< Matendo ga Mitume 9 >

1 Lakini Sauli, kayendelea longela vitishi hata kwa kiwo cha banapunzi ba Ngwana, atiyenda kwa kuhani nkolo
Lakini Sauli, aliendelea kusema vitisho hata vya kifo kwa wanafunzi wa Bwana, alikwenda kwa kuhani mkuu
2 na kunnaba barua kwa ajili ya Masinagogi kolyo Dameski, ili panga mana ampatike mundu ywabile katika ndela yelo, awe nnalome au nnwawa, abatabe na kubaleta Yerusalem.
na kumwomba barua kwa ajili ya masinagogi huko Dameski, ili kwamba akimpata mtu aliye katika Njia ile, awe mwanaume au mwanamke, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.
3 Paabile katika safari, ipangite kuwa paakaribie Dameski, gafla utimwangazia kotekote bweya boka kumaunde,'
Hata alipokuwa akisafiri, ilitokea kwamba alipokaribia Dameski, ghafla ikamwangaza kotekote nuru kutoka mbinguni,'
4 ni ywembe atomboka pae na ayowine lilobe lambakiye, “Sauli, Sauli, mbona wanitesa nenga?”
naye akaanguka chini na akasikia sauti ikimwambia,”Sauli, Sauli, mbona wanitesa mimi?”
5 Sauli kayangwa, Wenga wa nyai Ngwana? Ngwana kabaya, “Nenga ni Yesu waniudhi.
Sauli akajibu, U nani wewe Bwana? Bwana akasema, “Mimi ndiye Yesu unayeniudhi;
6 Lakini inuka, jingya mjini, wenga walowa bakilwa ya upalikwa kuyapanga.
Lakini inuka, ingia mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda
7 Balo bandu batisafiiri pamope na Sauli batami kimya, kabayowa lilobe ila bamweni kwaa mundu.
Wale watu waliosafiri pamoja na Sauli wakatulia kimya, wakisikiliza sauti, wasione mtu.
8 Sauli atiinuka katika nnema na paayongoli minyo gake, aweza kwaa bona kilebe, kabankamwa luboko bannetike Dameski.
Sauli akainuka katika nchi na alipofungua macho yake, hakuweza kuona kitu, wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski.
9 Kwa masoba atatu abweni kwaa, alya kwaa wala anywa kwaa.
Kwa siku tatu haoni, hali, wala hanywi.
10 Abile mwanapunzi Dameski lina lyake Anania, Ngwana alongela nae katika maono, “Anania.” No baya, “Linga, nibile pano, Ngwana.
Basi palikuwapo mwanafunzi Dameski jina lake Anania, Bwana alisema naye katika maono, “Anania.” Na akasema, “Tazama, nipo hapa, Bwana.
11 “Ngwana kammakiya, Inuka uyende zako katika mtaa waukemelwa Nyofu, na katika nyumba ya Yuda na ukannaluye mundu boka Tarso ywakemelwa Sauli; mana angali aloba:
“Bwana akamwambia, “Inuka uenda zako katika mtaa uitwao Nyofu, na katika nyumba ya Yuda na ukaulize mtu kutoka Tarso aitwaye Sauli; maana angali anaomba;
12 Na amweni katika maono mundu lina lyake Anania kajingya na kumbekya maboko nnani yake ila panga aweze kubona.
na alimwona katika maono mtu jina lake Anania akiingia na kumwekea mikono juu yake ili kwamba apate kuona.
13 Lakini Anania kanyangwa, “Ngwana, niyowine habari za mundu yoo kwa bandu banyansima, kwa kiasi gani abatendea mabaya batakatifu na kolyo Yerusalemu;
Lakini Anania akajibu, “Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, kwa kiasi gani alivyowatendea mabaya watakatifu wa huko Yerusalemu;
14 Pano abile na mamlaka boka kwa kuhani nkolo kuntaba kila yumo ywalikema lina lyako.
Hapa ana mamlaka kutoka kwa kuhani mkuu kumkamata kila mmoja anayeliitia jina lako.
15 Lakini Ngwana kammakiya, “Uyende, mana ywembe ni chombo kiteule sango, alitole lina lyango nnongi ya Mataifa na apwalume na bana ba Israeli.
Lakini Bwana akamwambia, “Nenda, kwa maana yeye ni chombo teule kwangu, alichukue jina langu mbele ya Mataifa na wafalme na wana wa Israeli.
16 Maana nalowa kuwabonekeya yabile ganyansima yaapalikwa kuteswa kwa ajili ya lina lyango.”
Maana nitawaonesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya jina langu”.
17 Anania kayenda, ajingii mu'nyumba; Kambekeya maboko kabaya, ndugu Sauli, Ngwana Yesu, ywakutokya katika ndela paubile waisa, anitumile upate kubona kae na utolilwe na Roho Mtakatifu.
Anania akaenda, akaingia mle nyumbani; Akamwekea mikono akasema, Ndugu Sauli, Bwana Yesu, aliyekutokea katika njia ulipokuwa unakuja, amenituma upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu.
18 Gafla vyatomboka ilebe kati magamba, apatike kubona, ayemi, akabatizwa; kalyaa chakulya na kupata ngupu,
Ghafla vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa; akala chakula na kupata nguvu.
19 Atami pamope na banapunzi bake kolyo Dameski kwa masoba ganyansima.
Akakaa pamoja na wanafunzi huko Dameski kwa siku nyingi.
20 Muda wowolo kantangaza Yesu katika masinagogi, kabaya panga ywembe ni Ngwana wa Nnongo.
Wakati huo huo akamtangaza Yesu katika masinagogi, akisema kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.
21 Na bote bayowine batishangala no baya, “Abile mundu yolo kwaa ywaatibaharibu bote balikemile lina lee kolyo Yerusalemu? Na pano kaisa kwa kusudi lya kuwafunga na kuwapeleka kwa makuhani,”
Na wote waliosikia walishangaa na kusema, “Siyo mtu huyu aliyewaharibu wote walioita Jina hili huko Yerusalemu? Na hapa alikuja kwa kusudi la kuwafunga na kuwapeleka kwa makuhani.”
22 Lakini Sauli atiwezeshwa hubiri na kubapanga Bayahudi batami Dameski basanganyikilwe na kuthibitisha ya kuwa ayoo nga Kristo.
Lakini Sauli aliwezeshwa kuhubiri na kuwafanya Wayahudi waliokaa Dameski wachanganyikiwe na kuthibitisha ya kuwa huyu ndiye Kristo.
23 Baada ya masoba ganansima, Bayahudi bapanga shauri pamope ili wamulage.
Baada ya siku nyingi, Wayahudi wakafanya shauri pamoja ili wamuue.
24 Lakini mpango wabe utiyowanika na Sauli. Kabamvizia pannango mutwekati na kilo bapate kumulaga.
Lakini mpango wao ukajulikana na Sauli. Wakamvizia mlangoni mchana na usiku wapate kumuua.
25 Lakini banapunzi bake kabantola kilo na kunshusha pitya ukutani, kabanneta pae mu'kitondo.
Lakini wanafunzi wake wakamchukua usiku wakamshusha kupitia ukutani, wakamtelemsha chini katika kapu.
26 Na sauli paaikite Yerusalemu, atijaribu kujiunga na banapunzi lakini babile bakimwogopa, basadiki kwaa kuwa ywembe ni mwanapunzi.
Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi lakini walikuwa wakimuogopa, wasisadiki kuwa yeye ni mwanafunzi.
27 Lakini Barnaba kantola na kumpeleka kwa mitume, na aabakiye jinsi Sauli yaamweni Ngwana mu'ndela na Ngwana yaa alongela nakwe, na jinsi Sauli atihubiri kwa ujasiri kwa lina lya Yesu kolyo Dameski.
Lakini Barnaba akamchukua na kumpeleka kwa mitume, Na akawaeleza jinsi Sauli alivyomuona Bwana njiani na Bwana alivyosema nae, na jinsi Sauli alivyohubiri kwa ujasiri kwa jina la Yesu huko Dameski.
28 Atikwembana nabembe kabajingya na boka Yerusalemu, abaya kwa ujasiri kwa lina lya Ngwana Yesu.
Alikutana nao walipoingia na kutoka Yerusalemu. Akanena kwa ujasiri kwa jina la Bwana Yesu,
29 Kabalongela na Ayahudi wa Kiyunani lakini batijaribu mara kwa mara kumulaga.
akihojiana na Wayahudi wa Kiyunani lakini wakijaribu mara kwa mara kumuua.
30 Muda palitangite likowe lee, kabantola mpaka Kaisaria, na batimpeleka ayende Tarso.
Wakati ndugu walipojua jambo hilo, wakamchukua mpaka Kaisaria, na wampeleke aende Tarso.
31 Bai likanisa lyote katika Uyahudi, Galilaya na Samaria, libile na amani, lichengwite, na tyanga katika hofu ya Ngwana na faraja ya Roho Mtakatifu, likanisa latikuwa na yongekeya idadi ya bandu.
Basi kanisa lote katika Uyahudi, Galilaya na Samaria, lilikuwa na amani, na likajengwa, na kutembea katika hofu ya Bwana na faraja ya Roho Mtakatifu, kanisa likakua kwa kuongezeka idadi.
32 Boka po itokii Petro paabile kazunguka zunguka pande zote za mkoa, akabateremkia baumini batama katika mji wa Lida.
Kisha ilitokea Petro alipokuwa akizungukazunguka pande zote za mkoa, akawateremkia waumini waishio katika mji wa Lida.
33 Amweni kolyo mundu yumo lina lyake Ainea, mundu yolo abile pakindanda myaka nane; mana abile atipooza.
Akamuona huko mtu mmoja jina lake Ainea, mtu huyo amekuwa kitandani miaka minane; maana alikuwa amepooza.
34 Petro kammakiya, “Ainea, Yesu Kristo akuponye; amka ni uyitandikiye kindanda sako.” mara atiamka.
Petro akamwambia, “Ainea, Yesu Kristo akuponye; Amka na ujitandikia kitanda chako,” Mara akaamka.
35 Na bandu bote batami Lida na Sharoni pabamweni mundu yolo, batimkerebukya Ngwana.
Na watu wote waliokaa Lida na Sharoni walipomuona mtu huyo, walimgeukia Bwana.
36 Pabile na mwanapunzi Yafa akemelwa Tabitha, ambalo mana yake “Dorcas” Ayoo nnwawa atwelilwe kazi inoite na matendo ga rehema aipangite kwa maskini.
Palikuwa na mwanafunzi Yafa aitwaye Tabitha, ambalo lilitafsiriwa kama “Dorcas” Huyu mwanamke alijaa kazi njema na matendo ya rehema aliyoyafanya kwa maskini.
37 Yatipangika katika masoba ago abile ntamwe na awile, pabamsafisha, no kumpandisha chumba cha kunani na kumgonjekea.
Ilitokea katika siku hizo aliugua na akafa; walipomsafisha, walimpandisha chumba cha juu na kumlaza.
38 Kwa namna Lida abile papipi na Yafa, banapunzi bayowine panga Petro abile kolyo, batibatuma bandu abele kwake, kabamsihi, “Uise kwitu bila kuchelewa.”
Kwa vile Lida ilikuwa karibu na Yafa, na wanafunzi walisikia kwamba Petro alikuwa huko, waliwatuma watu wawili kwake, wakimsihi, “Njoo kwetu bila kuchelewa”.
39 Petro atiamka na kaboka pamope nabembe. Paaikite, bannetike katika chumba cha kunani. Na ajane bote bayemi papipi niywembe niywembe kabalela, bakinlolekeya koti na ngobo ambazo Dorcas atibashonea muda abile pamope nabo.
Petro akaamka na akaondoka pamoja nao. Alipofika, walimleta katika chumba cha juu. Na wajane wote walisimama karibu naye wakilia, wakimwonyesha koti na nguo ambazo Dorcas aliwashonea wakati akiwa pamoja nao.
40 Petro kabatoa bote panja ya nyumba, kapiga magoti na kuloba, boka po, atiukerebukya yega, “Tabitha, amka.” Ayongoli minyo gake na paamweni Petro atami pae.
Petro akawatoa wote nje ya chumba, akapiga magoti akaomba, kisha akaugekia mwili, akasema, “Tabitha, amka”. Akafungua macho yake na alipomwona Petro akakaa chini.
41 Boka po ampeya luboko lwake na kumwinua, na paabakema baamini na bajane, atibakabidhi kwabe abile nkoto.
Kisha Petro akampa mkono wake akamwinua, na alipowaita waamini na wajane, akawakabidhi kwao akiwa hai
42 Likowe lee liyowanike Yafa yote, na bandu banyansima bamwaminiya Ngwana.
Jambo hili likajulikana Yafa yote, na watu wengi wakamwamini Bwana.
43 Ipangite Petro atama masoba ganyansima Yafa pamope na mundu ywakemelwa Simoni, ywatengeneza ngozi.
Ilitokea Petro akakaa siku nyingi Yafa pamoja na mtu aitwaye Simoni, mtengeneza ngozi.

< Matendo ga Mitume 9 >