< Mathayo 2 >

1 Baada ta Yesu, belekwa mu Bethlehemu ya Uyahudi plyo pa utawala ba mpwalume Herode bandu asomi buka kubwani ya kutalu baisile Yerusalemu kaakoya,
Baada ya Yesu kuzaliwa katika Bethelehem ya Uyahudi katika siku za mfalme Herode, watu wasomi kutoka mashariki ya mbali walifika Yerusalemu wakisema,
2 “ywabile kwaa'ko ywabelekilwe mpwalume Ayahudi? twabweni itondwa yabile mashariki yitu tuisi kumwabudu.
“Yuko wapi yeye ambaye aliyezaliwa Mfalme wa Wayahudi? Tuliiona nyota yake mashariki nasi tumekuja kumwabudu.”
3 Palyo mpwalume Herode payowine atiyogopa, ni Yerusalemu yote pamope ni ywembe.
Pindi Mfalme herode aliposikia haya alifadhaika, na Yerusalemu yote pamoja naye.
4 Herode nga akusanya boti apendo ba makuhani ni baandishi ba bandu, kaalokiya, “Kristo abelekwa kwako?”
Herode akawakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, naye akawauliza, “Kristo atazaliwa wapi?”
5 Kaba koya, “ku'Bethlehemu ya Ayahudi, mana nyon nga yaandikilwe ni manabii,
Wakamwabia, “Katika Bethelehemu ya Uyahudi, kwa kuwa hivi ndivyo ilivyoandikwa na nabii,
6 Ni wenga Bethlehemu, mu, nchi ya ya Yuda, nchunu kwaa nnonge ya iongozi ba Yuda. kwa kuwa kuoma kwako wabile mtawala ywalowa kuwachunga bandu bango ba Israeli.”
Nawe Bethelehemu, katika nchi ya Yuda, si mdogo miongoni mwa viongozi wa Yuda, kwa kuwa kutoka kwako atakuja mtawala atakayewachunga watu wangu Israeli.”
7 Herode kabakema balo asomi kwa siri ni kabakoya muda gani hasa itondwa ipala bonekana.
Hivyo Herode aliwaita wale wasomi kwa siri na kuwauliza ni wakati gani hasa nyota ilikuwa imeonekana.
8 Abatumite ku Bethlehemu, kakoya, “muyende mbolembole mukalaluye muda hasa mwana ywa abelekilwe. Palyo mwalowa m'bona, muniletei habari ili mwanja ni nenga niweche isa ni kumwabudu.”
Akawatuma Bethelehem, akisema, “Nendeni kwa uangalifu mkamtafute mtoto aliyezaliwa. Wakati mtakapomwona, nileteeni habari ili kwamba mimi pia niweze kuja na kumwabudu.”
9 Paba myowine mpwalume, bayei ni mwanja wabe, ni tondwa lelo waibweni ngolo ni yatikuwalongoya mpakanpaluyemi kunani ya mwana pabelekwile.
Baada ya kuwa wamemsikia mfalme, waliendelea na safari yao, na nyota ile waliyokuwa wameiona mashariki iliwatangulia hadi iliposimama juu ya mahali mtoto aliyezaliwa alipokuwa.
10 Palyo paibweni tondwa, bapulaike muno.
Wakati walipoiona nyota, walifurahi kwa furaha kuu mno.
11 Bajingii nnyumba ni bamweni mwana ywa belekilwe ni Mariamu mao bake, batikunolekea ni kunnoba. Baundwi misigo yabe ni kumpeya zawadi ya dhahabu, uvumba ni manemane.
Waliingia nyumbani na kumuona mtoto aliyezaliwa na Mariamu mama yake. Walimsujudia na kumwabudu. Walifungua hazina zao na kumtolea zawadi za dhahabu, uvumba, na manemane.
12 Nnongo atikubaonya mu'ndoto kana bapite kwa Herode, ila babuye kwa ndela yenge.
Mungu aliwaonya katika ndoto wasirudi kwa Herode, hivyo, waliondoka kurudi katika nchi yao kwa njia nyingine.
13 Baada ya kuoma, malaika ba Ngwana ampiye Yusufu mundoto ni kukoya,'Uluka, umpotwe mwana ni mao bake ni m'butukie Misri. Mutame kwoo mpaka pana mmakiya, mwanja Herode apala mwana amulage.
Baada ya kuwa wameondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto na kusema, “Inuka, mchukue mtoto na mama yake na mkimbilie Misri. Bakini huko mpaka nitakapowaambia, kwa kuwa Herode atamtafuta mtoto ili amwangamize.
14 Kilo Yusufu atiyumuka ni kupotwa mwana ni mao bake ni kabutukya Misri.
Usiku huo Yusufu aliamka na kumchukua mtoto na mama yake na kukimbilia Misri.
15 Atami kwoo mpaka Herode awile. Alee litimii lelo likowe lya longei Ngwana pitya kwa anabii, “kuoma Misri ni kemite mwana wango.”
Aliishi huko hadi Herode alipo kufa. Hii ilitimiza kile Bwana alichokuwa amenena kupitia nabii, “Kutoka Misri nimemwita mwanangu.”
16 Boka po Herode pabweni asomi batikonga, atikasirika sana. Alangi kwabulaga bana boti alalome bababile Bethlehemu miaka ibele mpaka pae yake kuoma muda ng'ulo wa akikishe na asomi.
Kisha Herode, alipoona kuwa amedhihakiwa na watu wasomi, alikasirika sana. Aliagiza kuuawa kwa watoto wote wa kiume waliokuwa Bethelehemu na wote katika eneo lile ambao walikuwa na umri wa miaka miwili na chini yake kulingana na wakati aliokuwa amekwisha thibitisha kabisa kutoka kwa wale watu wasomi.
17 Palyo ngalitimii likowe lya alongei mukano wa nabii Yeremia,
Ndipo lilipotimizwa lile neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yeremia,
18 “Lilobe lyayowinike Rmah, kilelo sa lobola muno, Raheli kalelya bana bake, ni akani kumpembelya, mana bawile.”
“Sauti ilisikika Ramah, kilio na maombolezo makubwa, Raheli akiwalilia watoto wake, na alikataa kufarijiwa, kwa sababu hawapo tena.”
19 Herode pawile, linga malaika wa Ngwana atikumpitya Yusufu mu ndoto kaakoya,
Herode alipo kufa, tazama malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri na kusema,
20 “Uluka untole mwana ni mao bake, ni myende mu'nnema ba'Aisraeli kwa maana babau palenge byomi wa mwana bawile.”
“Inuka mchukue mtoto na mama yake, na mwende katika nchi ya Israeli kwa maana waliokuwa wakitafuta uhai wa mtoto wamekufa.”
21 Yusufu kayumuka ngampotwa mwana pamope ni mao bake, kaisa kunnema wa Israel.
Yusufu aliinuka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, na wakaja katika nchi ya Israeli.
22 Lakini payowine panga Arikelau abile katawala Yuda badala ta tate bake Herode. endeyogopa yenda kwao. Baada ya Nnongo kukalipwa kwa lota, atibuka yenda kunnema wa Galilaya.
Lakini aliposikia kuwa Arikelau alikuwa anatawala Yuda mahali pa baba yake Herode, aliogopa kwenda huko. Baada ya Mungu kumuonya katika ndoto, aliondoka kwenda mkoa wa Galilaya
23 ni ayei tama kunnema woo waukemelwa Nazareti. Alee lenga lilimi likowe lyalongei kwa ndela ya manabii, panga alowa kemelwa Mnazareti.
na alienda kuishi katika mji uitwao Nazareti. Hili lilitimiza kile kilichokuwa kimekwisha kunenwa kwa njia ya manabii, kwamba ataitwa Mnazareti.

< Mathayo 2 >