< Matthew 4 >

1 Then was Iesus ledd awaye of ye spirite into wildernes to be tempted of ye devyll.
Kisha Roho alimwongoza Yesu mpaka jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi.
2 And when he had fasted fourtye dayes and fourtye nightes he was afterward an hungred.
Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa.
3 Then came to hym the tempter and sayde: yf thou be the sonne of God commaunde that these stones be made breed.
Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”
4 He answered and sayde: yt is wrytten man shall not lyve by brede onlye but by every worde yt proceadeth out of the mouth of God.
Yesu akamjibu, “Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: Binadamu hataishi kwa mikate tu, ila kwa kila neno asemalo Mungu.”
5 Then the devyll tooke hym vp into ye holy cite and set hym on a pynacle of the teple
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu,
6 and sayd vnto hym: yf thou be the sonne of God cast thy sylfe doune. For it is wrytte he shall geve his angels charge over the and with their handes they shall holde yt vp that thou dashe not thy fote agaynst a stone.
akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa: Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako; watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye jiwe.”
7 And Iesus sayde to hym it ys wrytten also: Thou shalt not tempte thy Lorde God.
Yesu akamwambia, “Imeandikwa pia: Usimjaribu Bwana, Mungu wako.”
8 The devyll toke hym vp agayne and ledde hym in to an excedynge hye mountayne and shewed hym all the kyngdomes of ye worlde and all ye glorie of them
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,
9 and sayde to hym: all these will I geue ye if thou wilt faull doune and worship me.
akamwambia, “Hivi vyote nitakupa kama tu ukipiga magoti na kuniabudu.”
10 Then sayde Iesus vnto hym. Avoyd Satan. For it is writte thou shalt worshyp ye Lorde thy God and hym only shalt thou serve.
Hapo, Yesu akamwambia, “Nenda zako Shetani! Imeandikwa: Utamwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake.”
11 Then the dyvell left hym and beholde the angels came and ministred vnto hym.
Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia.
12 When Iesus had hearde yt Ihon was taken he departed into Galile
Yesu aliposikia kwamba Yohane ametiwa gerezani alikwenda Galilaya.
13 and left Nazareth and went and dwelte in Capernaum which is a cite apon the see in ye coostes of zabulon and Neptalim
Aliondoka Nazareti, akaenda Kafarnaumu, mji ulio kando ya bahari ya Genesareti, mpakani mwa wilaya za Zabuloni na Naftali, akakaa huko.
14 to fulfill that whiche was spoken by Esay the Prophet sayinge:
Ndivyo lilivyotimia lile neno lililosemwa kwa njia ya nabii Isaya:
15 The londe of zabulon and Neptalim the waye of the see beyonde Iordan Galile of the Gentyls
“Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kuelekea baharini ng'ambo ya mto Yordani, Galilaya nchi ya watu wa Mataifa!
16 ye people which sat in darknes sawe greate lyght and to them which sate in the region and shadowe of deeth lyght is begone to shyne.
Watu waliokaa gizani wameona mwanga mkubwa. Nao walioishi katika nchi ya giza na kivuli cha kifo, mwanga umewaangazia!”
17 From yt tyme Iesus begane to preache and to saye: repet for ye kigdome of heve is at hode.
Tangu wakati huo Yesu alianza kuhubiri akisema, “Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia!”
18 As Iesus walked by the see of Galile he sawe two brethren: Simon which was called Peter and Andrew his brother castynge a neet into the see for they were fisshers
Yesu alipokuwa anatembea kando ya ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili wavuvi; Simoni (aitwae Petro) na Andrea, ndugu yake; walikuwa wakivua samaki kwa nyavu ziwani.
19 and he sayde vnto them folowe me and I will make you fisshers of men.
Basi, akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanya ninyi wavuvi wa watu.”
20 And they strayght waye lefte their nettes and folowed hym.
Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
21 And he went forthe from thence and sawe other twoo brethren Iames the sonne of zebede and Ihon his brother in the shippe with zebede their father mendynge their nettes and called them.
Alipokwenda mbele kidogo, aliwaona ndugu wengine wawili: Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo. Hao walikuwa ndani ya mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakitengeneza nyavu zao. Basi Yesu akawaita,
22 And they with out taryinge lefte the shyp and their father and folowed hym.
nao mara wakaiacha mashua pamoja na baba yao, wakamfuata.
23 And Iesus went aboute all Galile teachyng in their synagoges and preachynge ye gospell of the kyngdome and healed all maner of sicknes and all maner dyseases amoge ye people.
Yesu alikuwa anakwenda kila mahali wilayani Galilaya, akifundisha katika masunagogi na kuhubiri Habari Njema juu ya ufalme wa Mungu. Aliponya kila namna ya maradhi na magonjwa waliyokuwa nayo watu.
24 And his fame spreed abroode through oute all Siria. And they brought vnto hym all sicke people that were taken with divers diseases and gripinges and them yt were possessed with devils and those which were lunatyke and those that had the palsie: and he healed the.
Habari zake zikaenea katika mkoa wote wa Siria. Wagonjwa wote wenye maradhi ya kila namna na wale waliosumbuliwa na kila namna ya taabu: waliopagawa na pepo, wenye kifafa na watu waliokuwa wamelemaa, walipelekwa kwake; naye akawaponya wote.
25 And ther folowed hym a greate nombre of people from Galile and from the ten cyties and from Ierusalem and from Iury and from ye regions that lye beyonde Iordan.
Makundi mengi ya watu kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Yudea na ng'ambo ya mto Yordani, walimfuata.

< Matthew 4 >