< Baebrania 10 >

1 Kwa yelo saliya nga kivuli cha makowe mema yaisa, yalo kwaa gabile halisi. Saliya yange wezekana kubakamilisha balo ambao batikunkaribia Nnongo kwa ndela ya dhabihu zezelo zabile ni makuhani batiyendelya kutoa mwaka baada ya mwaka.
Kwa vile sheria ni kivuli cha mambo mema yajayo, si yale yaliyo halisi. Sheria kamwe haiwezi kuwakamilisha wale ambao wanaomkaribia Mungu kwa njia ya dhabihu zilezile ambazo makuhani waliendelea kutoa mwaka baada ya mwaka.
2 Au vyabile dhabihu izo zawezike kwaa kukoma kutolelwa? Kwa kigezo chelo batiabudu, babile batisafirishwa mara jimo, kababile kwa ni utambuzi muno ba sambi.
Au vinginevyo dhabihu hizo zisingeweza kukoma kutolewa? Kwa kigezo hicho waabuduo, wakiwa wamesafishwa mara moja, wasingelikuwa na utambuzi zaidi wa dhambi.
3 Bali mu'dhabihu mwabile ni ukumbusho wa sambi zapangilwe mwaka baada ya mwaka.
Bali katika dhabihu hizo kuna ukumbusho wa dhambi zilizotendwa mwaka baada ya mwaka.
4 Kwa mana yatiwezekana kwaa mwai ya mafahari ni mbuzi kuziondoa sambi.
Kwa kuwa haiwezekani kwa damu ya mafahari na mbuzi kuziondoa dhambi.
5 Palyo Kristo paisile mudunia, kabaya, “Mutamaniye kwaa matokeo au dhabihu, badala yake, mwatiuandaa yega kwaajili yango.
Wakati Kristo alipokuja duniani, alisema, “Hamkutamani matoleo au dhabihu, badala yake, mliandaa mwili kwa ajili yangu.
6 Mwabile kwaa ni thamani mu'matokeo yoti ya kuteketezwa au dhabihu kwaajili ya sambi.
Hamkuwa na thamani katika matoleo yote ya kuteketezwa au dhabihu kwa ajili ya dhambi.
7 Boka po natibaya, “Lola, pano natiyapanga mapenzi gako, Nnongo, kati yaiandikilwe kunihusu nenga mu'gombo.”
Kisha nilisema, “Ona, hapa ninayafanya mapenzi yako, Mungu, kama ilivyoandikwa kunihusu mimi katika gombo”.
8 Kabaya kati abile abayilwe nnani: “Mwatitamani kwaa dhabihu, matoleo, au sadaka ga kutiniya kwaajili ya sambi, wala kana ubweni puraha nkati yake” dhabihu yabile yaboywile lengana na saliya.
Alisema kama ilivyo semwa hapo juu: “Hamkutamani dhabihu, matoleo, au sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi, wala hukuona furaha ndani yake” dhabihu ambazo zinatolewa kulingana na sheria.
9 Boka po kabaya, “Lola, nabile pano kupanga mapenzi gako.” Abekite mbwega taratibu zabile za mwanzo ili kuimarisha zalo zana ibele.
Kisha alisema, “Ona, niko hapa kufanya mapenzi yako”. Ameweka pembeni taratibu zilizo za awali ili kuimarisha zile za pili.
10 Mu'taratibu zanaibele, twatubile twatitengwa kwa Nnongo kwa mapenzi gake petya kuyitoa yega ya Yesu Kristo mara yimo kwa muda woti.
Katika taratibu za pili, tumekwisha tengwa kwa Mungu kwa mapenzi yake kupitia kujitoa kwa mwili wa Yesu Kristo mara moja kwa nyakati zote.
11 Ibile kweli, kila kuhani uyema kwa huduma lisoba ni lisoba, aboyite dhahabu yeyelo, yabile, kwa vyovyoti, kamwe ywaweza kwaa kuboywa sambi.
Ni kweli, kila kuhani husimama kwa huduma siku kwa siku, akitoa dhabihu ile ile, ambayo, kwa vyovyote, kamwe isingeweza kuziondoa dhambi.
12 Lakini baada ya Kristo kuboywa dhabihu mara yimo kwa sambi milele yoti, atitama luboko lwa mmalyo lya Nnongo,
Lakini baada ya Kristo kutoa dhabihu mara moja kwa dhambi milele yote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu,
13 atisubiri mpaka maadui bake babekwe pae ni kupangwa iteo kwaajili ya magolo gake.
akisubiri mpaka maadui zake watiwe chini na kufanywa kiti kwa ajili ya miguu yake.
14 Kwa mana kwa ndela ya toleo limo atei kwakamilisha milele balo babile batengwa ba Nnongo.
Kwa kuwa kwa njia ya toleo moja amewakamilisha milele wale ambao wametengwa kwa Mungu.
15 Nga Roho mpeletau ywashuhudia kwitu. Kwa mana kwanza kabaya,
Na Roho Mtakatifu pia ashuhudia kwetu. Kwa kuwa kwanza alisema,
16 “Lelo nga liagano nalowa kulipanga pamope nabo baada ya masoba ago; abayite Ngwana: nalowa ibeka saliya yango nkati ya mioyo yabe, nga nalowa andika mu'malango gabe.”
“Hili ni agano nitakalofanya pamoja nao baada ya siku hizo; asema Bwana: nitaweka sheria zangu ndani ya mioyo yao, na nitaziandika katika akili zao”.
17 Boka po kabaya, “Kabazikumbuka kwaa kae sambi ni makowe gabe ga'kiwo.”
Kisha alisema, “Hawatazikumbuka tena dhambi na matendo yao mafu”.
18 Nambeambe pandu pabile ni msamaha kwa aba, ntopo kae dhabihu yoyoti kwaajili ya sambi.
Sasa mahali palipo na msamaha kwa hawa, hakuna tena dhabihu yoyote kwa ajili ya dhambi.
19 Kwa eyo, alongo, twabile ni ujasiri ba jingya pandu patakatifu muno kwa mwai ya Yesu.
Kwa hiyo, ndugu, tunao ujasiri wa kuingia mahali patakatifu zaidi kwa damu ya Yesu.
20 Eyo nga ndela yabile itabilwe kwaajili yitu kwa ndela ya yega yake, mbeyambe ni ukoti yapitii mu'pazia.
Hiyo ni njia ambayo ameifungua kwa ajili yetu kwa njia ya mwili wake, mpya na hai inayopitia kwenye pazia.
21 Nga kwa mana twabile ni kuhani nkolo nnani ya nyumba ya Nnongo.
Na kwa sababu tunaye kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu,
22 nga tumkaribiye ni mwoyo wa kweli mu'utimilifu bake ba uhakika ba imani mana itei twabile ni mwoyo yabilenyunyiziwa safi kuoma ubou wa dhamiri ni kuba ni yega yitu yapeletike ni mase sapi.
na tumkaribie na moyo wa kweli katika utimilifu wa uhakika wa imani tukiwa na mioyo iliyonyunyiziwa safi kutoka uovu wa dhamiri na kuwa na miili yetu iliyooshwa kwa maji safi.
23 Bai nga tukamwe mu'uthabiti toba ya ujasiri ba tumaini litu, bila ya kelebuka, kwa mana Nnongo ywaatiahidi nga mwaminifu.
Basi na tushikilie kwa uthabiti katika ungamo la ujasiri wa tumaini letu, bila ya kugeuka, kwa sababu Mungu aliyeahidi ni mwaminifu.
24 Nga tuyongeye kuiwasa namna ya kumtia mwoyo kila yumo hupenda ni makowe ganoite.
Na tuzidi kutafakari namna ya kumtia moyo kila mmoja kupenda na matendo mema.
25 Nga kana tuleke kukusanyika pamope, kati pakapanga benge. Badala yake, kutiana mwoyo kila yumo zaidi ni zaidi, kati mwatibona lisoba latikaribia.
Na tusiache kukusanyika pamoja, kama wafanyavyo wengine. Badala yake, kutiana moyo kila mmoja zaidi na zaidi, kama muonavyo siku inakaribia.
26 Kati twatupanga kusudi kuyendelya kupanga sambi badala ya kuba twatipokya elimu ya ukweli, Dhabihu yenge ya sambi yasalia kwaa kae.
Kama tukifanya makusudi kuendelea kutenda dhambi baada ya kuwa tumepokea elimu ya ukweli, Dhabihu nyingine ya dhambi haisalii tena.
27 Badala yake, twabile ni tarajio kichake lya hukumu ya kutisha, ni ukale wa mwoto wabile utibateketeza maadui ga Mungu.
Badala yake, kuna tarajio pekee la hukumu ya kutisha, na ukali wa moto ambao utawateketeza maadui wa Mungu.
28 Yeyoti ywabile aakanikiye saliya ya Musa kabawaa bila rehema ya ushuhuda wa mashahidi abele au atatu.
Yeyote ambaye ameikataa sheria ya Musa hufa bila rehema mbele ya ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu.
29 Kiwango gani cha azabu muno ywakiwasa chalowa nstahili kila yumo ywatikumdharau mwana wa Nnongo, yeyoti ywaupangite mwai wa liagano kati kilebe chabile kitakatifu kwaa, mwai wabile wabekilwe wakfu ni Nnongo-yeyoti ywabile atikuntukana Roho ba neema.
kiwango gani zaidi cha adhabu unafikiri kinamstahiri kilammoja ambaye amemdharau mwana wa Mungu, yeyote aliyeitendea damu ya agano kama kitu kisicho kitakatifu, damu ambayo kwayo aliiweka wakfu kwa Mungu - yeyote ambaye amemtukana Roho wa neema?
30 Kwa mana twatanga yumo ywabile ayemi, “Kisasi ni chango, nalowa lepa.”Nga kae, Ngwana alowa kwahukumu bandu bake.”
Kwakuwa tunajua mmoja ambaye aliyesema, “Kisasi ni changu, nitalipa”. Na tena, “Bwana atawahukumu watu wake”.
31 Ni likowe lya kuogopa mundu kutomboka mu'maboko ga Nnongo ywabile nkoti!
Ni jambo la kuogofya mtu kuangukia katika mikono ya Mungu aliye hai!
32 Lakini kombokya masoba gapitike, baada ya kubekwa nuru kwinu, ni namna ya namani mwawezile kuvumilia makowe gaminya muno.
Lakini kumbuka siku zilizopita, baada ya kutiwa kwenu nuru, ni jinsi gani mliweza kuvumilia maumivu makali.
33 Mwabile m'bekilwe wazi mu'dhihaka ni matukangano ni mateso, ni mwabile ashiriki pamope ni balo bapetya mumateso kati ago.
Mlikuwa mmewekwa wazi katika dhihaka ya matukano na mateso, na mlikuwa washiriki pamoja na wale waliopitia mateso kama hayo.
34 Kwa mana mwabile ni mwoyoba huruma kwa abo babile afungwa, nga mwamupoki kwa puraha adhabu ya urithi winu mwatangite mwenga mwabene mwabile ni urithi unoite ni wa kudumu milele.
Kwa kuwa mlikuwa na moyo wa huruma kwa hao waliokuwa wafungwa, na mlipokea kwa furaha adhabu ya urithi wenu, mkijua kwamba ninyi wenyewe mlikuwa na urithi bora na wa kudumu milele.
35 Kwa eyo kana muuleke ujasiri winu, wabile ni zawadi ngolo.
Kwa hiyo msiutupe ujasiri wenu, ulio na zawadi kuu.
36 Kwa mana mwahitaji uvumilivu, ili kwamba mpale kupokya chelo Nnongo atikwaahidi, badala ya kupangilwa kuyatenda mapenzi gake.
Kwa kuwa mnahitaji uvumilivu, ili kwamba mpate kupokea ambacho Mungu amekiahidi, baada ya kuwa mmekwisha yatenda mapenzi yake.
37 Kwa mana baada ya muda nchene, yumo ywatiicha, alowa icha hakika ni alowa kawia kwaa.
Kwa kuwa baada ya kitambo kidogo, mmoja anayekuja, atakuja hakika na hatakawia.
38 Ywa bile ni haki wango alowa tama kwa imani. Kati ywaboi kunchogo, nalowa pendezwa kwaa ni ywembe.
Mwenye haki wangu ataishi kwa imani. Kama atarudi nyuma, sitapendezwa naye.”
39 Lakini twenga twabile kwaa kati balo bakerebukye kunchogo kwa angamya. Badala yake, twenga twabaadhi ya balo twabile ni imani ya kuilinda roho yitu.
Lakini sisi si kama wale warudio nyuma kwa kuangamia. Badala yake, sisi ni baadhi ya wale tulio na imani ya kuzilinda roho zetu.

< Baebrania 10 >