< Numbers 26 >

1 And it came to pass after the plague, that the LORD spake unto Moses and unto Eleazar the son of Aaron the priest, saying,
Baada ya hiyo tauni, Bwana akamwambia Mose na Eleazari mwana wa kuhani Aroni,
2 Take the sum of all the congregation of the children of Israel, from twenty years old and upward, by their fathers’ houses, all that are able to go forth to war in Israel.
“Hesabu jumuiya yote ya Kiisraeli kwa jamaa zao, wale wote wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, ambao wanaweza kutumika katika jeshi la Israeli.”
3 And Moses and Eleazar the priest spake with them in the plains of Moab by the Jordan at Jericho, saying,
Hivyo Mose na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare ya Moabu, ngʼambo ya Yordani kutokea Yeriko, wakasema,
4 [Take the sum of the people], from twenty years old and upward; as the LORD commanded Moses and the children of Israel, which came forth out of the land of Egypt.
“Hesabuni wanaume wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kama Bwana alivyomwagiza Mose.” Hawa ndio Waisraeli waliotoka Misri:
5 Reuben, the firstborn of Israel: the sons of Reuben; [of] Hanoch, the family of the Hanochites: of Pallu, the family of the Palluites:
Wazao wa Reubeni, mwana mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa: kutoka kwa Hanoki, ukoo wa Wahanoki; kutoka kwa Palu, ukoo wa Wapalu;
6 of Hezron, the family of the Hezronites: of Carmi, the family of the Carmites.
kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni; kutoka kwa Karmi, ukoo wa Wakarmi.
7 These are the families of the Reubenites: and they that were numbered of them were forty and three thousand and seven hundred and thirty.
Hizi zilikuwa ndizo koo za Reubeni; wale waliohesabiwa walikuwa 43,730.
8 And the sons of Pallu; Eliab.
Mwana wa Palu alikuwa Eliabu,
9 And the sons of Eliab; Nemuel, and Dathan, and Abiram. These are that Dathan and Abiram, which were called of the congregation, who strove against Moses and against Aaron in the company of Korah, when they strove against the LORD:
nao wana wa Eliabu walikuwa Nemueli, Dathani na Abiramu. Hawa wawili Dathani na Abiramu ndio walikuwa maafisa wa jumuiya ambao walimwasi Mose na Aroni, na walikuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora wakati walimwasi Bwana.
10 and the earth opened her mouth, and swallowed them up together with Korah, when that company died; what time the fire devoured two hundred and fifty men, and they became a sign.
Ardhi ilifunua kinywa chake na kuwameza pamoja na Kora, ambaye wafuasi wake walikufa wakati moto ulipowateketeza wanaume 250. Nao walikuwa kama alama ya onyo.
11 Notwithstanding the sons of Korah died not.
Pamoja na hayo, hao ukoo wa Kora hawakufa.
12 The sons of Simeon after their families: of Nemuel, the family of the Nemuelites: of Jamin, the family of the Jaminites: of Jachin, the family of the Jachinites:
Wazao wa Simeoni kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Nemueli, ukoo wa Wanemueli; kutoka kwa Yamini, ukoo wa Wayamini; kutoka wa Yakini, ukoo wa Wayakini;
13 of Zerah, the family of the Zerahites: of Shaul, the family of the Shaulites.
kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera; kutoka kwa Shauli, ukoo wa Washauli.
14 These are the families of the Simeonites, twenty and two thousand and two hundred.
Hizi ndizo koo za Simeoni; walikuwa 22,200.
15 The sons of Gad after their families: of Zephon, the family of the Zephonites: of Haggi, the family of the Haggites: of Shuni, the family of the Shunites:
Wazao wa Gadi kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Sifoni, ukoo wa Wasifoni; kutoka kwa Hagi, ukoo wa Wahagi; kutoka kwa Shuni, ukoo wa Washuni;
16 of Ozni, the family of the Oznites: of Eri, the family of the Erites:
kutoka kwa Ozni, ukoo wa Waozni; kutoka kwa Eri, ukoo wa Waeri;
17 of Arod, the family of the Arodites: of Areli, the family of the Arelites.
kutoka kwa Arodi, ukoo wa Waarodi; kutoka kwa Areli, ukoo wa Waareli.
18 These are the families of the sons of Gad according to those that were numbered of them, forty thousand and five hundred.
Hizi ndizo zilizokuwa koo za Gadi; wale waliohesabiwa walikuwa 40,500.
19 The sons of Judah, Er and Onan: and Er and Onan died in the land of Canaan.
Eri na Onani walikuwa wana wa Yuda, lakini walifia huko Kanaani.
20 And the sons of Judah after their families were; of Shelah, the family of the Shelanites: of Perez, the family of the Perezites: of Zerah, the family of the Zerahites.
Wazao wa Yuda kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Shela, ukoo wa Washela; kutoka kwa Peresi, ukoo wa Waperesi; kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera.
21 And the sons of Perez were; of Hezron, the family of the Hezronites: of Hamul, the family of the Hamulites.
Wazao wa Peresi walikuwa: kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni; kutoka kwa Hamuli, ukoo wa Wahamuli.
22 These are the families of Judah according to those that were numbered of them, threescore and sixteen thousand and five hundred.
Hizi ndizo zilizokuwa koo za Yuda; wale waliohesabiwa walikuwa 76,500.
23 The sons of Issachar after their families: [of] Tola, the family of the Tolaites: of Puvah, the family of the Punites:
Wazao wa Isakari kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Tola, ukoo wa Watola; kutoka kwa Puva, ukoo wa Wapuva;
24 of Jashub, the family of the Jashubites: of Shimron, the family of the Shimronites.
kutoka kwa Yashubu, ukoo wa Wayashubu; kutoka kwa Shimroni, ukoo wa Washimroni.
25 These are the families of Issachar according to those that were numbered of them, threescore and four thousand and three hundred.
Hizi ndizo zilizokuwa koo za Isakari; wale waliohesabiwa walikuwa 64,300.
26 The sons of Zebulun after their families: of Sered, the family of the Seredites: of Elon, the family of the Elonites: of Jahleel, the family of the Jahleelites.
Wazao wa Zabuloni kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Seredi, ukoo wa Waseredi; kutoka kwa Eloni, ukoo wa Waeloni; kutoka kwa Yaleeli, ukoo wa Wayaleeli.
27 These are the families of the Zebulunites according to those that were numbered of them, threescore thousand and five hundred.
Hizi ndizo zilizokuwa koo za Zabuloni, wale waliohesabiwa walikuwa 60,500.
28 The sons of Joseph after their families: Manasseh and Ephraim.
Wazao wa Yosefu kwa koo zao kutoka kwa Manase na kwa Efraimu walikuwa:
29 The sons of Manasseh: of Machir, the family of the Machirites: and Machir begat Gilead: of Gilead, the family of the Gileadites.
Wazao wa Manase: kutoka kwa Makiri, ukoo wa Wamakiri (Makiri alikuwa baba wa Gileadi); kutoka kwa Gileadi, ukoo wa Wagileadi.
30 These are the sons of Gilead: [of] Iezer, the family of the Iezerites: of Helek, the family of the Helekites:
Hawa ndio waliokuwa wazao wa Gileadi: kutoka kwa Iezeri, ukoo wa Waiezeri; kutoka kwa Heleki, ukoo wa Waheleki;
31 and [of] Asriel, the family of the Asrielites: and [of] Shechem, the family of the Shechemites:
kutoka kwa Asirieli, ukoo wa Waasirieli; kutoka kwa Shekemu, ukoo wa Washekemu;
32 and [of] Shemida, the family of the Shemidaites: and [of] Hepher, the family of the Hepherites.
kutoka kwa Shemida, ukoo wa Washemida; kutoka kwa Heferi, ukoo wa Waheferi.
33 And Zelophehad the son of Hepher had no sons, but daughters: and the names of the daughters of Zelophehad were Mahlah, and Noah, Hoglah, Milcah, and Tirzah.
(Selofehadi mwana wa Heferi hakuzaa wana, bali alikuwa na watoto wa kike tu, ambao majina yao yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa.)
34 These are the families of Manasseh: and they that were numbered of them were fifty and two thousand and seven hundred.
Hizi ndizo zilizokuwa koo za Manase; wale waliohesabiwa walikuwa 52,700.
35 These are the sons of Ephraim after their families: of Shuthelah, the family of the Shuthelahites: of Becher, the family of the Becherites: of Tahan, the family of the Tahanites.
Hawa walikuwa wazao wa Efraimu kwa koo zao: kutoka kwa Shuthela, ukoo wa Washuthela; kutoka kwa Bekeri, ukoo wa Wabekeri; kutoka kwa Tahani, ukoo wa Watahani;
36 And these are the sons of Shuthelah: of Eran, the family of the Eranites.
Hawa ndio walikuwa wazao wa Shuthela: kutoka kwa Erani, ukoo wa Waerani.
37 These are the families of the sons of Ephraim according to those that were numbered of them, thirty and two thousand and five hundred. These are the sons of Joseph after their families.
Hizi ndizo zilizokuwa koo za Efraimu; wale waliohesabiwa walikuwa 32,500. Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yosefu kwa koo zao.
38 The sons of Benjamin after their families: of Bela, the family of the Belaites: of Ashbel, the family of the Ashbelites: of Ahiram, the family of the Ahiramites:
Wazao wa Benyamini kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Bela, ukoo wa Wabela; kutoka kwa Ashbeli, ukoo wa Waashbeli; kutoka kwa Ahiramu, ukoo wa Waahiramu;
39 of Shephupham, the family of the Shuphamites: of Hupham, the family of the Huphamites.
kutoka kwa Shufamu, ukoo wa Washufamu; kutoka kwa Hufamu, ukoo wa Wahufamu.
40 And the sons of Bela were Ard and Naaman: [of Ard], the family of the Ardites: of Naaman, the family of the Naamites.
Wazao wa Bela kutoka kwa Ardi na Naamani walikuwa: kutoka kwa Ardi, ukoo wa Waardi; kutoka kwa Naamani, ukoo wa Wanaamani.
41 These are the sons of Benjamin after their families: and they that were numbered of them were forty and five thousand and six hundred.
Hizi ndizo zilizokuwa koo za Benyamini; wale waliohesabiwa walikuwa 45,600.
42 These are the sons of Dan after their families: of Shuham, the family of the Shuhamites. These are the families of Dan after their families.
Hawa ndio waliokuwa wazao wa Dani kwa koo zao: kutoka kwa Shuhamu, ukoo wa Washuhamu. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Dani:
43 All the families of the Shuhamites, according to those that were numbered of them, were threescore and four thousand and four hundred.
Wote walikuwa koo za Washuhamu; wale waliohesabiwa walikuwa 64,400.
44 The sons of Asher after their families: of Imnah, the family of the Imnites: of Ishvi, the family of the Ishvites: of Beriah, the family of the Beriites.
Wazao wa Asheri kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Imna, ukoo wa Waimna; kutoka kwa Ishvi, ukoo wa Waishvi; kutoka kwa Beria, ukoo wa Waberia;
45 Of the sons of Beriah: of Heber, the family of the Heberites: of Malchiel, the family of the Malchielites.
kutoka kwa wazao wa Beria: kutoka kwa Heberi, ukoo wa Waheberi; kutoka kwa Malkieli, ukoo wa Wamalkieli.
46 And the name of the daughter of Asher was Serah.
(Asheri alikuwa na binti aliyeitwa Sera.)
47 These are the families of the sons of Asher according to those that were numbered of them, fifty and three thousand and four hundred.
Hizi ndizo zilizokuwa koo za Asheri; wale waliohesabiwa walikuwa 53,400.
48 The sons of Naphtali after their families: of Jahzeel, the family of the Jahzeelites: of Guni, the family of the Gunites:
Wazao wa Naftali kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Yaseeli, ukoo wa Wayaseeli; kutoka kwa Guni, ukoo wa Waguni;
49 of Jezer, the family of the Jezerites: of Shillem, the family of the Shillemites.
kutoka kwa Yeseri, ukoo wa Wayeseri; kutoka kwa Shilemu, ukoo wa Washilemu.
50 These are the families of Naphtali according to their families: and they that were numbered of them were forty and five thousand and four hundred.
Hizi ndizo zilizokuwa koo za Naftali; wale waliohesabiwa walikuwa 45,400.
51 These are they that were numbered of the children of Israel, six hundred thousand and a thousand seven hundred and thirty.
Jumla ya hesabu ya wanaume wa Israeli ilikuwa 601,730.
52 And the LORD spake unto Moses, saying,
Bwana akamwambia Mose,
53 Unto these the land shall be divided for an inheritance according to the number of names.
“Watagawiwa nchi kama urithi kwa kulingana na hesabu ya majina.
54 To the more thou shalt give the more inheritance, and to the fewer thou shalt give the less inheritance: to every one according to those that were numbered of him shall his inheritance be given.
Kundi kubwa zaidi lipe urithi mkubwa zaidi, na kundi dogo zaidi lipewe urithi mdogo zaidi; kila kundi litapokea urithi wake kulingana na hesabu ya wale walioorodheshwa.
55 Notwithstanding the land shall be divided by lot: according to the names of the tribes of their fathers they shall inherit.
Hakikisha kuwa nchi inagawanywa kwa kura. Kile kitakachorithiwa na kila kikundi kitakuwa kwa kulingana na majina ya kabila la babu yao.
56 According to the lot shall their inheritance be divided between the more and the fewer.
Kila urithi utagawanywa kwa kura miongoni mwa makundi makubwa na madogo.”
57 And these are they that were numbered of the Levites after their families: of Gershon, the family of the Gershonites: of Kohath, the family of the Kohathites: of Merari, the family of the Merarites.
Hawa walikuwa Walawi ambao walihesabiwa kwa koo zao: kutoka kwa Gershoni, ukoo wa Wagershoni; kutoka kwa Kohathi, ukoo wa Wakohathi; kutoka kwa Merari, ukoo wa Wamerari.
58 These are the families of Levi: the family of the Libnites, the family of the Hebronites, the family of the Mahlites, the family of the Mushites, the family of the Korahites. And Kohath begat Amram.
Hizi pia zilikuwa koo za Walawi: ukoo wa Walibni; ukoo wa Wahebroni; ukoo wa Wamahli; ukoo wa Wamushi; ukoo wa wana wa Kora. (Kohathi alikuwa baba aliyemzaa Amramu;
59 And the name of Amram’s wife was Jochebed, the daughter of Levi, who was born to Levi in Egypt: and she bare unto Amram Aaron and Moses, and Miriam their sister.
jina la mke wa Amramu ni Yokebedi, naye pia alikuwa mzao wa Lawi, ambaye alizaliwa kwa Walawi nchini Misri. Alimzalia Amramu: Aroni, Mose na dada yao Miriamu.
60 And unto Aaron were born Nadab and Abihu, Eleazar and Ithamar.
Aroni alikuwa baba yake Nadabu na Abihu, Eleazari na Ithamari.
61 And Nadab and Abihu died, when they offered strange fire before the LORD.
Lakini Nadabu na Abihu walikufa wakati walitoa sadaka mbele za Bwana kwa moto usioruhusiwa.)
62 And they that were numbered of them were twenty and three thousand, every male from a month old and upward: for they were not numbered among the children of Israel, because there was no inheritance given them among the children of Israel.
Wanaume wote wa Walawi wa umri wa mwezi mmoja na zaidi walikuwa 23,000. Wao hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine kwa sababu hawakupokea urithi miongoni mwao.
63 These are they that were numbered by Moses and Eleazar the priest; who numbered the children of Israel in the plains of Moab by the Jordan at Jericho.
Hawa ndio walioorodheshwa na Mose na kuhani Eleazari wakati waliwahesabu Waisraeli kwenye nchi tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko.
64 But among these there was not a man of them that were numbered by Moses and Aaron the priest; who numbered the children of Israel in the wilderness of Sinai.
Hakuna hata mmoja wao aliyekuwa miongoni mwa wale waliohesabiwa na Mose na kuhani Aroni wakati waliwahesabu Waisraeli katika Jangwa la Sinai.
65 For the LORD had said of them, They shall surely die in the wilderness. And there was not left a man of them, save Caleb the son of Jephunneh, and Joshua the son of Nun.
Kwa maana Bwana alikuwa amewaambia hao Waisraeli hakika wangekufa huko jangwani, wala hakuna mmoja wao aliyeachwa, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Yoshua mwana wa Nuni.

< Numbers 26 >