< Zaburi 127 >

1 Yahwe asipoijenga nyumba, waijengao wafanya kazi bure. Yahwe asipoulinda mji, aulindaye afanya kazi bure. 2 Ni kazi bure kwa wewe unayeamka mapema, na kulala kwa kuchelewa, au kula mkate kwa kuufanyia kazi ngumu, maana Yahwe huwapa chakula awapendao hata wawapo usingizini. 3 Tazama, wana ni urithi kutoka kwa Yahwe, uzao wa tumbo ni thawabu kutoka kwake. 4 Kama mishale mkononi mwa shujaa, ndivyo walivyo wana wa ujanani. 5 Ni namna gani alivyo barikiwa mtu ambaye amelijaza podo lake hivyo. Hata aibishwa pindi atakapo kabiliana na adui zake katika lango.

< Zaburi 127 >