< Ufunuo 13 >

1 Boka po ling'ambo latiyema kunani ya miangi ufukweni mwa bahari. Boka po namweni mnyama kaboka mu'bahari. Abile ni mbembe komi ni mitwe saba. Katika mbembe yake mwabile ni litaji komi, na katika mutwe wake mwabile manene yankufuru Nnongo.
Kisha joka alisimama juu ya mchanga ufukwe wa bahari. Kisha nikaona mnyama akitoka kwenye bahari. Alikuwa na pembe kumi na vichwa saba. Katika pembe zake kulikuwa na taji kumi, na katika kichwa chake kulikuwa na maneno ya kufuru kwa Mungu.
2 Ayu mnyama wanimweni kati hobe. Magolo kati dubu, nkano wabile kati imba, nayuu ligambo atikumpeya ngupu ni katika iteo cha enzi, ni mamlaka yene ngupu muno ya tawala.
Huyu mnyama niliyemuona ni kama chui. Miguu yake ilikuwa kama ya dubu, na mdomo wake ulikuwa kama wa simba. Yule joka akampa nguvu, na katika kiti chake cha enzi, na mamlaka yenye nguvu sana ya kutawala.
3 Mtwee wa mnyama yumo kati be chatibonekana nalibokaa likolo ambalo lipalae sababisha mauti gake. Lakini libanga lyake latipona. ni kilambo soti satisangala ni kumkengama mnyama.
Kichwa cha mnyama mmojawapo kilionekana kuwa na jeraha kubwa ambalo lingesababisha mauti yake. Lakini jeraha lake likapona, na dunia yote ikashangazwa na ikamfuata mnyama.
4 Eloo ni kumwabudu ling'ambo, apeilwe mamlaka yolo mnyama. Batiendelea longela, “nyai kati mnyama? ni nyai wakombwana kwee?”
Pia wakamwabudu joka, maana alimpa mamlaka yule mnyama. Wakamwabudu mnyama pia, na wakaendelea kusema, “Nani kama mnyama? na “Nani atapigana naye?”
5 Mnyama apeyilwe nkano linga alongele makowe ga matusi batikumruusu kuwa ni utawala kwa miei arobaini na ibele.
Mnyama akapewa mdomo ili azungumze maneno ya kujisifu na matusi. Aliruhusiwa kuwa na mamlaka kwa miezi arobaini na miwili.
6 Nga nyoomnyama atiumukwa nkano longela matusi baina ya Nnongo, atitukana lina lyake, pakilambo patamage balo batamage kumaunde.
Hivyo mnyama alifungua mdomo wake kuongea matusi dhidi ya Mungu, akalitukana jina lake, eneo alililokuwa akiishi na wale wanaoishi mbinguni.
7 Mnyama atiruhusiwa kupanga vita ni baamini na kubashinda. Pia, apeilwe mamlaka kunani ya kila kabila, bandu, lugha ni taifa.
Mnyama aliruhusiwa kufanya vita na waamini na kuwashinda. Pia, alipewa mamlaka juu ya kila kabila, watu, lugha na taifa.
8 Boti batami mukilambo watamwabudu yembe, boka umbaji kwa kilambo, kati kitabu cha ukoti ambacho ni cha mwana wa ngondolo, ambaye atichinjwa.
Wote walioishi duniani watamwabudu yeye, kila mmoja ambaye jina lake halijaandikwa, toka uumbaji wa dunia, katika kitabu cha uzima, ambacho ni cha Mwana Kondoo, ambaye alichinjwa.
9 Mana ipangite yeyoti abi ni likutu, ni ayowe.
Ikiwa yeyote ana sikio, na asikilize.
10 Mana ipangite mundu yumo batikumtola kwa ngupu, ni atiyenda kwa ngupu, yumo abulaga kwa lipanga, kwa lipanga ubulagwa. Hawo nga mkemao wa utlivu ni uvumilivu ni amani haba babile watakatifu.
Ikiwa mmojawapo amechukuliwa mateka, na kwenye mateka ataenda. Ikiwa mmojawapo ataua kwa upanga, kwa upanga atauawa. Huu ni mwito wa utulivu na uvumilivu na imani kwa hao walio watakatifu.
11 Namweni mnyama ywenge kaicha boka mu, kilambo. Abile mwene mbembe ibele kati ngondolo ni atilongela kati mng'ambo.
Tena nikaona mnyama mwingine anakuja kutoka katika nchi. Alikuwa mwenye pembe mbili kama kondoo na akazungumza kama joka.
12 Atilaya mamalaka yoti ya katika mnyama yolo ywa kwanza katika uwepo wake, ni panga katika kilambo na baro baishi wakimuabudu yolo mnyama wakwanza, yolo libaka lyake liponike.
Alionyesha mamlaka yote katika mnyama yule wa kwanza katika uwepo wake, na kufanya katika dunia na wale walioishi wakimuabudu yule mnyama wa kwanza, yule ambaye jeraha lake limepona.
13 Apangite miujiza yenye ngupu, hata panga mwoto kuruka nkati ya kilambo boka kumaunde nnonge ya bandu.
Akafanya miujiza yenye nguvu, hata akafanya moto ushuke katika dunia kutoka mbinguni mbele ya watu,
14 ni kwa ishara atiruhusiwa panga, atikuwakonga balo baatama mukilambo, akiabakiya tengeneza kinyago kwa heshima a mnyama aba ambaye atijeruiwa kwa lipanga, lakini bado katama.
na kwa ishara aliruhusiwa kufanya, akawadanganya hao wakaao katika dunia, akiwaambia kutengeneza sanamu kwa heshima ya mnyama ambaye alikuwa amejeruhiwa kwa upanga, lakini bado aliishi.
15 Atikuruhusu pia mbumo katika kinyango sa mnyama yolo kinyango iweze baya ni sababisha balo boti bakani kuabudu mnyama ba'awee.
Aliruhusiwa kutoa pumzi katika ile sanamu ya mnyama ili sanamu iweze kusema na kusababisha wale wote waliokataa kumwabudu mnyama wauawe.
16 Pia atikuwalazimisha kila yumo, ngaa abile kwaa samani ni mwene ngupu, tajiri, ni maskini, huru ni mmanda, poke alama katika luboko lwa kuume au pakibonge.
Pia akalazimisha kila mmoja, asiye na thamani na mwenye nguvu, tajiri na maskini, huru na mtumwa, kupokea alama katika mkono wa kuume au katika paji la uso.
17 Yabile iwezekana kwaa kila mundu apeme au mbala pema isipokuwa mwene alama ya mnyama, ni yeno namba yene indabaya lina lyake.
Ilikuwa haiwezekani kwa kila mtu kuuza au kununua isipokuwa mwenye alama ya mnyama, na hii ni namba yenye kuwakilisha jina lake.
18 Ayee ipalikwa busara. Ikiwa yeyoti anafahamu, munleke ili apange hesabu ya namba ya mnyama, mana namba yakibinadamu. Namba yake 666.
Hii inahitaji busara. Ikiwa yeyote ana ufahamu, mwache aweze kufanya hesabu ya namba ya mnyama. Maana ni namba ya kibinadamu. Namba yake ni 666.

< Ufunuo 13 >