Preface
Read
+
Publisher
Nainoia, Inc.
PO Box 462, Bellefonte, PA 16823
(814) 470-8028
Nainoia Inc, Publisher
LinkedIn/NAINOIA-INC
Third Party Publisher Resources
Request Custom Formatted Verses
Please contact us below
Submit your proposed corrections
I understand that the Aionian Bible republishes public domain and Creative Commons Bible texts and that volunteers may be needed to present the original text accurately. I also understand that apocryphal text is removed and most variant verse numbering is mapped to the English standard. I have entered my corrections under the verse(s) below. Proposed corrections to the New Swahili Bible, Psalms Chapter 74 https://www.AionianBible.org/Bibles/Swahili---New-Swahili-Bible/Psalms/74 1) Mungu, kwa nini umetukataa milele? Kwa nini hasira yako inawaka dhidi ya kondoo wa malisho yako? 2) Wafikilie watu wako, ambao uliwanunua siku nyingi zilizopita, kabila ambalo wewe umelikomboa liwe urithi wako, na Milima Sayuni, mahali uishipo. 3) Uje utazame uharibifu kamili, uharibifu ambao umefanywa na adui mahali patakatifu. 4) Washindani wako walivamia katikati ya mahali pako maalumu; walipandisha bendera zao za vita. 5) Walipakatakata kwa shoka kama katika msitu mnene. 6) Walipaharibu na kuvunja sanaa zilizonakshiwa zote; walizivunja kwa shoka na nyundo. 7) Walipachoma patakatifu pako; walipanajisi mahari unapoishi, wakigongagonga kwenye ardhi. 8) Walisema mioyoni mwao, “Tutawaharibu wote.” Walichoma sehemu zako zote za kukutania katika nchi. 9) Sisi hatuoni tena ishara; hakuna tena nabii, na hakuna yeyote miongoni mwetu ajuaye haya yatadumu kwa muda gani. 10) Mpaka lini, Mungu, adui atakurushia wewe matusi? Je, atalitukana jina lako milele? 11) Kwa nini umerudisha nyuma mkono wako, mkono wako wa kuume? Utoe mkono wako kwenye mavazi yako na uwaangamize. 12) Lakini Mungu amekuwa mfalme wangu tangu enzi, akileta wokovu tuniani. 13) Wewe uliigawa bahari; ulishambulia vichwa vya majitu ya kutisha baharini majini. 14) Wewe ulishambulia vichwa vya lewiathani; na kumfanya awe chakula cha viumbe hai jangwani. 15) Ulizifungulia chemchem na vijito; uliikausha mito itiririkayo. 16) Mchana ni wako, na usiku ni wako pia; uliweka jua na mwezi mahari pake. 17) Umeiweka mipaka ya nchi; umeumba majira ya joto na majira ya baridi. 18) Kumbula vile adui alivyo vurumisha matusi kwako, Yahwe, na kwamba watu wapumbavu wamelitukana jina lako. 19) Usimtoe njiwa afe kwa mnyama wa porini. Usiusahau milele uhai wa watu wako walio onewa. 20) Kumbuka agano lako, maana majimbo ya giza ya nchi yamejaa maeneo ya vurugu. 21) Usiwaache walioonewa warudishwe kwa aibu; uwaache maskini na walioonewa walisifu jina lako. 22) Inuka Mungu, itetee heshima yako; kumbuka wajinga wanavyokutukana machana kutwa. 23) Usisahau sauti ya adui zako au kelele za wale wanaoendelea kukuchafua. Additional comments?
Refresh Captcha
The world's first Holy Bible un-translation!