< Matendo ga Mitume 10 >

1 Pabile na mundu pulani katika mji wa Kaisaria, lina lyake akemelwa Kornelio, abile nkolo wa kikosi sa Baitalia.
Kulikuwa na mtu fulani katika mji wa kaisaria, jina lake aliitwa Kornelio, alikuwa mkuu wa kikosi cha Kiitalia.
2 Abile ancha Nnongo na atimwabudu Nnongo na nyumba yake yoti; atitoa mbanje yanansima kwa Ayahudi na aloba kwa Nnongo masoba gote.
Alikuwa mchamungu na alimwabudu Mungu na nyumba yake yote; alitoa pesa nyingi kwa wayahudi na aliomba kwa Mungu siku zote.
3 Muda wa saa tisa ya mutwekati, abweni maono malaika wa Nnongo kambakiya, “Kornelio!
Muda wa saa tisa za mchana, akaona maono Malaika wa Mungu anakuja kwake. Malaika akamwambia “Kornelio!
4 Kornelio kamlolekeya malaika na abile na hofu ngolo muno kabaya “Ayee nga namani nkolo?” Malaika kammakiya Maombi ni sadaka yako kwa maskini zimepanda nnani kati kumbukumbu mu'uwepo wa Nnongo.”
Kornelio akamwangalia malaika na alikuwa na hofu kubwa sana akasema “Hii ni nini mkuu?” Malaika akamwambia “Maombi yako na zawadi zako kwa masikini zimepanda juu kama kumbukumbu kwenye uwepo wa Mungu”.
5 Nambeambe ubatume bandu yendya mji wa Yafa kunneta mundu yumo ywakemelwa Simoni ywabile ukemelwa Petro.
Sasa tuma watu kwenda mji wa Yafa kumleta mtu mmoja anayeitwa Simoni ambaye pia huitwa Petro.
6 Atama na nchenga ngozi ywakemelwa Simoni ambaye nyumba yake ibile kando ya bahari.”
Anakaa na mtengenezaji wa Ngozi aitwaye Simoni ambaye nyumba yake iko kando ya bahari.”
7 Baada ya malaika ywabaya ni ywembe kuboka, Kornelio abakema batumishi ba mu'nyumba yaker abele, na askari ywatimwabudu Nnongo kati ya askari babile bamtumikya.
Baada ya Malaika aliyekuwa akisema naye kuondoka, Kornelio akawaita watumishi wa nyumbani kwake wawili, na askari aliyekuwa akimwabudu Mungu kati ya maaskari waliokuwa wanamtumikia.
8 Kornelio kaabakiya gote yapangike na kabatuma Yafa.
Kornelio aliwaambia yote yaliyotokea na akawatuma Yafa.
9 Lisoba lya nyaibele saa sita babile mundela na babile papipi na mji, Petro kapanda nnani mu'dari loba.
Siku iliyofuata muda wa saa sita wakiwa njiani na wamekaribia mjini, Petro akapanda juu darini kuomba.
10 Na abile na njala na apala kilebe cha kulya, lakini muda bandu bateleka chakulya, kabonekeya maono,
Na pia akawa na njaa na alihitaji kitu cha kula, lakini wakati watu wanapika chakula, akaonyeshwa maono,
11 Abweni anga liyongoliwe na chombo chatiuluka na kilebe fulani kati ngobo kolo yatiuluka pae pa'nnema katika kona zote ncheche.
akaona anga limefuguka na chombo kinashuka na kitu fulani kama nguo kubwa ikishuka chini kwenye ardhi katika kona zake zote nne.
12 Nkati yake pabile na aina yoti ya anyama babile na magolo ncheche na batambaa nnani ya nnema, na iyuni ba angani.
Ndani yake kulikuwa na aina zote za wanyama wenye miguu minne na watambaao juu ya ardhi, na ndege wa angani.
13 Lilobe lyabaya kwake, “amka, Petro chinja na ulyee.”
Tena sauti ikasema kwake “Amka, Petro chinja na ule”.
14 Lakini Petro kabaya “nga nyoo kwaa, Ngwana kwa sababu nalowa lyaa kwaa kilebe chochte kinajisi na kichapu.
Lakini Petro akasema “Siyo hivyo, Bwana kwa sababu sijawahi kula kitu chochote najisi na kichafu.
15 Lakini lilobe lyaisa kwake kae kwa mara yana ibele “Chaakitakasa Nnongo kana ukikeme najisi wala kichafu.”
Lakini sauti ikaja kwake tena kwa mara ya pili “Alichokitakasa Mungu usikiite najisi wala kichafu”.
16 Ayee ipangika mara tatu, na chelo chombo chatitolwa kae angani.
Hii ilitokea mara tatu, na kile chombo kikawa kimechukuliwa tena angani.
17 Palyo petro abile katika hali ya changanyikiwa nnani ya ago maono yatimaanisha namani, Linga bandu batumilwe na Kornelio bayemi nnongi ya
Na wakati Petro akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa juu ya hayo maono yanamaanisha nini, Tazama, watu waliokuwa wametumwa na Kornelio wakasimama mbele ya lango, wakiuliza njia ya kwenda kwenye nyumba.
18 nnango, kannaluya ndela ya kuyenda mu'nyumba. Bakema na kunnaluya mana Simoni ywakemelwa Petro atama palo.
Na wakaita na kuuliza kama Simoni ambaye pia aliitwa Petro kama alikuwa anakaa pale.
19 Muda woo Petro abile awasa nnani ya ago maono, Roho kabaya na ywembe, “Linga bandu atatu bakupala.
Wakati huo Petro alipokuwa akiwaza juu ya hayo maono, Roho akasema naye, “Tazama watu watatu wanakutafuta.
20 Amka na uuluke pae na uyende nakwe. Uyogope kwaa yenda nabembe, kwa mana niatumile.”
Amka na ushuke chini na uende nao. Usiogope kwenda nao, kwa sababu nimewatuma.”
21 Petro atiuluka pae kwao na baya “Nenga nga yolo mwamumpala. kwa mwanja namani muisile?”
Petro akashuka chini kwao na kusema “Mimi ni yule mnayemtafuta. Kwa nini mmekuja?”
22 Babaya, “Akida yumo lina lyake Kornelio, mundu wa haki na hupenda kumwabudu Nnongo, na bandu ubaya vema katika litaifa lyote lya Ayahudi, abakilwe na malaika ba Nnongo kututuma twenga ili kuyenda mu'nyumba yake, ili ayowe ujumbe boka kwako.”
Wakasema, “Akida mmoja jina lake Kornelio, mtu wa haki na hupenda kumwabudu Mungu, na watu humsema vyema katika taifa lote la kiyahudi, ameambiwa na malaika wa Mungu kukutuma ili kwenda kwenye nyumba yake, ili asikie ujumbe kutoka kwako.”
23 Petro kabakaribisha jingya mu'nyumba na tama pamope nakwe. Bwamba ya lisoba lyanaibele atiyumuka kayenda pamope nakwe, na alongo achache boka Yafa batikengamana naywembe.
Petro akawakaribisha kuingia ndani na kukaa pamoja naye. Asubuhi iliyofuata akaamka akaenda pamoja naye, na ndugu wachache kutoka Yafa wakaambatana naye.
24 Baikite Kaisalia lisoba lyanaibele. Na Kornelio abile atibalenda abakema pamope alongo bake na mbwiga bake ba karibu.
Siku iliyofuata walikuja Kaisaria. Na Kornelio alikuwa akiwasubiri; na alikuwa amewaita pamoja ndugu zake na marafiki zake wa karibu.
25 Petro pajingii mu'nyumba, Kornelio atikumlaki na kuinama mpaka pae mu'magolo gake kwa kumweshimu.
Wakati Petro akiingia ndani, Kornelio akamlaki na kuinama hadi chini kwenye miguu yake kwa kumheshimu.
26 Lakini Petro kamwinua no baya “Yema; nenga namwene na mundu kae.”
Lakini Petro akamwinua na kusema “Simama; mimi mwenyewe pia ni mwanadamu.”
27 Palyo Petro atilongela naywembe, atiyenda mu'nyumba kaakuta bandu batikusanyika pamope.
Wakati Petro akiwa anaongea naye, alienda ndani akakuta watu wamekusanyika pamoja.
28 Kaamakiya, “Mwenga mwabene mutangite panga ibile kwaa saliya ya kiyahudi shirikiana na tembeleana na mundu ywabile kwaa wa taifa lee. Lakini Nnongo kanibonekeya nenga kuwa nipalika kwaa kumwita mundu yeyote najisi au mchafu.
Akawaambia, “Ninyi wenyewe mnajua kuwa siyo sheria ya kiyahudi kushirikiana au kutembelewa na mtu ambaye si wa taifa hili. Lakini Mungu amenionesha mimi kuwa sipaswi kumwita mtu yeyote ni najisi au mchafu.
29 Nga nyoo niisile bila kubisha, panitumilwe kwa ajili yelo. Kwa eyo naanaluya kwa mwanja namani mwatumilwe kwa ajili yango?”
Na ndiyo maana nimekuja bila kubisha, nilipotumwa kwa ajili ya hiyo. Kwa hiyo niwaulize kwa nini mlitumwa kwa ajili yangu.”
30 Kornelio kabaya, “Masoba ncheche ganchogo bka leno, muda kati wolo nibile naloba muda wa saa tisa mutwekati mu'nyumba yango: Nibweni nnongi yango mundu ayemi abile na ngobo nyuepe,
Kornelio akasema, “Siku nne zilizopita, wakati kama huu nilikuwa naomba muda wa saa tisa mchana ndani ya nyumba yangu; Nikaona mbele yangu mtu amesimama akiwa na mavazi meupe,
31 Kanibakiya “Kornelio maombi gako gatiyowanika na Nnongo, na sadaka zako kwa maskini zibile kati ukumbusho nnongi ya Nnongo.
Akaniambia “Kornelio maombi yako yamesikiwa na Mungu, na zawadi zako kwa masikini zimekuwa ukumbusho mbele za Mungu.
32 Kwa eyo batume bandu Yafa na bankeme mundu yumo ywakemelwa Simoni aise kwako, ambaye ukemwa Petro, ambaye atama kwa ywachenga ngozi yumo ywakemelwa Simon ambae nyumba yake ibile pembeni ya libahari.
Kwa hiyo tuma mtu Yafa na akamwite mtu mmoja anayeitwa Simoni aje kwako, ambaye pia huitwa Petro. ambaye anaishi kwa mtengenezaji wa Ngozi mmoja aitwaye Simoni ambaye nyumba yake iko pembeni mwa bahari.
33 Zingatia mtari wolo, “Ni ywembe paaisa alowa baya nimwenga” ubile kwaa mu'maandiko ga kale.
Zingatia: Msatri huu, “Naya atakapokuja atasema nanyi,” haumo kwenye maandiko ya kale.
34 Petro ayongoli nkano wake no baya, “Kweli, naaminiya kuwa Nnongo aweza kwaa kuwa na upendeleo.
Ndipo Petro akafungua mdomo wake na kusema “Kweli, nimeamini kuwa Mungu hawezi kuwa na upendeleo.
35 Badala yake, kila taifa mundu yeyote ywamwabudia na kupanga matendo ga haki anakubalika kwake.
Badala yake, kila taifa mtu yeyote anayemwabudu na kufanya matendo ya haki anakubalika kwake.
36 Uutangite ujumbe ulioutoa kwa bandu ba Israeli. abile akitangaza habari njema ya amani pitya Yesu Kristo ywabile ni Ngwana wa bote.
Unajua ujumbe alioutoa kwa watu wa Israel, alipokuwa akitangaza habari njema ya amani kupitia Yesu Kristo ambaye ni Bwana wa wote-
37 mwenga mwabene mutangite tukio lyalipangite, ambalo lipangite Yudea yote na litumbwile Galilaya, baada ya ubatizo ambao Yohana atiutangaza.
ninyi wenyewe mnajua tukio lililotokea, ambalo limetokea Yudea yote na lilianzia Galilaya, baada ya ubatizo ambao Yohana alitangaza.
38 likowe lyalibile linamuhusu Yesu Kristo jinsi Nnongo atimtia mauta kwa Roho Mtakatifu na kwa nguvu. Apangite mema na kuponya bote bateswile na ibilisi, kwa mana Nnongo abile pamope naywembe.
tukio lililokuwa linamhusu Yesu Kristo jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na kwa nguvu. Alienda akifanya mema na kuponya wote walioteswa na ibilsi, kwa kuwa Mungu alikuwa pamoja naye.
39 Twenga ni mashaidi ba makowe yote yaapangite katika nchi ya Uyahudi na katika Yerusalemu-ayoo ni Yesu ywamulaga na kuntundika mu'nkongo.
Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyoyafanya katika nchi za Uyahudi na katika Yerusalemu- huyu ni Yesu waliyemuua na kumtundika mtini.
40 Ayoo mundu Nnongo atikumfufua lisoba lya tatu na kumpeya kuyowanika.
Huyu mtu Mungu alimfufua siku ya tatu na kumpa kujulikana,
41 Kwa bandu bote kwaa, lakini twenga twabene, twalya naywembe na nywaa niywembe baada ya kufufuka boka mu kiwo.
si kwa watu wote, lakini kwa mashahidi waliochaguliwa kabla na Mungu. - sisi wenyewe, tulio kula naye na kunywa naye baada ya kufufuka kutoka kwa wafu.
42 Atituagiza kuhubiri kwa bandu na kushuhudia kuwa ayoo nga Nnongo ywamchawile kuwa mwamuzi wa babile akoto na babile mu'kiwo.
Ametuagiza kuhubiri kwa watu na kushuhudia kuwa huyu ndiye ambaye Mungu alimchagua kuwa mwamuzi wa walio hai na waliokufa.
43 Katika ywembe manabii bote bashuhudie, ili panga kila ywaaminiye katika ywembe alowa pokya msamaha wa sambi pitya lina lyake.
Katika yeye manabii wote washuhudie, ili kwamba kila anayeamini katika yeye atapokea msamaha wa dhambi kupitia jina lake.”
44 Palyo Petro kayendelya longela nyoo, Roho Mtakatifu kaatweliya bote babile bauyowine ujumbe wake.
Wakati Petro akiendelea kusema haya, Roho Mtakatifu akawajaza wote waliokuwa wakisikiliza ujumbe wake.
45 Bandu balo bahusika na likundi lya baaminiya babile atahiriwa-balo bote baisile na Petro-batishangala, kwa sababu ya karama ya Roho Mtakatifu ywatimwagwa kwa mataifa.
Watu wale wanaohusika na kikundi cha waamini waliotahiriwa- wale wote waliokuja na Petro- walishangazwa, kwa sababu ya karama ya Roho Mtakatifu aliyemwagwa pia kwa wamataifa.
46 Kwa kuwa bayowine aba bamataifa balongela kwa lugha yenge na kumwabudu Nnongo. Petro kayangwa,
Kwa kuwa walisikia hawa wamataifa wanaongea kwa lugha zingine na kumwabudu Mungu. Petro akajibu,
47 “Abile mundu yoyote ywaweza kuzuia maji ili bandu babatizwe kwaa. Bandu aba batimpokya Roho Mtakatifu kati twenga?”
“Kuna mtu yeyote anaweza kuzuia maji ili watu wasibatizwe, Watu hawa wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi?”
48 Nga kabaamuru babatize kwa lina lya Yesu Kristo. Baadaye banobite atame nabo kwa masoba kadhaa.
Ndipo akawaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Baadaye wakamwomba akae nao kwa siku kadhaa.

< Matendo ga Mitume 10 >