< Baebrania 2 >

1 Kwa eyo tugabeke nnonge galyo tuayowine, kana tuise kulekwa kutalu ni ego.
Kwa hiyo ni lazima tuweke kipaumbele zaidi kwa yale tuliyosikia, ili kwamba tusije tukatengwa mbali nayo.
2 maana sa bakoya malaika ni halali ni kila likoya ni uasi upokya adhabu bai.
Kwa maana ikiwa ujumbe uliozungumzwa na malaika ni halali, na kila kosa na uasi hupokea adhabu tu,
3 Twapata buli kuenguka mana tayari kwa uokou gono nkolo? Uokou waukoiwe ni Ngwana ni kuthibitisha kwitu ni balyo baayowine.
tutapataje kuepuka kama tusipojali wokovu huu mkuu? —wokuvu ambao kwanza ulitangazwa na Bwana na kuthibitishwa kwetu na wale waliousikia.
4 Nnongo iyeya atiuthibitisha kwa ishara, kwa maajabu ni itendo mbalembale, ni zawadi za Roho mtakatifu azibagine kuyendana ni mapenzi gake mwene.
Mungu pia aliuthibitisha kwa ishara, maajabu, na kwa matendo makuu mbalimbali, na kwa zawadi za Roho Mtakatifu alizozigawa kulingana na mapenzi yake mwenyewe.
5 Nnongo aubekite kwaa ulimwengu waisa, tulongelya habari zake, pae ya mamlaka.
Mungu hakuuweka ulimwengu ujao, ambao tunaongelea habari zake, chini ya malaika.
6 Badala yake mundu pulani ashuhuduli mahali pulani kakoya, “Mundu nyai, mpaka unkomboki? au mwana wa mundu, hata antunze?
Badala yake, mtu fulani ameshuhudia mahali fulani akisema, “Mtu ni nani, hata uweze kumkumbuka? Au mwana wa mtu, hata umtunze?
7 Untei mundu kuba nsunu kuliko malaika, ung'walike taji ya utukufu ni heshima(Zingatia gano mayaulio; umbei kunani ya kasi ya maboko gako”ago ago kunakala za kale)
mtu kuwa mdogo kuliko malaika; umemvika taji ya utukufu na heshima. (Zingatia: Katika nakala halisi za kwanza, mstari huu haupo. “Na umemuweka juu ya kazi ya mikono yako.)
8 Ubei kila kilebe pae ya magolo gake, “Eyo Nnongo abei kila kilebe pae ya mundu. Alei kwa kilebe sosote sa kanga bekwa pae yake. Lakini mbeyambe bado tubona kwaa kila kilebe kibi pae yake.
Umeweka kila kitu chini ya miguu yake.” Kwa hiyo Mungu ameweka kila kitu chini ya mtu. Hakuacha kitu chochote ambacho hakiko chini yake. Lakini sasa hivi hatuoni bado kila kitu kikiwa chini yake.
9 Ata eyo tubona ywa antei kwa muda, pae kuliko malaika-Yesu mwalowa kukunda kwake masaka ni kiwo saka wauliywe taji ya utukufu ni heshima. kwa eyo Yesu apaiye kiwo kiwo mwalo wa kila mundu.
Hata hivyo, tunaona ambaye alikuwa amefanywa kwa muda, chini kuliko malaika—Yesu, ambaye, kwa sababu ya mateso yake na kifo chake, amevikwa taji ya utukufu na heshima. Hivyo sasa kwa neema ya Mungu, Yesu ameonja kifo kwa ajili ya kila mtu.
10 Nnongo yabi sawasawa, kila kilebe sabi mwalo wake kupetya ywembe, aletike bana bingi kuutukufu, yalengani kumtenda kiongozi kuuokovu wabe kuba mkamilifu kupetya masaka.
Ilikuwa sahihi kwamba Mungu, kwa sababu kila kitu kipo kwa ajili yake na kupitia yeye, alipaswa kuwaleta watoto wengi katika utukufu, na kwamba alipaswa kumfanya kiongozi katika wokovu wao kuwa mkamilifu kupitia mateso yake.
11 Kwa mana bote abele ywaa abeka wakfu ni balyo babeka wakfu, bote baoma kuasili yimo. Nnongo mwalo gono ywa ababei wakfu, kwa Nnongo abona kwa oni kuakema alongo.
Kwa maana wote wawili yule anayeweka wakfu na wale ambao wanawekwa wakfu, wote wanatoka kwenye asili moja, Mungu. Kwa sababu hii yule anayewaweka wakfu kwa Mungu haoni aibu kuwaita ndugu.
12 Akoya, “Nilikoya lina lyako kwa alongo bako nayemba kuhusu wenga pa kipenga.”
Anasema, “Nitatangaza jina lako kwa ndugu zangu, nitaimba kuhusu wewe kutoka ndani ya kusanyiko.”
13 Kakoya iyeya, “Niamini ywembe.” lelo, “lola pano nibile ni bana ambei Nnongo.”
Tena asema, “Nitaamini katika yeye.” Na tena, “Tazama, hapa nipo na watoto ambao Mungu amenipa.”
14 Bana bote ba Nnongo hushiriki yega ni damu, Yesu ni ywembe alishiriki kupitya waa iliapate kumtombologa ywa abile ni mamlaka baunani ya kiwo, ywenge kwaa ni ibilisi.
Kwa hiyo, kwa kuwa watoto wa Mungu wote hushiriki mwili na damu, kadhalika Yesu alishiriki vitu vilevile, ili kwamba kupitia kifo apate kumdhohofisha yule ambaye ana mamlaka juu ya mauti, ambaye ni ibilisi.
15 Yeno yabi eyo ili kuabeka huru balo bote bai kabayogopa kiwoo. Maisha gabe goti bai abanda.
Hii ilikuwa hivyo ili awaweke huru wale wote ambao kupitia hofu ya kifo waliishi maisha yao yote katika utumwa.
16 Balatu malaika kwa aboayangata. Badala yake, abayangata bana ba Abrahamu.
Kwa hakika siyo malaika anaowasaidia. Badala yake, anawasaidia wazao wa Abraham.
17 Kwa eyo yabi lazima ywembe abi kati nlongo wabe mundila yoti, ili awese kuba kuhani nkolo mwene kuja ni uaminifu kwa ilebe ya Nnongo iyeya abe ni uweso wakupitya msaada kwa bandu bene sambi.
Kwa hiyo, ilikuwa lazima yeye awe kama ndugu zake katika njia zote, ili aweze kuwa kuhani mkuu mwenye huruma na mwaminifu kwa vitu vya Mungu, na ili kwamba awe na uwezo wa kutoa msamaha kwa dhambi za watu.
18 Mwalo Yesu mwene ikundike masaka, ni kugeywa, abi ni uweso wa kuwayangata balyo benge bageywa.
Kwa sababu Yesu mwenyewe ameteseka, na kujaribiwa, ana uwezo wa kuwasaidia wale wanaojaribiwa.

< Baebrania 2 >