< Matendo ga Mitume 21 >

1 Muda tubile twatilekana nabo, na twatisafiri mubahari, tuiikite moja kwa moja pa'mji wa Kosi, na malabo yake tuikite mji wa Rodo, na boka kolyo tuikite mji wa Ptara.
Wakati tulipokua tumeachana nao, na tunasafiri baharini, tukafika moja kwa moja kwenye mji wa Kosi, na kesho yake tukafika mji wa Rodo, na kutoka huko tukafika mji wa Patara.
2 Tupatike meli yayoka kuyenda Foinike, twatisafiri na meli yoo.
Tulipopata meli inayovuka kwenda Foinike, tulipanda tukasafiri.
3 Patuikite nnongi ya kisiwa cha Kipro, tuilekite upande wa mashoto, tuikite mpaka Siria, twaitosa nanga katika mji wa Tiro, kwa mana kolyo nga meli yatipakulilwa lishehena lyake.
Tulipofika mbele ya kisiwa cha Kipro, tukaiacha upande wa kushoto, tukasafiri hadi Siria, tukaweka nanga katika mji wa Tiro, kwa sababu huko ndiko meli ilikuwa ipakuliwe shehena yake.
4 Baada ya kuabona banafunzi, twatama masoba saba. Banafunzi aba bammakiya Paulo pitya kwa Roho panga ywembe kana ayende Yerusalemu.
Baada ya kuwaona wanafunzi, tukakaa huko siku saba. Wanafunzi hawa wakamwambia Paulo kupitia kwa Roho kwamba yeye asikanyage Yerusalemu.
5 Hata patuitimize masoba ago, twenga twatiboka kuyenda zetu. Bote pamope, na alwawa babe na bana babe, batitusindikiza katika ndela yitu mpaka patuboi panja ya mji. Boka po twatipiga magoti pwani, na kuloba, twatiagana kila yumo.
Hata tulipotimiza siku zile, sisi tukaondoka tukaenda zetu. Wote pamoja, na wanawake zao na watoto wao, walitusindikiza katika njia zetu hadi tulipotoka nje ya mji. Kisha tukapiga magoti pwani, tukaomba, tukaagana kila mmoja.
6 Twapanda mu'meli, na bembe batikerebuka kae munyumba yabe.
Tukapanda meli, huku nao wakarudi nyumbani kwao tena.
7 Patuyomwile safari yitu boka Tiro, tuikite Tolemai. Palo tuasimamii alongo, na tama nabo kwa lisoba limo.
Hata tulipomaliza safari yetu kutoka Tiro, tukafika Tolemai. Pale tulisalimia ndugu, na kukakaa nao kwa siku moja.
8 Malabo yake tubokite kuyenda Kaisaria. Twenga tujingii munyumba ya Filipo, muhubiri wa injili, ywabile yumo wa balo saba, ni twenga tutami pamope naye.
Kesho yake tuliondoka tukaenda Kaisaria. Sisi tukaingia nyumbani mwa Filipo, mhubiri wa injili, aliyekuwa mmoja wa wale saba, nasi tukakaa pamoja naye.
9 Mundu yolo abile na alombo ncheche makikra ambao baritabiri.
Mtu huyu alikuwa na mabinti wanne mabikira ambao walitabiri.
10 Baada ya tama kwa masoba kadhaa, atiuluka boka Uyahudi nabii yumo ywa kemelwa Agabo.
Baada ya kukaa huko kwa siku kadhaa, akashuka kutoka Uyahudi nabii mmoja aitwaye Agabo.
11 Ywembe atiisa kwitu na atiutola mkanda wa Paulo. kwa huo atiyataba magolo na maboko gake mwene nobaya, “Roho Mtakatifu abaya nyoo,” “Bayahudi ba Yerusalemu balowa kuntaba mundu ywamilikiya mkando wolo, nibembe balowa kunkabidhi mumaboko ga bandu ba mataifa.”
Yeye alikuja kwetu na akautwaa mkanda wa Paulo. kwa huo alijifunga miguu na mikono yake mwenyewe na kusema, “Roho Mtakatifu asema hivi,” “Wayahudi wa Yerusalemu watamfunga mtu anayemiliki mkanda huu, nao watamkabidhi mikononi mwa watu wa mataifa.”
12 Patuyowine makowe aga, twenga na bandu babile atama mahali palo twatimsihi Paulo kana ayende Yerusalemu.
Tuliposikia mambo hayo, sisi na watu waliokuwa wakiishi mahali pale tulimsihi Paulo asipande kwende Yerusalemu.
13 Nga Paulo kayangwa, “Mupanga kele, mwalela na kunivunja mwoyo wango? Kwa mana nibile tayari, kufungwa kwaa kae, lakini pia bulagwa kolyo Yerusalemu kwa ajili ya lina lya Ngwana Yesu.”
Ndipo Paulo alijibu, “Mnafanya nini, mnalia na kunivunja moyo wangu? Kwa maana niko tayari, siyo tu kufungwa, lakini pia kufia huko Yerusalemu kwa ajili ya jina la Bwana Yesu.”
14 Kwa mana Paulo apala kwaa kushawishiwa, tulekite no baya, “Bai mapenzi ya Ngwana yapangike.”
Kwa vile Paulo hakutaka kushawishiwa, tuliacha na kusema, “Basi mapenzi ya Bwana yafanyike.”
15 Baada ya masoba aga, tutolile mifuko yitu na kupanda kuyenda Yerusalemu.
Baada ya siku hizi, tulichukua mifuko yetu na tukapanda Yerusalemu.
16 Baadhi ya banafunzi boka Kaisaria pia batikengamana na twenga. Batinneta mundu yumo ywakemelwa Mnasoni, mundu wa Kipro, mwanafunzi wa zamani, ambaye tutami naye.
Baadhi ya wanafunzi kutoka Kaisaria pia walifuatana nasi. Wakamleta mtu mmoja aitwaye Mnasoni, mtu wa Kipro, mwanafunzi wa zamani, ambaye tulikaa naye.
17 Patuikite Yerusalemu, alongo balitukaribisha kwa puraha.
Tulipofika Yerusalemu, ndugu walitukaribisha kwa furaha.
18 Malabo yake Paulo atiyenda pamope na twenga kwa Yakobo, na apindo bote babile poo.
Kesho yake Paulo alienda pamoja nasi kwa Yakobo, na wazee wote walikuwepo.
19 Baada ya kuwasalimu, alibapeya taarifa yimo baada ya yenge ya makowe ambayo Nnongo apangite nkati ya mataifa kwopitya huduma yake.
Baada ya kuwasalimu, aliwapa taarifa moja baada ya nyingine ya mambo ambayo Mungu aliyotenda miongoni mwa mataifa kwa kupitia huduma yake.
20 Muda bayowine ago, batimsifu Nnongo, na kummakiya, “Ubweni, alongo, kubile na maelfu ilenga baaminiya nkati ya Ayahudi. Bembe bote babile na nia ya kuikamwa saliya.
Wakati waliposikia hayo, wakamsifu Mungu, na wakamwambia, “Unaona, ndugu, kuna maelfu wangapi wameamini miongoni mwa Wayahudi. Wao wote wana nia ya kushika sheria.
21 Babakilwe kuhusu wenga, panga wafundisha Ayahudi batama kati ya mataifa kunleka Musa, na panga uwabakiye kana baatahiri bana babe, na kana baipange desturi ya zamani.
Wameambiwa kuhusu wewe, kwamba unafundisha Wayahudi wanaoishi kati ya mataifa kuachana na Musa, na kwamba unawaambia wasiwatahiri watoto wao, na wasifuate desturi za zamani.
22 Tupalikwa panga namani? Bila shaka balowa yowa kuwa weka uisile.
Tunapaswa tufanye nini? Bila shaka watasikia kwamba wewe umekuja.
23 Nga nyo upange chelo ambacho twenga twakubakiya nambeambe: tubile na bandu ncheche ambao batiweka nadhiri.
Hivyo fanya kile sisi tunachokuambia sasa: tunao watu wanne ambao wameweka nadhiri.
24 Watole bandu aba na ujitakase mwene pamope nabembe, na uwalipiye gharama yabo, ili waweze kunyoa ntwe wabe. Nga nyoo kila yumo apate kuyowa panga makowe gaamakiwe kuhusu wenga ni ubocho. Balowa kujifunza panga wenga kae uikengama saliya.
Wachukue watu hawa na ujitakase mwenyewe pamoja nao, na uwalipie gharama zao, ili waweze kunyoa vichwa vyao. Hivyo kila mmoja apate kujua kwamba mambo waliyoambiwa kuhusu wewe ni ya uongo. Watajifunza kwamba wewe pia unafuata sheria.
25 Lakini kwa habari ya mataifa ambao babile baumini, twaandikiye na kutoa maagizo panga bapalikwa kujiepusha na ilebe vyatitolewa dhabihu kwa sanamu, na myai, bokana na chelo chakinyongwa, na bajiepushe na umalaya.”
Lakini kwa habari za mataifa ambao wamekuwa waumini, tuliandika na kutoa maagizo kwamba wanapaswa kujiepusha na vitu vilivyotolewa dhabihu kwa sanamu, na damu, kutokana na kile kilichonyongwa, na wajiepushe na uasherati.”
26 Nga nyo, Paulo atibatola analome na lisoba lya nyaibele, atijitakasa mwene pamope nabembe, na kujingya mu'hekalu, kutangaza kipindi cha masoba ya kujitakasa, mpaka sadaka yatolewa kwa ajili ya kila yumo wao.
Ndipo, Paulo aliwatwaa wanaume, na siku ya pili, akajitakasa mwenyewe pamoja nao, akaingia Hekaluni, kutangaza kipindi cha siku za kujitakasa, hadi sadaka itolewa kwa ajili ya kila mmoja wao.
27 Masoba ago saba payakaribie yomoka, baadhi ya Bayahudi boka Asia bamweni Paulo mu'lihekalu, na makutano batikasirika, na kunnyoshea maboko.
Siku hizo saba zilipokaribia kumalizika, baadhi ya Wayahudi kutoka Asia wakamuona Paulo Hekaluni, na makutano wakakasirika, na wakamnyoshea mikono.
28 Babile bakikombwa ndoti, “Bandu ba Israeli, mutusaidie. Ayoo nga yolo mundu ywafundisha bandu kila mahali makowe ambayo ni kunchogo na bandu, saliya, na mahali pano. Pia atibaleta Ayunani katika lihekalu na kupanajisi mahali pano patakatifu.”
Walikuwa wanapiga kelele, “Watu wa Israeli, tusaidieni. Huyu ni yule mtu anayewafundisha watu kila mahali mambo ambayo ni kinyume na watu, sheria, na mahali hapa. Pia amewaleta Wayunani katika Hekalu na kupanajisi mahali hapa patakatifu.”
29 Kwa mana mwanzo babile bamweni Trofimo Muefeso abile pamope niywembe mjini, na bembe patangite panga Paulo annetike mulihekalu.
Kwa kuwa mwanzoni walikuwa wamemwona Trofimo Muefeso akiwa pamoja naye mjini, nao walidhani kwamba Paulo alimleta hekaluni.
30 Mji wote ubile na taharuki, na bandu babutuka pamope ni kunkamwa Paulo. Patintoa panja ya lihekalu, na nnango mara itabilwe.
Mji wote ulikuwa na taharuki, na watu wakakimbia pamoja na kumkamata Paulo. Wakamtoa nje ya Hekalu, na milango mara ikafungwa.
31 Pababile bakijaribu kummulaga, habari iikite kwa nkolo wa jeshi lya alinzi kuwa Yerusalemu yote ibile itwelilwe ghasia.
Walipokuwa wakijaribu kumuua, habari zilimfikia mkuu wa jeshi la walinzi kuwa Yerusalemu yote ilikuwa imejaa ghasia.
32 Mara iyo atibatola askari na jemedari atikibutukia kipenga sa bandu. Muda bandu bamweni nkolo ba jeshi na askari atimkaribia na kunkamwa Paulo.
Mara hiyo akawachukua askari na jemadari akaukimbilia umati. Wakati Watu walipomwona mkuu wa jeshi na askari, wakaacha kumpiga Paulo.
33 Boka po nkolo wa jeshi atiamuru atabwe minyororo ibele. Kannaluya wenga wa nyai na upangite kele.
Kisha mkuu wa jeshi alimkaribia na akamshika Paulo, na akaamuru afungwe minyororo miwili. Akamuuliza yeye ni nani na amefanya nini.
34 Baadhi ya bandu katika kipenga babile batipayuka kilebe cheno benge chelo. Kwa mana jemedari aweza kwaa kuwamakiya chochote kwa sababu ya yelo ndoti, atiamuri Paulo aletwe mkati ya ngome.
Baadhi ya watu kwenye umati walikuwa wanapayuka kitu hiki na wengine kingine. Kwa kuwa jemadari hakuweza kuwaambia chochote kwa sababu ya zile kelele, akaamuru Paulo aletwe ndani ya ngome.
35 Bai paakite mu'ngazi, atitolewa na askari kwa sababu za kipenga sa bandu.
Basi alipofika kwenye ngazi, akachukuliwa na askari kwa sababu ya ghasia za umati.
36 Maana kipenga sa bandu batikengamana na yendelea kukombwa ndoti, “muntole yolo!”
Maana umati wa watu walimfuata na waliendelea kupiga kelele, “Mwondoeni huyu!”
37 Paulo paabile atiletwa nkati ya ngome, atimmakiya nkolo wa jeshi, “Naweza kukumakiya kilebe?” Yolo nkolo wa jeshi kabaya, “Je walongela kiyunani?
Paulo alipokuwa analetwa ndani ya ngome, alimwambia mkuu wa jeshi, “Naweza kukwambia kitu?” Yule mkuu wa jeshi akasema, “Je unaongea Kiyunani?
38 Je wenga wa Mmisri ambaye awali utiongoza uasi na kubatola magaidi elfu ncheche mmwitu?”
Je, wewe si yule Mmisri ambaye awali aliongoza uasi na alichukua magaidi elfu nne nyikani?”
39 Paulo kabaya, “Nenga na Myahudi, boka mji wa Tarso ya Kilikia. Nenga ni raia wa mji maarufu. Naaloba, mniruhusu nilongele na bandu.”
Paulo akasema, “Mimi ni Myahudi, kutoka mji wa Tarso ya Kilikia. Mimi ni raia wa mji maarufu. Nawaomba, mniruhusu nizungumze na watu.”
40 Muda jemedari ampeya ruhusa, Paulo ayemi pa'ngazi na kutoa ishara kwa bandu kwa luboko lwake. Muda woo pabile na ukimya muno, akalongela nabo kwa Kiebrania. kabaya.
Wakati jemadari alipompa ruhusa, Paulo akasimama penye ngazi na akatoa ishara kwa watu kwa mkono wake. Wakati kulipokuwa na ukimya sana, akaongea nao kwa Kihebrania. Akasema,

< Matendo ga Mitume 21 >