< Mathayo 7 >

1 Kana uhukumu, ni wenga walowa hukumilwa.
Usihukumu, nawe usije ukahukumiwa.
2 Kwa hukumu yalowa kubahukumu benge, ni wenga walowa hukumilwa. Kwa kipimo sa upimite ni wenga walowa pemelwa chechelo.
Kwa hukumu unayohukumu, nawe utahukumiwa. Na kwa kipimo unachopima na wewe pia utapimiwa hicho hicho.
3 Mwanja namani ulolekipande cha kibile muliyo lya nnongowo, lakini utanga kwaa lipekete lya libile muliyo lyako?
Na kwa nini unatazama kipande cha mti kilichoko kwenye jicho la ndugu yako, lakini hutambuwi kipande cha gogo ambalo limo katika jicho lako?
4 Uweza buli baya kwa nongowo, linda nikubuye kipande sa kibile muliyo lya nongowo, wakati wabile ni lipekete mu'liyo lyako?
Unawezaje kusema kwa ndugu yako, ngoja nikutolee kipande kilichomo kwenye jicho lako, wakati kipande cha gogo kimo ndani ya jicho lako?
5 Wannafiki wenga, “wete uboye lipekete lyalibile muliyo lyako, ngauweza kuliboa kinanoga ni kummoya nongowo lyalibile muliyo lya nnongowo.
Mnafiki wewe; kwanza toa gogo lililomo kwenye jicho lako, na ndipo utakapoweza kuona vizuri na kukitoa kipande cha mti kilichomo kwenye jicho la ndugu yako.
6 Kana uwapei mbwa chakulya kitakatifu, ni kana wataikuli magombe kilebe cha thamani nnonge yabe. Mana balowa kuitahabikya ni kwi lebata kwa magolo, ni kai bakugalambukya wenga ni kukupalangwana ipande ipande.
Usiwape mbwa kilicho kitakatifu, na usiwarushie nguruwe lulu mbele yao. Vinginevyo wataviharibu na kuvikanyaga kwa miguu, na tena watakugeukia wewe na kukurarua vipande vipande.
7 Loba, ni wenga walowa pata, Upate ni wenga walowa kwibonapanga. Upinge hodi, ni wenga wapala yogolelwa.
Omba, nawe utapewa. Tafuta, nawe utapata. Bisha hodi, na wewe utafunguliwa.
8 ywoywoti ywa loba, upokya. Ni ywoywoti ywabisha hodi, apala yogolelwa,
Kwa yeyote anayeomba, hupokea. Na kwa yeyote anayetafuta, hupata. Na kwa mtu ambaye anayebisha hodi, atafunguliwa.
9 Au abile mundu nkati yinu ywabile, mwana wake anobite kipande sa nkate apala mpei liwe?
Au kuna mtu miongoni mwenu ambaye, ikiwa mtoto wake amemwomba kipande cha mkate atampa jiwe?
10 Au maa anobite omab, ni ywembe apala mpeya lingambo?
Au ikiwa atamwomba samaki, na yeye atampa nyoka?
11 Kwa eyo, mana itei mwenga mwabaya mutangite kuwapea wana winu zawadi inogite, je kiasi gani kwa Tate ywabile kumaunde apala kuwapea ilebe inanoga balo bannobite?
Kwa hiyo, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, Je! Ni kiasi gani zaidi Baba aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wanao muomba yeye?
12 Kwasababu eyo, waupala pangilwa ni bandu benge ni wenga wapayi nyonyonyo mana ayee sheria ni manabii.
Kwa sababu hiyo, unapotaka kufanyiwa kitu chochote na watu wengine, nawe pia itakupasa kuwafanyia hivyo hivyo wao. Kwa kuwa hiyo ni sheria na manabii.
13 Mjingi kwo pitya niyango wabana, Mana nnyango nkolo ni ndela ngolo yeyenda kuobi, ni bandu babapeta ndela yoo bananchima.
Ingieni kwa kupitia geti jembamba. Kwa kuwa geti ni pana na njia ni pana inayoongoza kwenye uharibifu, na kuna watu wengi wanaopitia njia hiyo.
14 Nnyango watibana, nnyango wabana ni ndela yeeyenda kuukoti achunu baweza kuibona.
Geti ni jembamba, Geti jembamba ni njia inayongooza katika uzima na ni wachache wanaoweza kuiona.
15 Muiazari ni manabii baubocho, balowaicha bawati likengo lya ngondolo, lakini kumbe kibwa mwitu akale.
Jihadhari na manabii wa uongo, wanaokuja wamevaa ngozi ya kondoo, lakini kweli ni mbweha wakali.
16 Kwa matokeo gabe mwalowa kuwataba, je bandu baweza una matunda gaanoga muichongoma, au tini mukongo wa mbaruti?
Kwa matunda yao mtawatambua. Je watu wanaweza kuvuna matunda kwenye miba, au mtini kwenye mbengu ya mbaruti?
17 Kwa nyoo bai, kila mkongo unanoga upambika matunda gananoga, lakini mkongo mmaya upambika matunda ganoite kwaa.
Kwa jinsi hiyo, kila mti mzuri huzaa matunda mazuri, lakini mti mbaya huzaa matunda mabaya.
18 Mkongo unanoga uweza kwaa pambika matunda yanoite kwaa, ata mkongo unanyata uweza kwa pambika matunda gananoga.
Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri.
19 Kila mkongo waupambika kwaa matunda yanoite walowa taikwa mu mwoto.
Kila mti ambao hauzai matunda mazuri utakatwa na kutupwa katika moto.
20 Nga nyo, mwalowa kwatanga bokana ni matunda gabe.
Hivyo basi, utawatambua kutokana na matunda yao.
21 Si kila mundu ywanikema nenga,'Ngwana, Ngwana,' alowa jingya mu upwalume wa kumaunde, ila yolo ywapanga gagapendike Tate bangu ba kumaunde.
Si kila mtu aniambiaye mimi, 'Bwana, Bwana,' ataingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yule pekee atendaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Bandu bananchima banibakiya lisoba lyo,'Ngwana, Ngwana, twapiyete kwa unabii kwa lina lyako, tukemile kwa masetani kwa lina lyako ni lina lyako twapagite makowe makolo?'
Watu wengi wataniambia siku hiyo, 'Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako, hatukutoa mapepo kwa jina lako, na kwa jina lako tulifanya matendo mengi makuu?'
23 Nga niakokiya wazi,'Niatangite kwaa mwenga! muboke kachango, mwamupanga sambi!'
Ndipo nitawaambia wazi, 'sikuwatambua ninyi! Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu!'
24 Kwa eyo, kila yumo ywayowa maneno gango ni kugatii alowa landana ni mundu mwene lunda ywachengite nyumba yake paliwe.
Kwa hiyo, kila mmoja asikiaye maneno yangu na kutii atafanana na mtu mwenye hekima aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.
25 Ulatiniya machegatitwelyana na mbonga ya tiputa nyumba yoo lakini wawezike kwa bomoka maana ya chengilwa paliwe.
Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuweza kuanguka chini, kwa kuwa ilikuwa imejengwa juu ya mwamba.
26 Namundu jwa liyowa likowe iyango alitikwako aliwapangitwa katimundu ngalunda jwachungite nyumba yake palwangi.
Lakini kila mtu anayesikia neno langu na asilitii, atafananishwa na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga.
27 Ulatisa mafuliko gatiicha mbonga yatipukatya na kwikobwa nyumba yoo! ngobomoka na alibika sana.
Mvua ikaja, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na kuipiga nyumba hiyo. Na ikaanguka, na uharibifu wake ukakamilika.”
28 Wakati yesu payomwi longule makowe gaa bandu batigasangala mapundisho gake.
Ulifika wakati ambao Yesu alipomaliza kuongea maneno haya, makutano walishangazwa na mafundisho yake,
29 Mana apundishike katimundu mwene utawala sio kati waandishi babe
kwa kuwa alifundisha kama mtu mwenye mamlaka, na si kama waandishi wao.

< Mathayo 7 >