< Luka 6 >

1 Yesu abile atipeta mu, migunda ya nafaka ni banapunzi bake babile bakitombwanga masuke, bakabasungwanga kati ya luboko lwake bandaliya nafaka.
Sasa ilitokea kwenye Sabato kwamba Yesu alikuwa akipita katika ya shamba la nafaka na wanafunzi wake walikuwa wakichuma masuke, wakayasuguasugua kati ya mikono yao wakala nafaka.
2 Lakini baadhi ya mafarisayo batibaya, “namani upanga kikowe ambacho halali kwaa kisheria kukipanga lichoba lya sabato”?
Lakini baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Kwa nini mnafanya kitu ambacho si halali kisheria kukifanya siku ya sabato”?
3 Yesu atikubajibu, akibaya, “muwaite kwaa soma chelo Daudi chakipangite pabile ni njala, ywembe ni banarome bababile pamope nakwe.
Yesu, akawajibu, akisema, “Hamkuwahi kusoma kile Daudi alifanya alipokuwa na njaa, yeye na wanaume waliokuwa pamoja naye?
4 Atiyenda mu'nyumba ya Nnongo, ni atolite libumunda litakatifu na liya baadhi, ni kuiboya baadhi kwa bandu bababile nakwe lyaa, hatakama ibile halali kwa makuhani lyaa.”
Alikwenda katika nyumba ya Mungu, na akachukuwa mikate mitakatifu na kuila baadhi, na kuitoa baadhi kwa watu aliokuwa nao kuila, hatakama ilikuwa halali kwa makuhani kuila.”
5 Boka po atikuwabakiya, “mwana wa Adamu ni Ngwana wa sabato.”
Kisha akawaambia, “Mwana wa Adamu ni Bwana wa Sabato.”
6 Yabonekine mu'sabato yenge kwamba atiyenda nkati ya sinagogi ni kubapundisha bandu kwa pabile ni mundu ambaye luboko lwake lwa mmaliyo watipooza.
Ilitokea katika Sabato nyingine kwamba alikwenda ndani ya sinagogi na kuwafundisha watu huko. Palikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kulia ulikuwa umepooza.
7 Baandishi ni mafarisayo babile banda kunlinga kwa makini bona kati anyeponya mundu lichoba lya sabato, ili wecha pata sababu ya kumshitaki kwa panga likosa.
Waandishi na Mafarisayo walikuwa wanamwangalia kwa makini kuona kama angemponya mtu siku ya Sabato, ili waweze kupata sababu ya kumshtaki kwa kufanya kosa.
8 Lakini atangite namna cha fikiria na baya kwa mundu ywabile atipooza luboko uyumuka uyema pana kati ya kila yumo.” Nga nyo yolo mundu atikakatuka ni yema palo.
Lakini alijua nini walikuwa wanafikiri na akasema kwa mtu aliyekuwa amepooza mkono, “Amka, simama hapa katikati ya kila mmoja.” Hivyo huyo mtu akanyanyuka na kusimama pale.
9 Yesu atibaya kwabe, “ninda kuwalokiya mwenga ni halali lichoba lya sabato panga mema au panga madharau, kuokoa maisha amakuyaaribu, Boka po atikubalinga boti ni kum'bakiya yolo mundu.
Yesu akasema kwao, “Nawauliza ninyi, ni halali siku ya Sabato kufanya mema au kufanya madhara, kuokoa maisha au kuyaharibu?” Kisha aliwaangalia wote na kumwambia yule mtu,
10 “Nyoosha luboko lwako,” Apangite nyaa, ni luboko lwake labile litinyooka.
“Nyoosha mkono wako.” Akafanya hivyo, na mkono wake ulikuwa umeponywa.
11 Lakini batwelile ni hasira, batilongela bene kwa bene husu namani chapaswa apange kwa Yesu.
Lakini walijawa na hasira, wakaongeleshana wao kwa wao kuhusu nini wanapaswa wafanye kwa Yesu.
12 Yatibonekana machoba ago kwamba atiyenda pakitombe loba, Aatiyendeleya kilo yoti loba Nnongo.
Ilitokea siku hizo kwamba alikwenda mlimani kuomba. Aliendelea usiku mzima kumuomba Mungu.
13 Paibile bwamba, atikubakema benepunzi bake kwake, ni atikuwachawa komi ni ibele kati yabe, ambao pia atikubakema, “Mitume”
Ilipokuwa asubuhi, aliwaita wanafunzi wake kwake, na akawachagua kumi na wawili kati yao, ambao pia aliwaita “mitume.”
14 Majina ya balo mitume yabile Simoni, (ywa pia atikumkema Petro) ni Andrea nnuna wake, Yakobo, Yohana, Filipo, Bartolomayo,
Majina ya wale mitume yalikuwa Simoni (ambaye pia alimwita Petro) na Andrea ndugu yake, Yakobo, Yohana, Filipo, Bartolomayo,
15 Mathayo, Tomaso ni Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni ywa akemwa Zelote,
Mathayo, Tomaso na Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni, ambaye aliitwa Zelote,
16 Yuda mwana wa Yakobo ni Yuda Iskariote, ywa abile msaliti.
Yuda mwana Yakobo na Yuda Iskariote, ambaye alikuwa msaliti msaliti.
17 Boka po Yesu atitelemka pamope nakwe boka mukitombe ni yema mahali palibende. Benepunzi bakr banyansima babile kwo pamope ni bandu benge banyansima boka Uyahudi ni Yerusalem ni boka mbwani ya Tiro na Sidoni. Baichile kumpekanya ni ponywa magonjwa yabe.
Kisha Yesu alitelemka pamoja nao toka mlimani na kusimama mahali tambarare. Idadi kubwa ya wanafunzi wake walikuwa huko, pamoja na idadi kubwa ya watu kutoka Uyahudi na Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni.
18 Bandu babile bandasumbuliwa ni nchela bachapu batiponywa pia.
Walikuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Watu waliokuwa wakisumbuliwa na pepo wachafu waliponywa pia.
19 Kila yumo kwenye lyoo kusanyiko atijaribu kumkamwa kwa sababu ngupu ya uponyaji yabile bonekana nkati yake, ni atikubaponya boti.
Kila mmoja kwenye hilo kusanyiko alijaribu kumgusa kwa sababu nguvu za uponyaji zilikuwa zikitokea ndani yake, na aliwaponya wote.
20 Boka po atikubalinga benepunzi bake, ni baya, “mtibarikiwa mwenga mwa m'bile maskini, kwa maana ufalme wa Nnongo ni winu.
Kisha akawaangalia wanafunzi wake, na kusema, “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini, kwa maana ufalme wa Mungu ni wenu.
21 Mtibarikiwa mwenga mwabile ni njala nambeambe, kwa maana mpala yukuta. Mtibarikiwa mwenga mwamlela nambeambe kwa maana mpala eka.
Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, kwa maana mtashibishwa. Mmebarikiwa ninyi mliao sasa, kwa maana mtacheka.
22 Mtibarikiwa mwenga ambao bandu bapala kubachukianga ni kubatenga ni kubashutumu mwenga kwamba mwa'ovu, kwa ajili ya mwana wa Adamu.
Mmebarikiwa ninyi ambao watu watakapowachukia na kuwatenga na kuwashutumu ninyi kwamba ni waovu, kwa ajili ya Mwana Adamu.
23 Pulaini katika lichoba lyoo ni goloka goloka kwa pulaha, kwa sababu hakika mpala pata thawabu ngolo kumaunde, kwa maana tate bao batikubatenda nyonyonyoo mananbii.
Furahini katika siku hiyo na kurukaruka kwa furaha, kwa sababu hakika mtakuwa na thawabu kubwa mbinguni, kwa maana baba zao waliwatendea vivyohivyo manabii.
24 Lakini ole winu mwabile matajili kwa maana myomwile pata faraja yinu.
Lakini ole wenu mlio matajiri! Kwa maana mmekwisha pata faraja yenu.
25 Ole winu mwabile yukwita nambeambe! kwa mana mpala bona njala baalaye, Ole winu mwamueka nambeambe mpala lomboleza ni lela baalae.
Ole wenu mlio shiba sasa! Kwa maana mtaona njaa baadaye. Ole wenu mnaocheka sasa! Kwa maana mtaomboleza na kulia baadaye.
26 Ole winu mwapala lumbwa ni bandu boti! kwa mana tate bao atikubatenda manabii wa ubocho nyonyonyo.
Ole wenu, mtakaposifiwa na watu wote! Kwa maana baba zao waliwatendea manabii wa uongo vivyohivyo.
27 Lakini nibaya kwinu mwenga mwamunipekaniya, mwapende adui zenu ni kupanga mema kwa babawachukiya.
Lakini nasema kwenu ninyi mnaonisikiliza, wapendeni adui zenu na kufanya mema kwa wanao wachukieni.
28 Mubabariki balo babalaani mwenga ni mubalobii balo babaoneya.
Wabarikini wale wanao walaani ninyi na waombeeni wale wanaowaonea.
29 Kwa ywembe ywa akukombwa shavu limo, mgalauliye ni lya ibelr. Kati mundu akupokonyile jyoho lyako kanamchibi na nganzu.
Kwake yeye akupigaye shavu moja, mgeuzie na la pili. Kama mtu akikunyang'anya joho lako usimzuilie na kanzu.
30 Mbei kila ywa akuloba. Kati mundu akupokonyile kilebe ni mali yako, kana umrobe akubuyanganiye.
Mpe kila akuombaye. Kama mtu akikunyang'anya kitu ambacho ni mali yako, usimuombe akurudishie.
31 Kati ubapendavyo bandu babatendii, ni mwenga mubatendi nyonyonyo.
Kama mpendavyo watu wawatendee, nanyi watendeeni vivyo hivyo.
32 Kati mkiwapenda bandu baba mpendanga mwenga tu, eyo ni thawabu ya namani kwinu” kwa maana hata bene dhambi huwapenda balo babapendile.
Kama mkiwapenda watu wawapendao ninyi tu, hiyo ni thawabu gani kwenu? Kwamaana hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao.
33 Kati mwatendi mema balo bawatendi wema ni mwenga, eyo nga thawabu gani kwinu? kwa mana hata ywabile ni sambi apanga nyoo.
Kama mkiwatendea mema wale wanaowatendea ninyi mema, hiyo ni thawabu gani kwenu? Kwa maana hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo.
34 Kati mwatikunkopesha ilebe kwa bandu mwabile mutegemie kwamba balowa kubabuyanganikiya, eyo nga thawabu gani kwinu? Mana hata balo babile ni sambi balowa kopesha benge sambi benge, ni tegemya pokya kiasi chechelo kae.
Kama mkikopesha vitu kwa watu ambao mnategemea watawarudishia, hiyo ni thawabu gani kwenu? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, na hutegemea kupokea kiasi hicho hicho tena.
35 Lakini mwapende adui zenu ni mwatendei mema. Mubakopeshe ni mhofie kwaa kuhusu kubuyanganikiwa, ni thawabu yinu ipalika kuba ngolo. Mpalikwa kuba bana ba Ywabile kunani, kwa mana ywembe mwene nga mwema kwa bandu babile kwaa ni shukrani ni baovu.
Lakini wapendeni adui zenu na watendeeni mema. Wakopesheni na msihofu kuhusu kurudishiwa, na thawabu yenu itakuwa kubwa. Mtakuwa wana wa Aliye Juu, kwasababu yeye mwenyewe ni mwema kwa watu wasio na shukurani na waovu.
36 Mube ni huruma, kati Tate binu ywabile ni huruma.
Iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.
37 Kana mhukumu, mwenga muhukumilwa kwaa. Kana mulaani, ni mwenga mulaanilwa kwaa. Musamei benge, ni mwenga mwalowa sameelwa.
Msihukumu, nanyi hamta hukumiwa. Msilaani, nanyi hamtalaaniwa. Sameheni wengine, nanyi mtasamehewa.
38 Mwapei benge, mwenga mwalowa peilwa. Kiasi sa ukarimu-chakisindililwe, sukwasukwa ni mwagilwa-mwagilwa mumagoti yinu. Kwamana kwa kipimo chochote mwakitumile pemya, kipimo chechelo chapanga tumilwa kubapemya ni mwenga.
Wapeni wengine, nanyi mtapewa. Kiasi cha ukarimu - kilichoshindiliwa, kusukwasukwa na kumwagika - kitamwagika magotini penu. Kwa sababu kwa kipimo chochote mnachotumia kupimia, kipimo hicho hicho kitatumika kuwapimia ninyi.”
39 Boka po kabamakiya kwa mpwano kae, “Je mundu ywange bona aweza kumwongoza kipofu ywenge? Kati atipanga nyoo, bai boti balowa tombokya mulimbwa, je kana batumbukii?
Kisha akawaambia mfano pia. “Je mtu aliye kipofu aweza kumwongoza mtu mwingine kipofu? Kama alifanya hivyo, basi wote wangalitumbukia shimoni, je wasingetumbukia?
40 Mwanapunzi aweza kwaa kuba nkolo kuliko mwalimu wake, lakini kila mundu kaayomwa pundishwa kwa ukamilifu alowa kati mwalimu bake.
Mwanafunzi hawi mkubwa kuliko mwalimu wake, lakini kila mtu akiisha kufundishwa kwa ukamilifu atakuwa kama mwalimu wake.
41 Mwanja namani bai mwakilola kibanzi nkati ya liyo lya nongo wo, ni wabile ni boriti nkati ya liyo lyako uilola kwaa?
Na kwa nini basi wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti lililo ndani ya jicho lako huliangalii?
42 Waweza kwaa kummakiya nongowo, Nongo wango kiboywe ibanzi mu'liyo lyako, “wenga ulola kwaa boriti yaibile muliyo lyako wa mwene, Nga ubona inanoga kumoywa kibanzi mu'liyo lya nongo bako.
Utawezaje kumwambia ndugu yako, 'Ndugu, naomba nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako,' nawe huangalii boriti iliyo katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Kwanza itoe boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utaona vizuri kutoa kibanzi katika jicho la ndugu yako.
43 Kwamana ntopo nkongo unoyite upambike matunda ganoite kwaa, wala ntopo nkongo unoyite kwaa upambika matunda ganoite.
Kwa sababu hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala hakuna mti mbaya uzaao matunda mazuri.
44 Kwa mana kila nkongo bandu uyowanika kwa matunda gake. Kwamana bandu bachuma kwaa tini boka mu'miba, wala kana bachuma zabibu boka mu'michongoma.
Kwa sababu kila mti hutambulika kwa matunda yake. Kwa sababu watu hawachumi tini kutoka kwenye miba, wala hawachumi zabibu kutoka kwenye michongoma.
45 Mundu mwema mu'hazina njema ya mwoyo wake kumoywa galyo mema, ni mundu mwou mu'hazina mbou ya mwoyo wake umoywa galyo maou. Kwamana ntwe wake ubaya galo gaujazike mwoyo wake.
Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu. Kwa sababu kinywa chake husema yale yaujazayo moyo wake.
46 Kwa namani mwanikema,'Ngwana, Ngwana, na balo muyatendi kwaa galo ganiabakiya?
Kwanini mnaniita, 'Bwana, Bwana', na bado hamyatendi yale nisemayo?
47 KIla mundu ywanikengama nenga ni kugayowa makoweni kugatendii kazi, nalowa kwaonesha ywabile.
Kila mtu ajaye kwangu na kuyasikia maneno yangu na kuyatendea kazi, nitawaonyesha jinsi alivyo.
48 Atilandana ni mundu ywachenga nyumba yake, ywa chimba pae muno, ni kuchenga msingi ba nyumba nnani ya mwamba imara. Mafuriko gaisile, maporomoko ga mase, gaikombwile nyumba, lakini yaweza kwaa kwitikisa, kwa mana yabile ichengwite vizuri.
Anafanana na mtu ajengae nyumba yake, ambaye huchimba chini sana, na kujenga msingi wa nyumba juu ya mwamba imara. Mafuriko yalipokuja, maporomoko ya maji yaliipiga nyumba, lakini hayakuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri.
49 Lakini ywoywoti ywaliyowa neno lyango no kulitii kwaa, mpwano wake ywa mundu ywachengite nyumba nnani ya mbwega pabile kwaa ni msingi, mto wauilukie kwa ngupu, nyumba yelo yapatike maangamizi makolo.
Lakini yeyote asikiaye neno langu na hakulitii; mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ulipoishukia kwa nguvu, nyumba ile ilitopata maangamizi makubwa.

< Luka 6 >