< Ufunuo 21 >

1 Boka po namweni maunde yaayambe ni kilambo chayambe, kwa kuwa maunde ya kwanza ni kilambo sa kwanza ipitike, ni bahari yabile ntopo.
Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, kwa kuwa mbingu ya kwanza na nchi ya kwanza zimekwishapita, na bahari haikuwepo tena.
2 Nabweni mji mtakatifu, Yerusalem yayambe, wauichile pae boka kumaunde kwa Nnongo, utiandaliwa kati bibi harusi bampambike kwa ajili ya nchengowe.
Niliona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ambao ulikuja chini kutoka mbinguni kwa Mungu, ulioandaliwa kama bibi harusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe.
3 Nayowine lilobe likolo boka pakiteo sa enzi yatibaya, “Lola! makao ya Nnongo yabile pamope ni wanadamu, naye alwatama pamope nabo. Bapanga bandu bake, ni Nnongo mwene apanga Nnongo wabe.
Nilisikia sauti kubwa kutoka kwenye kiti cha enzi ikisema, “Tazama! Makao ya Mungu yapo pamoja na wanadamu, naye ataishi pamoja nao. Watakuwa watu wake, na Mungu mwenyewe atakuwa nao na atakuwa Mungu wao.
4 Apakufuta kila moli kutoka katika minyo yinu, ni ntopo kiwo kae ni lombola, ama lela, ama maumivu, makowe ya zamani yapitike.
Atafuta kila chozi kutoka katika macho yao, na hapatakuwa na kifo tena, au kuomboleza, au kulia, au maumivu. Mambo ya zamani yamekwishakupita.
5 Ywembe ywabile, atamile kunani ya kiteo cha enzi atibaya, Lola! napanga makowe goti panga yayambe.” Atibaya, “Andika leno kwa sababu maneno haga ni ya hakika ni kweli.'
Yeye ambaye alikuwa ameketi juu ya kiti cha enzi alisema, “Tazama! Nafanya mambo yote kuwa mapya.” Alisema, “Andika hili kwa sababu maneno haya ni ya hakika na kweli.”
6 Atikunibakiya, “makowe haga yapitike! Nenga ni Alfa na Omega, wanncogo ni wa mwisho. kwa yoyoti ywabona nyota nipala kumpea makano bila ya gharama boka pa kinyanyu sa mache ya ukoti.
Aliniambia, “Mambo haya yalikwisha kupita! Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho. Kwa yeyote aonaye kiu nitampatia kinywaji bila gharama kutoka katika chemchemi za maji ya uzima.
7 Ywembe ywashinda apalarithi makowe haga, ni nipala panga Nnongo wake, ni ywembe apalapanga mwana wango.
Yeye ashindaye atayarithi mambo haya, na nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
8 Lakini kati yaibile kwa bayogopa boti, bangaliamini, babauchi, bababulaga, wamalaya, babe, waabudu inyago, ni wabocho boti sehemu yabe ipala panga katika ziwa lya mwoto wa kiberiti wautiniya. Ago nga mauti gana ibele.” (Limnē Pyr g3041 g4442)
Lakini kama ilivyo kwa waoga, wasioamini, wachukizao, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, na waongo wote, sehemu yao itakuwa katika ziwa la moto wa kiberiti uunguzao. Hiyo ndiyo mauti ya pili.” (Limnē Pyr g3041 g4442)
9 Yumo wa malaika saba aichile kwango nee, yumo ywabile ni mabakuli saba yagatwelile mapigo saba ya mwisho ni atibaya, “Iche pano! Nipala kukulaya bibi harusi, nnwawa wa mwana ngondolo.”
Mmoja wa malaika saba alikuja kwangu, mmoja ambaye alikuwa na mabakuli saba yaliyojaa mapigo saba ya mwisho na alisema, “Njoo hapa. Nitakuonesha bibi harusi, mke wa mwana kondoo.”
10 Boka po atikunitola kwakulipite katika Roho pakitombe kikolo ni kilambo naatikunilaya mji mpeletau, Yerusalemu, utiuluka pae boka kumaunde kwa Nnongo.
Kisha alinichukua mbali katika Roho kwenye mlima mkubwa na mrefu na alinionesha mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka chini kutoka mbinguni kwa Mungu.
11 Yerusalemu wabile ni utukufu wa Nnongo, ni uzuri wake wabile kati kito cha thamani, kati maliwe ya kilolo safi lya yaspi.
Yerusalemu ulikuwa na utukufu wa Mungu, na uzuri wake ulikuwa kama kito cha thamani, kama jiwe la kioo safi la yaspi.
12 Wabile ni kingombe kikolo, mnacho wene mnyango komi ni ibele, pamope malaika komi ni ibele munyango. Kunani ya mnyango pabile patiyandikwa malina ya makabila komi ni ibele ya bana ba Israeli.
Ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu wenye milango kumi na miwili, pamoja na malaika kumi na wawili milangoni. Juu ya milango palikuwa pameandikwa majina ya makabila kumi na mawili ya wana wa Israeli.
13 Upande wa mashariki pabile ni mnyango itatu, upande wa kusini minyango itatu, upande wa kaskazini minyango itatu, ni upande wa magharibi minyango itatu.
Upande wa mashariki palikuwa na milango mitatu, upande wa kusini milango mitatu, upande wa kaskazini milango mitatu, na upande wa magharibi milango mitatu.
14 Kingombe cha mji yabile ni misingi komi ni ibele, ni kunani yake pabile ni malina komi ni ibele ya mitume komi ni ibele wa mwana ngondolo.
Kuta za mji zilikuwa na misingi kumi na miwili, na juu yake palikuwa na majina kumi na mawili ya mitume kumi na wawili wa Mwana Kondoo.
15 Yumo atilongela na nee abile ni kipimo cha bakola yaitengenezwile na dhahabu kwaajili ya lenga mji mnyango wake ni kingombe chake
Mmoja aliyeongea nami alikuwa na kipimo cha fimbo iliyotengenezwa kwa dhahabu kwa ajili ya kupima mji, milango yake na kuta zake.
16 mji wabekite nkati ya mraba, urefu wake wabile sawa ni upana wakeAtilenga mji kwa kipimo cha fimbo, stadia 12,000 kwa uracho. uracho wake, upana ni kiyemo vyatilingana).
Mji uliwekwa ndani ya mraba; urefu wake ulikuwa sawa na upana wake. Alipima mji kwa kipimio cha fimbo, stadia 12, 000 kwa urefu (urefu wake, upana, na kimo vilifanana).
17 Nyonyo atilenga kingombe chake, ukolo ukolo wake wabile dhiraa 144 kwa vipimo vya kianadamu(ambavyo vyabile vipimo vya malaika).
Vilevile alipima ukuta wake, unene wake ulikuwa dhiraa 144 kwa vipimo vya kibinadamu (ambavyo pia ni vipimo vya malaika).
18 kingombe chabile kichengilwe kwa yaspi ni mji wenge dhahabu safi, kati kilolo safi.
Ukuta ulikuwa umejengwa kwa yaspi na mji wenye dhahabu safi, kama kioo safi.
19 Msingi ya kingombe yabile itipambwa ni kila aina ya liwe lya thamani. Lya kwanza yabile yaspi, lya naibele yabile yakati samawi, lana itatu yabile kalkedon, lya ncheche zumaridi,
Misingi ya ukuta ilikuwa imepambwa na kila aina ya jiwe la thamani. La kwanza lilikuwa yaspi, la pili lilikuwa yakuti samawi, la tatu lilikuwa kalkedon, la nne zumaridi,
20 lya tano Sardoniki, lya sita akiki, lya saba krisolitho, lya nane zabarajadi, lya tisa yakuti ya manjano, lya komi krisopraso, lya komi ni jimo hiakintho, lya komi ni ibele amethisto.
la tano sardoniki, la sita akiki, la saba krisolitho, la nane zabarajadi, la tisa yakuti ya manjano, la kumi krisopraso, la kumi na moja hiakintho, la kumi na mbili amethisto.
21 Mnyango komi ni ibele yabile lulu komi ni ibele, ya kila mnyango watengenezwile boka kwenye lulu jimo. Mitaa ya mji yabile dhahabu safi, yabokine kati kilolo safi.
Milango kumi na miwili ilikuwa lulu kumi na mbili, kila mlango ulitengenezwa kutoka kwenye lulu moja. Mitaa ya mji ilikuwa dhahabu safi, ikionekana kama kioo safi.
22 Namweni kwa hekalu loloti nkati ya mji, kwa luwa Ngwana Nnongo, ywembe mtawala kunani ya vyoti, ni mwana ngondolo ni hekalu lyake.
Sikuona hekalu lolote ndani ya mji, kwa kuwa Bwana Mungu, ambaye anatawala juu ya vyote, na Mwana Kondoo ni hekalu lake.
23 Mji haupalile kwaa lumu ama mwei lenga angaza kunani yake kwa sababu utukufu wa Nnongo watimulika kunani yake, ni taa yake ni mwana ngondolo.
Mji haukuhitaji jua au mwezi ili kungaza juu yake kwa sababu utukufu wa Mungu uliangaza juu yake, na taa yake ni Mwana Kondoo.
24 Mataifa batwanga kwa mbwea wa mji wao. Wafalme wa kilambo baleta fahari yabe nkati yake.
Mataifa watatembea kwa mwanga wa mji huo. Wafalme wa dunia wataleta fahari zao ndani yake.
25 Mnyango yake yajigalikwa kwaa wakati wa mutwekati, ni papanga ntopo kilo palo.
Milango yake haitafungwa wakati wa mchana, na hapatakuwa na usiku pale.
26 Batelanga fahari ni heshima ya mataifa nkati yabe.
Wataleta fahari na heshima ya mataifa ndani yake,
27 Na ntopo kichapu chapala jingiya nkati yake. wala yoyoti ywapanga makowe ni oni ama nakonga hajingiya kwaa, bali balo tu malina yabe yoti yandikwa katika kitabu cha ukoti cha mwana ngondolo.
na hakuna kichafu kitakachoingia ndani yake. Wala yeyote ambaye afanyaye jambo lolote la aibu au udanganyifu hataingia, bali ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana Kondoo.

< Ufunuo 21 >