< Ufunuo 16 >

1 Nayowine lilobe likolo kuoma kwa pandu paapeletau ni itibaya kwa balo malaika saba, “Uyende ni kumwaga nnani ya lunia mabakuli ga dhahabu ga Nnongo.”
Nikasikia sauti kubwa ikiita kutoka kwenye sehemu ya patakatifu na ikasema kwa wale malaika saba, “Nenda na ukamwage juu ya dunia mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu.”
2 Malaika ba kwanza kayenda ni kumwaga bakuli lyake mu'lunia; ilonda mbaya ni yabile ni maumivu makale yatiisa kwa bandu babile ni alama ya mnyama, kwa balo batikumwabudu sanamu ywake.
Malaika wa kwanza alienda na kumwaga bakuli lake katika dunia; majeraha mabaya na yenye maumivu makali yalikuja kwa watu wenye alama ya mnyama, kwa wale ambao waliabudu sanamu yake.
3 Malaika wanaibele amwayite libakuli lyake mubahari; yabile kati mwai ya mundu ywatiwaa, ni kila kiumbe kibile kikoti mubahari satiwaa.
Malaika wa pili alimwaga bakuli lake katika bahari; ikawa kama damu ya mtu aliyekufa, na kila kiumbe hai katika bahari kilikufa.
4 Malaika ba tatu amwayite bakuli lyake mu'mito ni mu'chemichemi za mase; zabile mwai.
Malaika wa tatu akamwaga bakuli lake katika mito na katika chemichemi za maji; zikawa damu.
5 nayowine malaika wa mase kabaya, “Wenga wa mwaminifu yumo ywaubile ni wabile, Mpeletau-kwa kuwa utuletya hukumu yeno.
Nikasikia malaika wa maji akisema, “Wewe ni mwaminifu - mmoja uliyepo na uliyekuwako, Mtakatifu - kwa sababu umezileta hukumu hizi.
6 Kwa mana wamwayite mwai za baamini ni manabii, utikwapeya balo kunywea mwai; nga kabastahili.”
Kwa sababu walimwaga damu za waamini na manabii, umewapa wao kunywa damu; ndicho wanachostahili.”
7 Nayowine madhabahu yatikuyanga, “Eloo! Ngwana Nnongo ywabile ni utawala nnani ya ilebe yoti, hukumu zako ni kweli ni zabile ni haki.
Nikasikia madhabahu ikijibu, “Ndiyo! Bwana Mungu mwenye kutawala juu ya vyote, hukumu zako ni kweli na za haki.”
8 Malaika wa ncheche ngamwaite kuoma kulibakuli lyake nnani ya liumu, ni kulipeya ruhusa kutiniya bandu kwa mwoto.
Malaika wa nne akamwaga kutoka kwenye bakuli lake juu ya jua, na likapewa ruhusa kuunguza watu kwa moto.
9 Batiniyilwe kwa lyoto lyakutisha, na kabakupuru lineno lya Nnongo, ywabile ni ngupu nnani ya mapigo goti. Batubu kwaa wala kumpeya ywembe utukufu.
Waliunguzwa kwa joto lenye kutisha, na wakalikufuru neno la Mungu, mwenye nguvu juu ya mapigo yote. Hawakutubu wala kumpa yeye utukufu.
10 Malaika atano amwayite kuoma kulibakuli lyake mu'iteo ya enzi sa mnyama, ni libendo lyatiunika upwalume bake. Batisaga mino mu'maumivu makale.
Malaika wa tano akamwaga kutoka kwenye bakuli lake katika kiti cha enzi cha mnyama, na giza likaufunika ufalme wake. Walisaga meno katika maumivu makali.
11 Kabantukana Nnongo bakumaunde kwamana maumivu yabe ni majeraha yabe, ni balo batiyendelya kutubu kwaa chelo chakipanga.
Wakamtukana Mungu wa mbinguni kwa sababu ya maumivu yao na majeraha yao, na bado waliendelea kutokutubu kwa kile walichotenda.
12 Malaika ba sita kabamwaga mu'bakuli lyake mu'nto nkolo. Frati, ni mache yake yatikauka ili kuweza kuandaa ndela ya apwalume baikite kuoma mashariki.
Malaika wa sita alimwaga kutoka kwenye bakuli lake katika mto mkubwa, Frati, na maji yake yakakauka ili kuweza kuandaa njia kwa wafalme watakaokuja kutoka mashariki.
13 Naibona roho tatu chapu yatibonekana kati chura baboka panja ya nkanwa wa yolo ng'ambo, yolo mnyama, ni yolo nabii wa uongo.
Nikaona roho tatu chafu zilizoonekana kama chura watokao nje ya mdomo wa yule joka, yule mnyama, na yule nabii wa uongo.
14 Ni roho ya nchela zalowa panga ishara ni miujiza. Babile kabayenda kwa mpwalume ba lunia yoti ili weza kubakusanya pamope kwa vita mu'lisoba kolo lya Nnongo, ywabile ntawala nnani ya goti.
Ni roho za pepo zitendazo ishara na miujiza. Walikuwa wakienda kwa wafalme wa dunia yote ili kuweza kuwakusanya pamoja kwa vita katika siku kuu ya Mungu, mwenye kutawala juu ya vyote.
15 (“Linga! Nilowa isa kati mwii! Heri yolo ywadumu mu'nkesha, ywatunzaye ngobo yake ili yendya panja bila wala ngobo ni kuionia oni yake.”)
(“Tazama! Ninakuja kama mwizi! Heri yule adumuye katika kukesha, atunzaye mavazi yake ili asiweze kwenda nje uchi na kuiona aibu yake.”)
16 Kabanletike pamope pandu pakemelwage kiebrania Amagedoni.
Waliwaleta pamoja katika sehemu iliyoitwa katika kiebrania Amagedoni.
17 Malaika wa saba amwaite kuoma mu'libakuli lyake mu'anga. Boka po lilobe lyayowanike kuoma kutakatifu ni mu'iteo ya enzi, lyabayite, “Iyomwike!”
Malaika wa saba alimwaga kutoka kwenye bakuli lake katika anga. Kisha sauti kuu ikasikika kutoka pakatifu na kutoka kwenye kiti cha enzi, ikisema, “Imekwisha!”
18 Pabile ni miale ya mbweya ba radi, ngurumo, ishindo ya radi, ni lilendemo lyakutisha-lilendemo likolo lya bui lyapangite kwaa mu'dunia tangu bandu babile tama mu'dunia, eyo nga lilendemo likolo muno.
Kulikuwa na miale ya mwanga wa radi, ngurumo, vishindo vya radi, na tetemeko la kutisha - tetemeko kubwa la ardhi ambalo halijawahi kutokea duniani tangu wanadamu wamekuwepo duniani, hivyo ni tetemeko kubwa zaidi.
19 Mji nkolo wapapwanike mu'ipande itatu, ni ijiji ya mataifa yayogolilwe. Boka po Nnonga kankumbusha nkolo wa Babeli, ni kuupea mji woo kikombe chabile ni divai kuoma kwa ghadhabu yake yabile kale.
Mji mkuu uligawanyika katika sehemu tatu, na miji ya mataifa ikaanguka. Kisha Mungu akamkumbusha Babeli mkuu, na akaupa mji huo kikombe kilichokuwa kimejaa divai kutoka kwenye ghadhabu yake iliyo kali.
20 Kila kisiwa chaboyite na itombe yoti yangana bonekine kae.
Kila kisiwa kikapotea na milima haikuonekana tena.
21 Ula ngolo ya maliwe, yabile ni uzito wa talanta, yatombwike kuoma kumaunde nnani ya bandu, ni kabamlaani Nnongo kwa mapigo ga ula ya maliwe kwa mana lelo pigo lyabile baya muno.
Mvua kubwa ya mawe, ikiwa na uzito wa talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya watu, na wakamlaani Mungu kwa mapigo ya mvua ya mawe kwa sababu lile pigo lilikuwa baya sana.

< Ufunuo 16 >