< Matendo ga Mitume 28 >

1 Patuikite salama, tutangite panga kisiwa kikemelwa Malta.
Tulipofikishwa salama, tulitambua kwamba kisiwa kinaitwa Malta.
2 Bandu batama poo ni balo patupeya ukarimu wa kawaida wa kwaa, ila baliwasha mwoto na kutukaribisha twabote, kwa sababu ya ula na mbepo yaibile itiendelea.
Watu wenyeji wa pale si tu kwamba walitupa ukarimu wa kawaida, bali waliwasha moto na kutukaribisha sote, kwa sababu ya mvua na baridi iliyokuwa ikiendelea.
3 Lakini Paulo paabile atikusanya mzigo wa anju na kuubeka pamwoto, nng'ambo nchunu ywabile na sumu aboka mu'yelo anju kwa sababu ya lelo lijoto, na akajizungusha mu'maboko gake.
Lakini Paulo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni na kuuweka motoni, nyoka mdogo mwenye sumu akatoka kwenye zile kuni kwa sababu ya lile joto, na akajizungusha kwenye mkono wake.
4 Bandu wenyeji wa palo pabamweni yolo mnyama atining'ia boka mu'maboko gake, babaya bene kwa bene, “Mundu yolo hakika ni muuaji ambaye aboka mulibahari, lakini haki haimuruhusu tama.”
Watu wenyeji wa pale walipoona mnyama ananing'inia kutoka kwenye mkono wake, wakasemezana wao kwa wao, “Mtu huyu hakika ni muuaji ambaye ametoroka baharini, lakini haki haimuruhusu kuishi.”
5 Lakini ywembe atintupia yolo mnyama katika mwoto na apata kwaa madhara yoyote.
Lakini yeye akamtupia huyo mnyama katika moto na hakupata madhara yoyote.
6 Bembe batimgojea avimbe kwa homa au atomboke gafla na kubulagika. Lakini baada ya kunlolekeya kwa muda mrefu na kubona panga ntopo likowe ambalo ni lakwaida kwaa kwake, balibadilisha malango yabe no baya abile nongo.
Wao walimngojea avimbe kwa homa au aanguke ghafla na kufa. Lakini baada ya kumwangalia kwa muda mrefu na kuona kwamba hakuna jambo ambalo si la kawaida kwake, walibadilisha mawazo yao na kusema alikuwa mungu.
7 Bai mahali palo papipi pabile na bui ambayo ubile mali ya nkolo wa kisiwa, mundu ywakemelwa Pablio. Atitukaribisha na kutukarimu kwa masoba atatu.
Basi mahali pale karibu palikuwa na ardhi ambayo ilikuwa mali ya mkuu wa kisiwa, mtu aliyeitwa Pablio. Alitukaribisha na kutukarimu kwa siku tatu.
8 ipalike panga tate ba Pablio abile na homa na ugonjwa wa kuhara. Na Paulo pmwendea, akiloba, kabeka maboko nnani yake, na kumponya.
Ilitokea kwamba baba wa Pablio alishikwa na homa na ugonjwa wa kuhara. Na Paulo alipomwendea, aliomba, akaweka mikono juu yake, na kumponya.
9 Baada ya lee pangika, bandu benge palo pakisiwa baabile atamwe batiyenda na kuponelwa.
Baada ya hili kutokea, watu wengine pale kisiwani waliokuwa wanaumwa pia walikwenda na waliponywa.
10 Bandu batimuheshimu kwa heshima yanyansima. Tubile twatijiandaa kusafiri, batupeya yelo twahitajia.
Watu wakatuheshimu kwa heshima nyingi. Tulipokuwa tunajiandaa kusafiri, walitupa vile tulivyovihitaji.
11 Baada ya miei itatu, twatisafiri nkati ya meli ya iskanda ambayo ibile imepigwa mbepo kolyo pakisiwa, ambayo viongozi wake babile alongo abele mapacha.
Baada ya miezi mitatu, tulisafiri ndani ya meli ya Iskanda ambayo ilikuwa imepigwa baridi hapo kisiwani, ambayo viongozi wake walikuwa ndugu wawili mapacha.
12 Baada ya kuwa twatua katika mji wa Sirakusa, twatama kolyo masoba atatu.
Baada ya kuwa tumetua katika mji wa Sirakusa, tulikaa pale siku tatu.
13 Iapangike palo twatisafiri katika mji wa Regio. Baada ya lisoba limo mbepo wa kusini uboite ghafla, na baada ya masoba abele tuikite katika mji wa Putoli.
Kutokea pale tulisafiri tukafika katika mji wa Regio. Baada ya siku moja upepo wa kusini ulitokea ghafla, na baada ya siku mbili tukafika katika mji wa Putoli.
14 Kolyo twatikwembana baadhi ya alongo na twatikaribishwa na tama nao kwa masoba saba. Kwa ndela yee tuisile Rumi.
Huko tuliwakuta baadhi ya ndugu na tulikaribishwa kukaa nao kwa siku saba. Kwa njia hii tukaja Rumi.
15 Boka kolyo balo alongo, baada ya kuwa wayowine habari zetu, baisile kutupokya kolyo kulisoko lya Apias na Hotel tatu. Paulo paabweni balo alongo atimshukuru Nnongo kajipea ujasiri.
Kutoka huko wale ndugu, baada ya kuwa wamesikia habari zetu, walikuja kutupokea huko soko la Apias na Hotel tatu. Paulo alipowaona wale ndugu alimshukuru Mungu akajitia ujasiri.
16 Patujingii Roma, Paulo atiruhusiwa tama kichake pamope na yolo askari ywabile akinlinda.
Tulipoingia Roma, Paulo aliruhusiwa kuishi peke yake pamoja na yule askari aliyekuwa akimlinda.
17 Bai ibile baada ya masoba atatu Paulo atibakema pamope balo alalome babile viongozi kati ya Ayahudi. Pabaisile pamope, abaya kwao, “Alongo, pamope na panga nipangite kosa lolote kwa bandu aba au panga kinchogo na taratibu za apindo bitu batuyongolya, natitolewa kati mfungwa boka Yerusalemu mpaka katika maboko ga Arumi.
Basi ilikuwa baada ya siku tatu Paulo aliwaita pamoja wale wanume waliokuwa viongozi kati ya Wayahudi. Walipokuja pamoja, alisema kwao, “Ndugu, pamoja na kwamba sijafanya kosa lolote kwa watu hawa au kufanya kinyume na taratibu za mababa zetu waliotutangulia, nilitolewa kama mfungwa kutoka Yerusalemu hadi kwenye mikono ya Warumi.
18 Baada ya kunnaluya, batamaniya kunileka huru, kwa sababu kwabile ntopo sababu kwango nenga yastahili adhabu ya kiwo.
Baada ya kunihoji, walitamani kuniacha huru, kwa sababu kulikuwa hakuna sababu kwangu mimi ya kustahili adhabu ya kifo.
19 Lakini balo Ayahudi pabalongela kinyume cha shauku yabe, nililazimika kukata rufaa kwa Kaisaria, ila ibile kwaa kati panga naleta mashitaka nnani ya litaifa lyango.
Lakini wale Wayahudi walipoongea kinyume cha shauku yao, nililazimika kukata rufaa kwa Kaisaria, japokuwa haikuwa kana kwamba naleta mashtaka juu ya taifa langu.
20 Kwa sababu ya kukata kwango rufaa, nga nyo, niloba kubabona na longela namwenga. Kwa sababu ya chelo ambacho Israeli abile na ujasiri nacho, nitabilwe na kifungo chee.
Kwa sababu ya kukata kwangu rufaa, hivyo, niliomba kuwaona na kuongea nanyi. Ni kwa sababu ya kile ambacho Israel anaujasiri kwacho, nimefungwa na kifungo hiki.
21 Boka po bammakiya, “Twapokya kwaa barua boka Yudea kuhusu wenga, wala ntopo nongo ywaisa na kutoa taarifa au baya neno lolote linoite kwaa nnani ya wenga.
Kisha wakamwambia, “Hatujawahi kupokea barua kutoka Yudea kukuhusu wewe, wala hakuna ndugu aliyekuja na kutoa taarifa au kusema neno lolote baya kuhusu wewe.
22 Lakini twapala kuyowa boka kwako wawaza namani kuhusu lee likundi lya bandu aba, kwa sababu iyowanike kwetu panga lalongela kinyume kila mahali.”
Lakini tunataka kusikia kutoka kwako unafikiri nini kuhusu hili kundi la watu hawa, kwa sababu inajulikana kwetu kwamba linaongea kinyume kila mahali.”
23 Pababile batitenga lisoba kwa ajili yake, bandu banyansima baisa mahali paabile atama. Kabaya lelo likowe kwao na kushuhudia kuhusu ufalme wa Nnongo. Atijaribu kubashawishi kuhusu Yesu, kwa namna zote ibele boka katika saliya ya Musa na boka kwa manabii, toka bwamba mpaka kitamwinyo.
Walipokuwa wametenga siku kwa ajili yake, watu wengi zaidi walimwijia mahali alipokuwa anaishi. Alisema lile jambo kwao na kushuhudia kuhusu ufalme wa Mungu. Alijaribu kuwashawishi kuhusu Yesu, kwa namna zote mbili kutoka katika sheria za Musa na kutoka kwa manabii, kuanzia asubuhi hadi jioni.
24 Baadhi ya bembe batishawishika kuhusu makowe yalo yabayilwe, na benge baaminiya kwaa.
Baadhi yao walishawishika kuhusu mambo yale yaliyosemwa, wakati wengine hawakuamini.
25 Pabatishindwa yeketyana bene kwa bene, batiboka baada ya Paulo kulibaya likowe lee limo, “Roho Mtakatifu abaya vyema pitya Isaya nabii kwa tate bitu,
Waliposhindwa kukubaliana wao kwa wao, waliondoka baada ya Paulo kulisema jambo hili moja, “Roho Mtakatifu alisema vyema kupitia Isaya nabii kwa baba zenu.
26 Abaya,'Yenda kwa bandu aba ubaye, “Kwa makutu yinu mwalowa sikia, lakini mupekania kwaa; na kwa minyo yinu mwalowa lola lakini mutangite kwaa.
Alisema, 'Nenda kwa watu hawa useme, “Kwa masikio yenu mtasikia, lakini hamtaelewa; Na kwa macho yenu mtaona lakini hamtatambua.
27 Kwaajili ya mioyo ya bandu aba ibile dhaifu, makutu gabe gapekanie kwa taabu, watifunga minyo yabe; ili panga kana patange kwa minyo yabe, na kupekania kwa makutu gabe, na kutanga kwa mioyo yabe, na kerebuka kae, na nalowa kubaponya.”
Kwa ajili ya mioyo ya watu hawa imekuwa dhaifu, masikio yao yamesikia kwa taabu, wamefumba macho yao; ili kwamba wasijekutambua kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kuelewa kwa mioyo yao, na kugeuka tena, na ningeliwaponya.”'
28 Kwa eyo mpalikwa kutanga panga awoo wokovu wa Nnongo utipelekwa kwa bandu ba Mataifa, na balowa kuwapekania.”
Kwa hiyo, mnapaswa kujua kwamba huu wokovu wa Mungu umepelekwa kwa watu wa Mataifa, na watasikiliza.” (Zingatia: Mstari huu
“Wakati alipokuwa amesema mambo haya, wayahudi waliondoka, wakiwa na mashindano makubwa kati yao.,” haumo kwenye nakala bora za kale).
30 Pulo atami mu'nyumba yake ya kupanga kwa miaka yote ibele, na atibakaribisha bote baisile kwake.
Paulo alikaa katika nyumba yake ya kupanga kwa miaka yote miwili, na aliwakaribisha wote waliokuja kwake.
31 Abile akihubiri ufalme wa Nnongo na abile akifundisha makowe nnani ya Ngwana Yesu Kristo kwa ujasiri wote. Ntopo ywankanikiya.
Alikuwa akihubiri ufalme wa Mungu na alikuwa akifundisha mambo juu ya Bwana Yesu Kristo kwa ujasiri wote. Hakuna aliyemzuia.

< Matendo ga Mitume 28 >