< 1 Yohana 1 >

1 Habari hii ya yahusu Neno la uzima lililokuwako tangu mwanzo. Sisi tumepata kulisikia na kuliona kwa macho yetu wenyewe; tulilitazama na kulishika kwa mikono yetu wenyewe.
What was from the beginning, what we have heard, what we have seen with our eyes, what we looked upon, and our hands touched, concerning the Word of life
2 Uzima huo ulipotokea sisi tuliuona na sasa tunasema habari zake na kuwaambieni juu ya uzima huo wa milele uliokuwa kwa Baba na uliodhihirishwa kwetu. (aiōnios g166)
(and the life was made known, and we have seen, and testify, and declare to you the eternal life that was with the Father, and was made known to us), (aiōnios g166)
3 Tulichokiona na kukisikia ndicho tunachowatangazieni ninyi pia ili nanyi mpate kushirikiana nasi katika umoja tulio nao na Baba na Mwanae Yesu Kristo.
what we have seen and heard we also declare to you, so that ye also may have fellowship with us. Even also our fellowship with the Father, and with his Son Jesus Christ.
4 Tunawaandikia ninyi mambo haya kusudi furaha yetu ikamilike.
And we write these things to you, so that our joy may be made full.
5 Basi, habari tuliyoisikia kwake Yesu na tunayowahubirieni ndiyo hii: Mungu ni mwanga na hamna giza lolote ndani yake.
And this is the message that we have heard from him and declare to you, that God is light, and in him is no darkness at all.
6 Tukisema kwamba tuna umoja naye, na papo hapo twaishi gizani, tutakuwa tumesema uongo kwa maneno na matendo.
If we say that we have fellowship with him and walk in the darkness, we lie, and do not the truth.
7 Lakini tukiishi katika mwanga, kama naye alivyo katika mwanga, basi tutakuwa na umoja sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwanae, inatutakasa dhambi zote.
But if we walk in the light, as he is in the light, we have fellowship with each other, and the blood of Jesus Christ his Son cleanses us from every sin.
8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe na ukweli haumo ndani yetu.
If we say that we have no sin, we lead ourselves astray, and the truth is not in us.
9 Lakini tukiziungama dhambi zetu, basi Mungu ni mwaminifu na mwadilifu, naye atatusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote.
If we confess our sins, he is faithful and righteous so that he will forgive us our sins, and cleanse us from every unrighteousness.
10 Tukisema kwamba hatujatenda dhambi, tutakuwa tumemfanya Mungu mwongo, na neno lake halimo ndani yetu.
If we say that we have not sinned, we make him a liar, and his word is not in us.

< 1 Yohana 1 >