< Ufunuo 17 >

1 Yumo ywa malaika saba ywabile ni itasa saba kaisa ni kunimakiya, “Uichange, nalowa kukubonikiya hukumu ya kahaba nkolo ywatama nnani ya mase
Mmoja wa malaika saba aliyekuwa na vitasa saba alikuja na kuniambia, “Njoo, nitakuonesha hukumu ya kahaba mkuu akaaye juu ya maji mengi,
2 mengi, ywabile mpwalume ba nnema bapangite makowe ga uzinzi niywembe ni nnani ya mvinyo wa umalaya bake watama mu'dunia watileweshwa.
ambaye wafalme wa nchi wamefanya mambo ya uzinzi naye na juu ya mvinyo wa uzinzi wake wakaao duniani wameleweshwa.”
3 Malaika kantola mu'roho mpaka mupongote, na nimweni nnwawa atami nnani ya mnyama nkele ywabile ni maina ga matukangano. Mnyama ywabile ni ntwe saba ni mbembe komi.
Malaika akanichukua katika Roho mpaka nyikani, na nilimwona mwanamke amekaa juu ya mnyama mwekundu aliyejaa majina ya matukano. Mnyama alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.
4 Ywa nnwawa atiwala ngobo ya zambarau ni ngele ni apambwilwe kwa dhahabu, maliwe ga thamani, ni lulu. Abile akamwile kikombe sa dhahabu muluboko lwake sabile ni ilebe ya machukizo ya uchapu wa umalaya wake.
Mwanamke alivikwa nguo ya zambarau na nyekundu na amepambwa kwa dhahabu, mawe ya thamani, na lulu. Alikuwa ameshikilia mkononi mwake kikombe cha dhahabu kilichojaa vitu vya machukizo ya uchafu wa uasherati wake.
5 Nnani ya paji lyake liyandikilwe lina lya siri: “BABELI NKOLO, MAO BA MAKAHABA NI ILEBE YA MACHUKIZO GA NNEMA.”
Juu ya paji la uso wake limeandikwa jina la siri: “BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA YA VITU VYA MACHUKIZO YA NCHI.”
6 Namweni ya kuba nnwawa yoo abile atilebata wimbi kwa mwai ya baumini ni mwai ya balo bawile kwaajili ya Yesu. Mana kabamweni, nabile ni mshangao nkolo.
Nikaona ya kuwa mwanamke huyo alikuwa amelewa kwa damu ya waumini na damu ya waliokufa kwa ajili ya Yesu. Wakati nilipomwona, nilikuwa na mshangao mkuu.
7 Lakini malaika kanibakiya, “Kwa mwanja namani watishangala? Nalowa kukubakiya maana ya yolo nnwawa ni mnyama ywantolile(mnyama ywabile ni ntwe saba na mbembe komi).
Lakini malaika akaniambia, “Kwa nini unashangaa? Nitakueleza maana ya mwanamke na mnyama amchukuaye (mnyama huyo mwenye vichwa saba na zile pembe kumi).
8 Mnyama ywamweni abile, ni abile kwa leno, lakini tayari kupanda kuoma mu'yembwa lyange yomoka. Boka po kayendelya ni uharibifu. Balo batamii nnani ya nnema, balo babile maina yabe yaandikilwe kwaa mu'kitabu cha ukoti tangu kubekwa misingi ya nnema-batishangala batimwona mnyama ywabile, kuwa yabile kwaa leno, lakini ywabile karibu kuyenda. (Abyssos g12)
Mnyama uliyemwona alikuwepo, hayupo tena sasa, lakini yuko tayari kupanda kutoka katika shimo lisilo na mwisho. Kisha ataendelea na uharibifu. Wale wakaao juu ya nchi, wale ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu - watashangaa wamwonapo mnyama aliyekuwepo, kwamba hayupo sasa, lakini yupo karibu kuja. (Abyssos g12)
9 Wito wolo ni kwaajili ya malango ga hekima. Mitwe saba nga itombe saba yabile nnwawa atami nnani yake.
Wito huu ni kwa ajili ya akili zilizo na hekima. Vichwa saba ni milima saba ambapo mwanamke alikaa juu yake.
10 Ni kae nga apwalume saba. Apwalume atano gatombwike, yumo abile, ni wenge aichile kwaa bado; muda baichile, walowa tama kwa muda mwipi.
Nayo pia ni wafalme saba. Wafalme watano wameanguka, mmoja yupo, na mwingine hajaja bado; wakati atakapokuja, atakaa kwa muda mfupi tu.
11 Mnyama ywabile, lakini ywabile, ywembe kae nga mpwalume wa nane; lakini nga yumo nkati ya balo apwalume saba, na atiyenda mu'uharibifu.
Mnyama aliyekuwepo, lakini sasa hayupo, yeye pia ni mfalme wa nane; lakini ni mmoja wa wale wafalme saba, na anaenda kwenye uharibifu.
12 Mbembe komi wazibweni nga apwalume babapokeyilwe upwalume, lakini kabapokya mamlaka kati apwalume kwa lisaa limo mpamo ni mnyama.
Zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi ambao hawajapokea ufalme, lakini watapokea mamlaka kama wafalme kwa saa moja pamoja na mnyama.
13 Haba banashauri yumo, ni kabampeya ngupu yabe ni mamlaka yolo mnyama.
Hawa wana shauri moja, na watampa nguvu zao na mamlaka yule mnyama.
14 Kabapanga vita kati yabe na mwana ngondolo. Lakini mwana ngondolo alowa kubashinda kwa mana nga Ngwana wa mangwana na Mpwalume ba apwalume-na mu'ywembe twakemilwe, tuchaulilwe, baaminifu.”
Watafanya vita baina yao na Mwana kondoo. Lakini Mwana kondoo atawashinda kwa sababu ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme - na katika yeye tuliitwa, tulichaguliwa, waaminifu.”
15 Mamlaka kanibakiya, “Galo mache gaugabweni, kabatama yolo malaya nga bandu, makutano, mataifa na lugha.
Malaika akaniambia, “Yale maji uliyoyaona, hapo alipoketi yule kahaba ni watu, makutano, mataifa na lugha.
16 Mbembe komi zauzibweni-zabile ni yolo mnyama kabanchukiya yolo kahaba. Na kabampanga kuba kichake ni kana atewala ngobo, kabaulya bwega wake, ni kabautiniya mwoto.
Zile pembe kumi ulizoziona - hizo na yule mnyama watamchukia yule kahaba. Nao watamfanya kuwa mpweke na uchi, watamla mwili wake, na watauteketeza kwa moto.
17 Mana Nnongo abekile mumyoyo yabe ni kupotwa kusudi lyake kwa makubaliano ga kumpeya mnyama ngupu kuntawala mpaka maneno ya Nnongo gabatimya.
Maana Mungu ameweka mioyoni mwao kubeba kusudi lake kwa makubaliano ya kumpa mnyama nguvu zao kumtawala mpaka maneno ya Mungu yatakapotimia.
18 Yolo nnwawa wamweni nga mji wolo ubile nkolo wautawala nnani ya afalme ba nnema.”
Yule mwanamke uliyemwona ni mji ule mkubwa utawalao juu ya wafalme wa nchi.”

< Ufunuo 17 >