< Arumi 8 >

1 Tumbwe lelo tupu azabu nkati ta bababile nkati ya Kirisitu Yesu.
Kwa hiyo basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
2 Kwasababu kanuni ya Roho ni wankoto waubile katika Kirisitu Yesu inipangite nenga ba uru kutalu na kanuni ya sambi na kiwo.
Kwa kuwa kanuni ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imenifanya mimi kuwa huru mbali na kanuni ya dhambi na mauti.
3 Mana kila sasasindwi seliya panga Mana Yabilelii na ngupu mu yega, Nnongo apangite. Atumite wana wake wakiyake kwa mfano wa yega ya sambi na kwi-ukumu sambi kwa yega.
Kwa maana kile ambacho sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ilikuwa dhaifu katika mwili, Mungu alifanya. Alimtuma Mwana wake wa pekee kwa mfano wa mwili wa dhambi awe sadaka ya dhambi, na akaihukumu dhambi katika mwili.
4 Apangite nyoo langwa kwa seliya gatimu nkati jitu tenga twatujenda bila fuata makowe gamuyega, Ila kwa kotea makowe ga Roho.
Alifanya hivi ili maagizo ya sheria yatimilizwe ndani yetu, sisi tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali kwa kufuata mambo ya Roho.
5 Baba-ikoteya yega waza kwabe makowe ga yenga, lakini ywa ifuata Roho bagawaza ga mwoyo.
Wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili, lakini wale waifuatao Roho huyafikiri mambo ya Roho.
6 Sababu kusudi lya yega ni kiwo, ila nia ya Roho ni ukoto na amani.
Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti, bali nia ya Roho ni uzima na amani.
7 Hayeye kwasababu niya ya yega adui wa Nnongo, sababu itilili seliya ya Nnongo, wataiweza kwa eshimu.
Hii ni kwa sababu ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.
8 Balo baufuata yega baweza kwa kumpendeza Nnongo.
Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
9 Hata nyo, paba bamuyega ila mumwoyo mana itei kweli mu Roho wa Nnongo tama nkati jino. Lakini mundu mana ntupu Roho wa Kirisitu jwembe jwake kwako.
Hata hivyo, hampo katika mwili bali katika Roho, kama ni kweli kwamba Roho wa Mungu huishi ndani yenu. Lakini kama mtu hana Roho wa Kristo, yeye si wake.
10 Mana Kirisitu abi nkati yino yega iwile kwa ikowe ya sambi ila mwoyo ubi nkoti kwa ikowe ya haki.
Kama Kristo yumo ndani yenu, mwili umekufa kwa mambo ya dhambi, bali roho ni hai kwa mambo ya haki.
11 Mene itei Roho wa yolo jwa mfufuwite Yesu buka mu kiwo atama nkati yinu, jwembe jwa mfufuwite Yesu buka mukiwo alowa kwipeya yega yinu ya kiwo ukoto kwa ndela ya Roho wake, jwa tama nkati yinu.
Ikiwa Roho wa yule aliyemfufua Yesu kutoka wafu huishi ndani yenu, yeye yule aliyemfufua Kristo kutoka katika wafu ataipa pia miili yenu ya mauti uhai kwa njia ya Roho wake, aishie ndani yenu.
12 Nga nyo bai, mwalongo bangu, twenga tubi na deni, lakini kwa yega kwa tutame kati mwaipendi yega.
Hivyo basi, ndugu zangu, sisi tu wadeni, lakini si kwa mwili kwamba tuishi kwa jinsi ya mwili.
13 Maana mana itei tama kaa ndela ya yega, mwikalibu yo'waa, lakini kwa Roho mugayebeya makowe ga yega, namwenga mwalama.
Maana ikiwa mnaishi kwa jinsi ya mwili, mpo karibu kufa, lakini ikiwa kwa Roho mnayafisha matendo ya mwili, nanyi mtaishi.
14 Mana Kati benge bananchima babe ongozwa na Roho wa Nnongo, haba bana ba Nnongo.
Maana kama ambavyo wengi wanaongozwa na Roho wa Mungu, hawa ni wana wa Mungu.
15 Mana mupoki kwa mwoyo wa utumwa kai hata muyogope. Badala yake, mupoki mwoyo wa panga mwabene, kwako twondolela, “Abba, Tati!”
Kwa kuwa hamkupokea roho wa utumwa tena hata muogope. Badala yake, mlipokea roho ya kufanywa kuwa wana, ambayo kwayo tunalia, “Abba, Baba!”
16 Roho mwene enda kutuakikishia nanyine Roho yito yo panga twenga twabana ba Nnongo.
Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu ya kuwa tu watoto wa Mungu.
17 Mana itei kweli twalowa teswa na jwembe lenga tupate lumbilwa pamope na jwembe.
Ikiwa tu watoto, basi tu warithi pia, warithi wa Mungu. Na sisi tu warithi pamoja na Kristo, ikiwa kwa kweli tunateseka na yeye ili tupate kutukuzwa pamoja naye.
18 Kwa kuwa indabalangilwa mateso ya wakati ngo panga ntupu kilebe nikifananise na utukupu wa wwbonekana kasitu.
Kwa kuwa nayahesabu mateso ya wakati huu kuwa si kitu nikilinganisha na utukufu utakaofunuliwa kwetu.
19 Mana iumbe yoti yenda tazamia kwa tamania kwananchima bonekana kwa mwana wa Nnongo.
Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu.
20 Mana umba na kwembe pangite pae ya ubocho, sio kwa penda mwene, Ila kwa sababu yake jwembe jwa itiisike, Na muli tumaini.
Kwa maana uumbaji pia ulitiishwa chini ya ubatili, si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye aliyevitiisha. Ni katika tumaini
21 Uumbaji wene na wembe wapikitwa uru na buyelwa mu utumwa wo alibika, na kujingiya mu'uru wa utukupu wa bana ba Nnongo.
kwamba uumbaji wenyewe nao utawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, na kuingizwa katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.
22 Tutangite panga umbilwa na wembe wenda minya na teswa kwo minya pamope hata leno.
Kwa maana twajua ya kuwa uumbaji nao pia unaugua na kuteseka kwa uchungu pamoja hata sasa.
23 Nga nyo bai-lii, ila twabene twatubi twa milembo ya Roho- twenga twabembe twenda minya mu nafsi yitu, katulenda pangilwa twa bana, yani kombolelwa kwa yega yitu.
Si hivyo tu, ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho - sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukisubiri kufanywa wana, yaani ukombozi wa miili yetu.
24 Kwa tegemea kwo twati okoyelwa. Lakini satukilandage sabonekine ntupu chatukilendage mana nyai jwakilenda chakibonekana?
Kwa maana ni kwa taraja hili tuliokolewa. Lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana hakuna taraja tena, kwa maana ni nani anayekitarajia kile akionacho?
25 Ila makatukilenda kilebe cha tukotoka kukibona ntupu saburi.
Bali tukikitarajia kitu tusichokiona, twakingojea kwa saburi.
26 Ila nanyonyo-nyo, Roho nembe kutuyangatia kwo dhaifu witu. mana tumanyi lii yupo kati mwaipangilwa, lakini Roho mwene kutulobya kwo minya uweza lii atabaya.
Kwa jinsi iyo hiyo, Roho naye hutusaidia katika udhaifu wetu. Kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
27 Naywembe kwilingulya mioyo na kwitanga akili ya Roho, ywembe loba kwaniaba ya baba aminile, lengana na mapenzi ga Nnongo.
Na yeye aichunguzaye mioyo huijua akili ya Roho, kwa sababu huomba kwa niaba yao walioamini kulingana na mapenzi ya Mungu.
28 Natwenga tutangite panga bote babampendi Nnongo, jwembe tenda kila kilebe pamo na wema, kwa balo babakemilwe kwa likusudi lyake.
Nasi twajua ya kuwa kwa wote wampendao Mungu, yeye hufanya mambo yote pamoja kwa wema, kwa wale wote walioitwa kwa kusudi lake.
29 Mana balo boti bapangite buka zamani, atikwa sawa buka zamani afananisa na mwana wake, lengo jwembe Abe mwelewa kwanza nkati ya alongo baingi.
Kwa sababu wale wote aliowajua tangu asili, pia aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miogoni mwa ndugu wengi.
30 Na balo basawile buka zamani, na bembe akemite, na balo bakemilwe, habo abatangite bai na haki. Na balo babalangilwe muhak, na bembe atikwalumba.
Na wale aliowachagua tangu asili, hao aliwaita pia. Na wale aliowaita, hao aliwahesabia haki. Na wale aliowahesabia haki, hao pia akawatukuza.
31 Tubaye buli kuhusu ikowe yee? Nnongo Mana abile upande witu, nyai jwa ba kunani jitu?
Tuseme nini basi juu ya mambo haya? Mungu akiwa upande wetu, ni nani aliye juu yetu?
32 Jwembe jwa kotwike kuneka mwana wake mwene ila atikumpiya kwa ajili yitu twenga twaboti alowa kosa buli kutukilimia na makowe goti pamoja na jwembe?
Yeye asiyemwachilia mwana wake mwenyewe bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?
33 Nyai awesa kuwasitaki ateule wa Nnongo? Nnongo mwene kwaesabia haki.
Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.
34 Nyai jwalowa kumwukumu adhabu? Kirisitu Yesu nga jwawile kwaajili yinu, na zaidi ya goo, jwembe nembe atiyolelwa. Enda tawala pamope na Nnongo na pandu pa heshima, na kai ngatulobya twenga.
Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa kwa ajili yetu, na zaidi ya hayo, yeye pia alifufuliwa. Naye anatawala pamoja na Mungu mahali pa heshima, na tena ndiye anayetuombea sisi.
35 Nyai jwaweza kutubuya mupendo wa Kirisitu? Sikikwa, au utumwa, au tesekwo, au njala, au bula, au hatari, au lipanga?
Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Dhiki, au shida, au mateso, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
36 Kati mwaiandikilwe “Kwa faida yako ni minya lisoba lyoti kutwa. Twabalangilwe nkati ngondolo jwo chinjilwa.”
Kama ilivyoandikwa, “Kwa faida yako tunauawa mchana kutwa. Tulihesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa.”
37 Katika ikowe yee yoti twenga twashindi nkati ya jwembe jwatupendile.
Katika mambo haya yote sisi tu zaidi ya washindi katika yeye aliyetupenda.
38 Mana niyomwile kongeka panga at ntuwi, wala ukoto, wala malaika, wala utawala, wala ilebe yaibile, wala ilebe yai isa wala ngupu,
Kwa maana nimekwisha kushawishika kwamba wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala mamlaka, wala vitu vilivyopo, wala vitu vijavyo, wala nguvu,
39 Wala yaibi kunani, Wala gagabile pae wala kyumbe sengi chote, kiweza-kwa kutubangania no upendo wa Nnongo, jwembe nga Kirisitu Yesu Nngwana witu.
wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote, hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu, ambaye ni Kristo Yesu Bwana wetu.

< Arumi 8 >