< Marko 10 >

1 Yesu aboi ni kuyenda mkoa wa Uyahudi ni eneo la kulonge ya lupondo Yordani, ni makutano bambengeiye, kabayegana tena, kati ya ibii kawaida yake kutenda.
Yesu aliondoka eneo hilo na akaenda katika mkoa wa Uyahudi na eneo la mbele ya Mto Yorodani, na makutano walimfuata tena. Aliwafundisha tena, kama ilivyokuwa kawaida yake kufanya.
2 Ni Mafarisayo baisi kun'geya, kabanlokiya “ni bwiso nnalome kunneka nyumbo wake?”
Na Mafarisayo walikuja kumjaribu na wakamuuliza, “Ni halali kwa mwanamume kuachana na mke wake?”
3 Yesu kabayangwa, “Musa abakokiye buli?”
Yesu akawajibu, “Musa aliwaamuru nini?”
4 Kabakoya “Musa aloywi kuandika seti sa kurekana ni kumbenga nnwawa.”
Wakasema, “Musa aliruhusu kuandika cheti cha kuachana na kisha kumfukuza mwanamke.”
5 “Mwalowa kunonopa mioyo yinu ndio maana aliwaandikia yino sheria. Yesu kabakokeya.
“Ni kwa sababu ya mioyo yenu migumu ndiyo maana aliwaandikia sheria hii,” Yesu aliwaambia.
6 “Kuoma mwanzo wa uumbaji,'Nnongo aumbike nnwawa ni nnalome.'
“Lakini kutoka mwanzo wa uumbaji, 'Mungu aliwaumba mwanamume na mwanamke.'
7 Nnalome kabaleka tate ni mao bake ni kuungana ni ayumbo bake,
Kwa sababu hii mwanamume atamwacha baba yake na mama yake na ataungana na mke wake,
8 Ni abo abele babamwili gumo, baba ubili kwaa lelo, bali mwili gumo.
na hao wawili watakuwa mwili mmoja; Kwa kuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
9 Eso akitei Nnongo kuba simo kanaaakibangane.”
Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”
10 Wakati bai nnyumba benepunzi bake kabaanlokiya kuhusu leno.
Walipokuwa ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamwuliza tena kuhusu hili.
11 Kabaakokiya, “Ywa anneka nnyumbo wee ni kutola nnwawa wenge, enda libekenya.
Akawaambia, “Yeyote amwachaye mke wake na kumwoa mwanamke mwingine, anafanya uzinzi dhidi yake.
12 Nnwawa ni ywembe mana anneki nsengo wake ni kutolwa ni nnalome ywenge, atenda libelenga.”
Mwanamke naye akimwacha mme wake na kuolewa na mwanamme mwingine, anafanya uzinzi.”
13 Ni bembe kaba nnetia banababe anangota abakamwee, lakini benepunzi kabaakalikiya.
Nao walimletea watoto wao wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wakawakemea.
14 Yesu palyo atangike apulaike kwaa kabaakokeya, “Alekeya bana basunu baise kwango na kana m'bakanikiye, kati bano upwalume wa Nnongo ni wabe.
Lakini Yesu alipotambua hilo, hakufurahishwa nalo kabisa akawaambia, “Waruhusuni watoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie, kwa sababu walio kama hawa ufalme wa Mungu ni wao.
15 Kweli nando kuwalokiya, ywa atami kupokya upwalume wa Nnongo kati mwana nnangota hakika ayingia kwaa kumpwalume wa Nnongo.
Ukweli nawaambia, yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hakika hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu.
16 Kaatola bana mmaboko bake kaabariki kaabekya maboko kunani yabe.
Kisha akawachukua watoto mikononi mwake na akawabariki akiwawekea mikono yake juu yao.
17 Katumbua mwenza wake mundu yumo kambotokiya ni kupiga mayuwa kulonge yake, kanlokiya “mwalimu mwema, ndendebuli niweze kurithi ukoto wa milele?” (aiōnios g166)
Na alipoanza safari yake mtu mmoja alimkimbilia na akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, “Mwalimu Mwema, nifanye nini ili niweze kurithi uzima ya milele?” (aiōnios g166)
18 Yesu kakoya “mwalowa kele ungema mwema? Ntopo aliye mwema ila Nnongo yika yake.
Na Yesu akasema, “Kwa nini unaniita mwema? Hakuna aliye mwema, isipokuwa Mungu peke yake.
19 Uzitangike amri: Kana ubulage, kana ubelenye, kana ubulage, kana uboswee, kana ukoye uboso, uba eshimu tate ni mao bako.”
Unazijua amri: 'Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, usidanganye, mheshimu baba na mama yako'.”
20 Mundu ywa kakoya, “mwalimu gono gote ni gatei tangu nge mwinsembe.”
Mtu yule akasema, “Mwalimu, haya yote nimeyatii tangu nikiwa kijana.”
21 Yesu kanlola ni kumpenda, kankokiya, “Upongwa kilebe kimo. Inapaswa usuluse ilebe yote ubinayo na ubagane akeba, na ubani azina kumbengo. Ndipo uise ungote.
Yesu alimwangalia na kumpenda. Akawambia, “Unapungukiwa kitu kimoja. Unapaswa kuuza vyote ulivyo navyo na uwape masikini, na utakuwa na hazina mbinguni. Ndipo uje unifuate.”
22 Akatike tamaa kwa mayegeyo gano, aboi kauzunika, kwa kubaa aii ni mali ganyansima.
Lakini alikata tamaa kwa sababu ya maelezo haya; aliondoka akiwa mwenye huzuni, kwa kuwa alikuwa na mali nyingi.
23 Yesu aloi kulyo ni kolyo kababakiya benepunzi bake, “buli ni kunonopa matajiri kuyingii kuupwalume wa Nnongo!
Yesu akatazama pande zote na kuwaambia wanafunzi wake, “Ni jinsi gani ilivyo vigumu kwa tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu!
24 Benepunzi batekanganya gano mayaulio. Yesu kabaakokeya yeya, “Bana kunonopa kunonopa kuyingi kupwalume wa Nnongo.
Wanafunzi walishangazwa kwa maneno haya. Lakini Yesu akawaambia tena, “Watoto, ni jinsi gani ilivyo vigumu kuingia katika ufalme wa Mungu!
25 Nantali Ngamia kuyingia mukipole sa sindano kuliko tajiri kuyingi kuupwalume wa Nnongo!
Ni rahisi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano, kuliko mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.”
26 Batekanganya muno kabakoya, “Eyo nyai ataokoka”
Walishangazwa sana na wakasemezana, “Hivyo nani ataokoka”
27 Yesu kabalola ni kukoya, “kwa bandu iwesekana kwaa, lakini sio kwa Nnongo. Kwa Nnongo gote gando wesekan.”
Yesu akawaangalia na kusema, “Kwa binadamu haiwezekani, lakini sio kwa Mungu. Kwa kuwa katika Mungu yote yanawezekana.”
28 Petro katumbua kulongela naye, “lola tulei gote na ttukubengeiye we.”
“Petro akaanza kuzungumza naye, “Angalia tumeacha vyote na tumekufuata.”
29 Yesu kakoya, “ukweli niakokiya mwenga ntopo alei nyumba, mwasage alombo bake, mao bake, tate bake, bana bake, bwee, mwalo wa nee ni mwalo wa Injili,
Yesu akasema, “Ukweli nawaambia ninyi, hakuna aliyeacha nyumba, au kaka, au dada, au mama, au baba, au watoto, au ardhi, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili,
30 Ambaye apokeya kwa mara mia zaidi ya sasa pano Duniani, nsengo, mwasa, nnombo, mao. bana, ni bwee, kwa masaka ni ulimwengu uisaa, ukoto wa milele. (aiōn g165, aiōnios g166)
ambaye hatapokea mara mia zaidi ya sasa hapa duniani: nyumba, kaka, dada, mama, watoto, na ardhi, kwa mateso, na ulimwengu ujao, uzima wa milele. (aiōn g165, aiōnios g166)
31 Bingi ba kwanza baba ba mwiso ni balyo ba mwisho baba ba kwanza.”
Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.”
32 Mundela kabayenda Yerusalem, Yesu abi kulonge yabe. Benepunzi batekanganya ni balyo ai kabaa kota ukyogo kaba yogopa. Yesu kabapinya pambwega balyo komi ni ibele na kutumbwa kuakokeya eso sa mpitia mbeyambe.
Walipokuwa njiani, kwenda Yerusalemu, Yesu alikuwa amewatangulia mbele yao. Wanafunzi walishangaa, na wale waliokuwa wanafuata nyuma waliogopa. Ndipo Yesu akawatoa pembeni tena wale kumi na wawili na akaanza kuwaambia ambacho kitamtokea hivi karibuni:
33 Lola, tuyenda mpaka Yerusalem, ni mwana wa Adamu aikinywa kwaa makuhani akolo ni aandishi. Wataukumu awee ni kumpiya kwa bandu ba mataifa.
“Tazama, tunakwenda mpaka Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atafikishwa kwa makuhani wakuu na waandishi. Watamhukumu afe na watamtoa kwa watu wa Mataifa.
34 Watamdhihaki, bamuunia mata, bampumunda fimbo na kumbulaga. Lakini lisiku nyaitatu ayoka.”
Watamdhihaki, watamtemea mate, watampiga fimbo, na watamwua. Lakini baada ya siku tatu atafufuka.”
35 Yakobo ni Yohana, bana ba Zebedayo, baisi kwake ni kukoya, “Mwalimu tukupala ututtendi sosote sa tukuyopa.”
Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, walikuja kwake na kusema, “Mwalimu, tunakuhitaji utufanyie chochote tukuombacho.”
36 Kabaakokeya, “mpala niatendi kele?
Aliwaambia, “Mnataka niwatendee nini?”
37 Kabakoya “Tupala kutama mwenga nkeya.”
Wakasema, “Turuhusu tukae nawe katika utukufu wako, mmoja katika mkono wako wa kuume na mwingine mkono wako wa kushoto.”
38 Yesu kayangwa, mtangite kwa eso muyopa. muwesa kunywa kikombo eso nannywea nenga au kustahamili ubatizo ago napatizana?
Lakini Yesu aliwajibu, “Hamjui mnachoomba. Mnaweza kukinywea kikombe ambacho nitakiywea au kustahimili ubatizo ambao nitabatizwa?”
39 Kabankokeya “Twando wesa” Yesu kabakokeya, “kikombe eso na nywea mtakinywea. Ni ubatizo ambao kwabe nmebatizwa, mtastahili.
Wakamwambia, “Tunaweza” Yesu akawaambia, “Kikombe nitakachokinywea, mtakinywea. Na ubatizo ambao kwao nimebatizwa, mtaustahimili.
40 Ywa atama kuluboko lwango lwa mmulyo au luboko lwango lwa nkeya nenga kwa wa upiya, kwa balyo ukasabe bayomwile kuandaa.”
Lakini atakayekaa mkono wangu wa kuume au mkono wangu wa kushoto sio mimi wa kutoa, lakini ni kwa wale ambao kwao imekwisha andaliwa.”
41 Balyo benepunzi benge komi ya bayowine gano, kabatumbwa kuakasirikia Yakobo ni Yohana.
Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia haya, wakaanza kuwakasirikia Yakobo na Yohana.
42 Yesu kabakema ni kukoya, “mwandotanga balyo badhaniwa kuba atawala wa bandu ba mataifa huwatawala, Ni bandu babe mashuhuri huwaonyesha mamlaka kunani yabe.”
Yesu akawaita kwake na kusema, “Mnajua kuwa wale wanaodhaniwa kuwa watawala wa watu wa Mataifa huwatawala, na watu wao mashuhuri huwaonyesha mamlaka juu yao.”
43 Lakini upaswa kwaa kuba eno nkati yinu. ywa aba mpendo kati yinu lazima atumikii,
Lakini haipaswi kuwa hivi kati yenu. Yeyote atakaye kuwa mkubwa kati yenu lazima awatumikie,
44 Ni ywa aba wakwanza nkati yinu ni lazima abe mmanda wa bote.
na yeyote atakaye kuwa wa kwanza kati yenu ni lazima awe mtumwa wa wote.
45 Mwalo mwana wa Adamu aisi kwa kutunukiwa bali aisi kutumika, ni kuyaoiya maisha gake kwa faida ya bingi.”
Kwa kuwa Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa bali kutumika, na kuyatoa maisha yake kuwa fidia kwa wengi.”
46 wakaja Yeriko. Palyo kaboka Yeriko ni benepunzi bake ni kipenga sa nyansima, Mwana wa Timayo, Batimayo, kipofu myopaji, atami mmbwega ya ndela.
Wakaja Yeriko. Alipokuwa akiondoka Yeriko na wanafunzi wake na kundi kubwa, mwana wa Timayo, Batimayo, kipofu mwombaji, alikaa kando ya barabara.
47 Palyo ayomi kuba Yesu Mnazareti katumbua kupiya lukalanga kakoya, “Yesu mwana wa DaudiYesu nibonee kiya.
Aliposikia kuwa ni Yesu Mnazareti, alianza kupiga kelele na kusema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!”
48 Bingi kabankoya wa ndolo, kabankokeya anyamale. Lakini kalela kwa sauti ngolo, Mwana wa Daudi nibone kiya!'
Wengi walimkemea yule kipofu, wakimwambia anyamaze. Lakini alilia kwa sauti zaidi, “Mwana wa Daudi, nihurumie!”
49 Yesu kayema ni kukoya akemwe. Kabakoya, baa ngangale! Yinuka! Yesu ando kukema.”
Yesu alisimama na kuamuru aitwe. Walimwita yule kipofu, wakisema, “Kuwa shujaa! Inuka! Yesu anakuita.”
50 Kalitaga pambwega likoti lyake kabutuka kuyenda kwa Yesu.
Akalitupa pembeni koti lake, akakimbia zaidi, na kuja kwa Yesu.
51 Yesu kan'yangwa ni kukoya, “upala nikutendi kele?” Ywa nnalome ndolo kayangwa, “mwalimu nipala kubona.”
Yesu akamjibu na kusema, “Unataka nikufanyie nini?” Yule mwanaume kipofu akamjibu, “Mwalimu, ninataka kuona.”
52 Yesu kambakiya, Yenda, imani yakuponinye.”papo hapo kagagumukuka, ni kunkota Yesu mu ndela.
Yesu akamwambia, “Nenda. Imani yako imekuponya.” Hapo hapo macho yake yakaona; na akamfuata Yesu barabarani.

< Marko 10 >