kwa ahadi.
24 Which things are an allegory: for these are the two covenants; the one from the mount Sinai, which gendereth to bondage, which is Agar.
Mambo haya yanaweza kuelezwa kwa kutumia mfano, kwa kuwa wanawake hawa wanafanana na maagano mawili. Mojawapo kutoka katika mlima Sinai. Huzaa watoto ambao ni watumwa. huyu ni Hajiri.
25 For this Agar is mount Sinai in Arabia, and answereth to Jerusalem which now is, and is in bondage with her children.
Sasa Hajiri ni mlima Sinai ulioko Arabuni. Hufananishwa na Yerusalem ya sasa, kwa kuwa ni mtumwa pamoja na watoto wake.
26 But Jerusalem which is above is free, which is the mother of us all.
Bali Yerusalemu ambayo iko juu ni huru, na hii ndiyo mama yetu.
27 For it is written, Rejoice, [thou] barren that bearest not; break forth and cry, thou that travailest not: for the desolate hath many more children than she who hath a husband.
Kwa kuwa imeandikwa, “Furahi, wewe mwanamke uliye tasa, wewe usiye zaa. Paza sauti na upige kelele kwa furaha, wewe ambaye huna uzoefu wa kuzaa. kwa maana wengi ni watoto wa aliye tasa, zaidi ya wale wa yule ambaye ana mume.”
28 Now we, brethren, as Isaac was, are the children of promise.
Sasa ndugu, kama Isaka, ninyi ni watoto wa ahadi.
29 But as then he that was born according to the flesh persecuted him [that was born] according to the Spirit, even so [it is] now.
Kwa wakati ule ambao mtu ambaye alizaliwa kwa mujibu wa mwili alimtesa yule aliyezaliwa kwa mujibu wa Roho. Kwa sasa ni vilevile.
30 Nevertheless, what saith the scripture? Cast out the bond-woman and her son: for the son of the bond-woman shall not be heir with the son of the free-woman.
Maandiko husemaje? “Muondoe mwanamke mtumwa pamoja na mwanawe wa kiume. Kwa kuwa mtoto wa mwanamke mtumwa hatarithi pamoja na mtoto wa mwanamke huru.”
31 So then, brethren, we are not children of the bond-woman, but of the free.
Kwa hiyo, ndugu, sisi si watoto wa mwanamke mtumwa, bali ni wa mwanamke huru.

< Galatians 4 >