< Matthew 9 >

1 Then he entred in to a shippe and passed over and came in to his awne cite.
Yesu alipanda mashua, akavuka ziwa na kufika katika mji wake.
2 And lo they brought to him a ma sicke of ye palsie lyinge in his bed. And when Iesus sawe ye faith of the he sayd to the sicke of ye palsie: sonne be of good chere thy sinnes be forgeve the.
Hapo watu walimletea mtu mmoja aliyepooza mwili, amelazwa juu ya kitanda. Yesu alipoona imani yao, akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Jipe moyo mwanangu! Umesamehewa dhambi zako.”
3 And beholde certeyne of ye scribes sayd in the selves this ma blasphemeth.
Baadhi ya walimu wa Sheria wakaanza kufikiri, “Mtu huyu anamkufuru Mungu!”
4 And whe Iesus sawe their thoughtes he sayd: wherfore thinke ye evill in youre hertes?
Yesu aliyajua mawazo yao, akasema, “Kwa nini mnawaza mabaya mioyoni mwenu?
5 Whether ys esyer to saye thy synnes be forgeven ye or to saye: arise and walke?
Ni lipi lililo rahisi zaidi: kusema, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Simama, utembee?
6 That ye maye knowe that ye sonne of ma hath power to forgeve sinnes in erth then sayd he vnto ye sicke of ye palsye: arise take vp thy beed and go home to thine housse.
Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kuwasamehe watu dhambi duniani.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Inuka, chukua kitanda chako, uende nyumbani kwako.”
7 And he arose and departed to his awne housse.
Huyo mtu aliyekuwa amepooza akainuka, akaenda nyumbani kwake.
8 And when ye people sawe it they marveyled and glorified god which had geve suche power to me.
Watu wote katika ule umati walipoona hayo, walishangaa na kuogopa; wakamtukuza Mungu aliyewapa binadamu uwezo wa namna hiyo.
9 And as Iesus passed forth fro thence he sawe a ma syt a receyuinge of custome named Mathew and sayd to him: folowe me.
Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda zake, alimwona mtu mmoja aitwaye Mathayo, ameketi katika ofisi ya ushuru. Basi, Yesu akamwambia, “Nifuate.” Naye Mathayo akainuka, akamfuata.
10 And he arose and folowed him. And it came to passe as he sat at meate in the housse: beholde many publicans and synners came and sate downe also with Iesus and hys disciples.
Yesu alipokuwa nyumbani ameketi kula chakula, watoza ushuru wengi na wahalifu walikuja wakaketi pamoja naye na wanafunzi wake.
11 When the Pharises sawe that they sayd to hys disciples: why eateth youre master wt publicans and synners?
Mafarisayo walipoona hayo, wakawaambia wanafunzi wake, “Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?”
12 When Iesus herde that he sayde vnto them: The whole neade not the phisicion but they that are sicke.
Yesu aliwasikia, akasema, “Watu wenye afya hawahitaji daktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. Sikuja kuwaita watu wema, ila wenye dhambi.
13 Goo and learne what that meaneth: I have pleasure in mercy and not in offerynge. For I am not come to call the rightewes but the synners to repentaunce.
Basi, kajifunzeni maana ya maneno haya: Nataka huruma, wala si dhabihu. Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi.”
14 Then came ye disciples of Ihon to hym sayinge: why do we and the Pharises fast ofte: but thy disciples fast not?
Kisha wanafunzi wa Yohane mbatizaji walimwendea Yesu, wakamwuliza, “Sisi na Mafarisayo hufunga mara nyingi; mbona wanafunzi wako hawafungi?”
15 And Iesus sayde vnto them: Can ye weddynge chyldren morne as longe as ye bridegrome is wt them? The tyme will come whe the bridegrome shalbe take fro them and then shall they faste.
Yesu akawajibu, “Je, walioalikwa arusini wanaweza kuomboleza wakati bwana arusi yupo pamoja nao? La hasha! Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kati yao; wakati huo ndipo watakapofunga.
16 Noo man peceth and olde garment with a pece of newe cloothe. For then taketh he awaye ye pece agayne from the garmet and the rent ys made greater.
“Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu. Maana kiraka hicho kitararua hilo vazi kuukuu, na pale palipokuwa pameraruka pataongezeka.
17 Nether do men put newe wyne into olde vessels for then the vessels breake and the wyne runneth oute and the vessels perysshe. But they powre newe wyne into newe vessels and so are both saved togeder.
Wala hakuna mtu awekaye divai mpya katika viriba vikuukuu. Akifanya hivyo, viriba hupasuka na divai ikamwagika, navyo viriba vikaharibika. Ila divai mpya hutiwa katika viriba vipya, na vyote viwili, viriba na divai, vikahifadhiwa salama.”
18 Whyls he thus spake vnto the beholde ther came a certayne ruler and worshipped him sayinge: my doghter is euen now deceased but come and lay thy honde on her and she shall live.
Yesu alipokuwa akisema hayo, ofisa mmoja Myahudi alifika, akamwinamia na kusema, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini, tafadhali njoo umwekee mkono wako naye ataishi.”
19 And Iesus arose and folowed hym with hys disciples.
Yesu akaondoka pamoja na wanafunzi wake, akamfuata.
20 And beholde a woman which was diseased wt an yssue of bloude. xii. yeres came behynde hym and toched ye hem of hys vesture.
Mama mmoja, mgonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, alimfuata Yesu nyuma, akagusa pindo la vazi lake.
21 For she sayd in her silfe: yf I maye toche but even his vesture only I shalbe safe.
Alifanya hivyo kwani alifikiri moyoni: “Nikigusa tu vazi lake, nitapona.”
22 Then Iesus tourned him about and behelde her sayinge: Doughter be of good conforte thy faith hath made the safe. And she was made whole even that same houre.
Basi, Yesu akageuka akamwona, akamwambia, “Binti, jipe moyo! Imani yako imekuponya.” Mama huyo akapona saa ileile.
23 And when Iesus came into ye rulers housse and sawe the minstrels and the people raginge
Kisha Yesu akaingia nyumbani kwa yule ofisa. Na alipowaona wapiga filimbi na umati wa watu wanaofanya matanga,
24 he sayde vnto them: Get you hence for ye mayde is not deed but slepeth. And they laughed hym to scorne.
akasema, “Ondokeni hapa! Msichana huyu hakufa, amelala tu.” Nao wakamcheka.
25 Assone as ye people were put forthe he went in and toke her by ye hond and the mayde arose.
Basi, umati wa watu ulipoondolewa, Yesu aliingia ndani, akamshika huyo msichana mkono, naye akasimama.
26 And this was noysed through out all that lande.
Habari hiyo ikavuma sana katika nchi ile yote.
27 And as Iesus departed thence two blynde men folowed hym crying and saying: O thou sonne of David have mercy on vs.
Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda, vipofu wawili walimfuata wakipiga kelele, “Mwana wa Daudi, utuhurumie!”
28 And when he was come to housse the blynd came to hym And Iesus sayde vnto them: Beleve ye that I am able to do thys? And they sayde vnto hym: ye Lorde.
Yesu alipoingia nyumbani, vipofu hao wawili wakamwendea, naye akawauliza, “Je, mnaamini kwamba naweza kuwafanyia jambo hilo?” Nao wakamjibu, “Naam, Mheshimiwa.”
29 Then touched he their eyes saying: acordynge to youre faythe be it vnto you.
Hapo Yesu akayagusa macho yao, akasema, “Na iwe kwenu kama mnavyoamini.”
30 And their eyes were opened. And Iesus charged the saying: Se yt no man knowe of it.
Macho yao yakafunguliwa. Naye Yesu akawaonya kwa ukali: “Msimwambie mtu yeyote jambo hili.”
31 But they assone as they were departed spreed abroade his name through oute all the londe.
Lakini wao wakaondoka, wakaeneza habari za Yesu katika nchi ile yote.
32 As they went out beholde they brought to hym a dome ma possessed af a devyll.
Watu walipokuwa wanakwenda zao, wengine walimletea Yesu mtu mmoja aliyekuwa bubu kwa sababu alikuwa amepagawa na pepo.
33 And as sone as the devyll was cast oute the domme spake: And the people merveled sayinge: it was never so sene in Israel.
Mara tu huyo pepo alipotolewa, mtu huyo aliyekuwa bubu akaanza kuongea tena. Watu wakashangaa na kusema, “Jambo kama hili halijapata kuonekana katika Israeli!”
34 But the Pharises sayde: he casteth oute devyls by the power of the chefe devyll.
Lakini Mafarisayo wakawa wanasema, “Anawatoa pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo wabaya.”
35 And Iesus went about all cities and tounes teachynge in their synagoges and preachyng the glad tidinges of ye kyngdome and healinge all maner sicknes and desease amoge ye people.
Yesu alitembelea miji yote na vijiji, akafundisha katika masunagogi yao akihubiri Habari Njema ya Ufalme wa Mungu, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila namna.
36 But when he sawe the people he had copassion on the because they were pyned awaye and scattered abroade eve as shepe havige no shepherd.
Basi, alipowaona watu, makundi kwa makundi, aliwaonea huruma kwa sababu walikuwa hoi na wenye wasiwasi kama kondoo wasio na mchungaji.
37 Then sayde he to hys disciples: the hervest is greate but the laborers are feawe.
Hapo akawaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi, lakini wavunaji ni wachache.
38 Wherfore praye the Lorde of the harvest to sende forthe laborers into hys harvest.
Kwa hivyo mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake.”

< Matthew 9 >