< Zaburi 63 >

1 Mungu, wewe ni Mungu wangu! Ninakutafuta wewe kwa bidii, moyo wangu unakiu yako, mwili wangu unakutamani sana wewe, katika ukame na nchi iliyochoka mahali ambapo hakuna maji. 2 Hivyo nimekutafuta wewe katika watu watakatifu kuona nguvu zako na utukufu wako. 3 Kwa sababu uaminifu wa agano lako ni bora kuliko uhai, midomo yangu itakusifu wewe. 4 Hivyo nitakutukuza wewe niwapo hai; kwa jina lako nitainua mikono yangu juu. 5 Itakuwa kana kwamba nilikula mlo wa mafuta na wenye kunona, kwa midomo ya furaha kinywa changu kitakusifu wewe, 6 nikufikiripo kitandani mwangu na kukutafakari wewe wakati wa saa za usiku. 7 Kwa maana umekuwa msaada wangu, na katika uvuli wa mbawa zako ninafurahia. 8 Ninashikamana nawe; mkono wako wa kuume unanisaidia. 9 Lakini wale watafutao kuuharibu uhai wangu wataenda chini kwenye sehemu ya chini kabisa ya nchi; 10 watakabidhiwa kwa wale ambao mikono yao hutumia upanga, nao watakuwa chakula cha mbweha. 11 Bali mfalme atashangilia katika Mungu; yeyote anaye apa kupitia yeye atajivunia yeye, lakini vinywa ya wale wasemao uongo watanyamazishwa.

< Zaburi 63 >