< Romans 13 >

1 Let every soule submit him selfe vnto the auctorite of ye hyer powers. For there is no power but of God.
Kila nafsi na iwe na utii kwa mamlaka ya juu, kwa kuwa hakuna mamlaka isipokuwa imetoka kwa Mungu. Na mamlaka zilizopo zimewekwa na Mungu.
2 The powers that be are ordeyned of God. Whosoever therfore resysteth power resisteth the ordinaunce of God. And they that resist shall receave to the selfe damnacio.
Kwa hiyo ambaye anapinga mamlaka hiyo hupinga amri ya Mungu; na wale waipingao watapokea hukumu juu yao wenyewe.
3 For rulars are not to be feared for good workes but for evyll Wilt thou be with out feare of the power? Do well then: and so shalt thou be praysed of the same.
Kwa kuwa watawala si tishio kwa watendao mema, bali kwa watendao maovu. Je unatamani kutoogopa mamlaka? Fanya yaliyo mema, na utasifiwa nayo.
4 For he is the minister of God for thy welth. But and yf thou do evyll then feare: for he beareth not a swearde for nought: but is the minister of God to take vengeaunce on them that do evyll.
Kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Bali kama utatenda yaliyo maovu, ogopa; kwa kuwa habebi upanga bila sababu. Kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, mlipa kisasi kwa ghadhabu juu ya yule afanyaye uovu.
5 Wherfore ye must nedes obeye not for feare of vengeaunce only: but also because of conscience.
Kwa hiyo inakupasa utii, si tu kwa sababu ya gadhabu, bali pia kwa sababu ya dhamiri.
6 And even for this cause paye ye tribute. For they are goddes ministers servynge for the same purpose.
Kwa ajili hii pia unalipa kodi. Kwa kuwa wenye mamlaka ni watumishi wa Mungu, ambao wanaendelea kufanya jambo hili.
7 Geve to every man therfore his duetie: Tribute to whom tribute belongeth: Custome to whom custome is due: feare to whom feare belongeth: Honoure to who honoure pertayneth
Mlipeni kila mmoja ambacho wanawadai: kodi kwa astahiliye kodi; ushuru kwa astahiliye ushuru; hofu kwa astahiliye hofu; heshima kwa astahiliye heshima.
8 Owe nothinge to eny man: but to love one another. For he that loveth another fulfylleth the lawe.
Msidaiwe na mtu kitu chochote, isipokuwa kupendana ninyi kwa ninyi. Kwa kuwa yeye ampendaye jirani yake ametimiliza sheria.
9 For these commaundementes: Thou shalt not comit advoutry: Thou shalt not kyll: Thou shalt not steale: Thou shalt not beare false witnes: Thou shalt not desyre and so forth (yf there be eny other comaundement) they are all comprehended in this sayinge: Love thyne neghbour as thy selfe.
Kwa kuwa, “Hautazini, hautaua, hautaiba, hautatamani,” na kama kuna amri nyingine pia, imejumlishwa katika sentensi hii: “Utampenda jirani yako kama wewe mwenyewe.”
10 Love hurteth not his neghbour. Therfore is love the fulfillynge of the lawe.
Upendo hamdhuru jirani wa mtu. Kwa hiyo, upendo ni ukamilifu wa sheria.
11 This also we knowe I mean the season howe that it is tyme that we shuld now awake oute of slepe. For now is oure salvacion nearer then when we beleved.
Kwa sababu ya hili, mnajua wakati, kwamba tayari ni wakati wa kutoka katika usingizi. Kwa kuwa wokovu wetu umekaribia zaidi ya wakati ule tulio amini kwanza.
12 The nyght is passed and the daye is come nye. Let us therfore cast awaye the dedes of darcknes and let vs put on the (Armoure) of lyght.
Usiku umeendelea, na mchana umekaribia. Na tuweke pembeni matendo ya giza, na tuvae silaha za nuru.
13 Let vs walke honestly as it were in the daye lyght: not in eatynge and drinkynge: nether in chamburynge and wantannes: nether in stryfe and envyinge:
Na tuenende sawa sawa, kama katika nuru, si kwa sherehe za uovu au ulevi. Na tusienende katika zinaa au tamaa isiyoweza kudhibitiwa, na si katika fitina au wivu.
14 but put ye on the Lorde Iesus Christ. And make not provision for the flesshe to fulfyll ye lustes of it.
Bali tumvae Bwana Yesu Kristo, na tusiweke nafasi kwa ajili ya mwili, kwa tamaa zake.

< Romans 13 >