< 2 Akoritho 6 >

1 Na kwa eyo, upanga kazi pamope, twendabasihi mwenga kana muipokee neema ya Nnongo pabile kwaa ni matokeo.
Na kwa hiyo, kufanya kazi pamoja, tunawasihi ninyi msiipokee neema ya Mungu pasipo matokeo.
2 Kwa kuwa abaya, “Wakati waukubalika nibile makini kwinu, na katika lisoba lya wokovu niliwasaidia.”Linga nambeambe ni wakati waukubaluka. Linga, nambeambe ni lisoba lya wokovu.
Kwa kuwa anasema, “Wakati uliokubalika nilikuwa makini kwenu, na katika siku ya wokovu niliwasaidia.” Tazama, sasa ni wakati uliokubalika. Tazama, sasa ni siku ya wokovu.
3 Twaweka kwaa liwe lya kizuizi nnonge ya mundu yoyote, kwa mana tuitakia kwaa huduma yitu iletwe katika sifa mbaya.
Hatuweki jiwe la kizuizi mbele ya mtu yeyote, kwa kuwa hatuitakii huduma yetu iletwe katika sifa mbaya.
4 Badala yake, twaihakiki bene kwa makowe yitu yote, panga tu atumishi ga Nnongo. Tubile atumishi bake katika baingi ba ustahimilivu, mateso, dhiki, ugumu wa maisha,
Badala yake, tunajihakiki wenyewe kwa matendo yetu yote, kwamba tu watumishi wa Mungu. Tu watumishi wake katika wingi wa ustahimilivu, mateso, dhiki, ugumu wa maisha,
5 kukombwa, vifungo, ghasia, katika panga kazi kwa bidii, katika kukosa lugono kilo, katika njala,
kupigwa, vifungo, ghasia, katika kufanya kazi kwa bidii, katika kukosa usingizi usiku, katika njaa,
6 katika usafi, maarifa, uvumilivu, wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo halisi
katika usafi, maarifa, uvumilivu, wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo halisi.
7 Tubile abatumishi bake katika eneo lya kweli, katika ngupu ya Nnongo. Tubile ni silaha ya haki kwa ajili ya luboko lwa mmalyo na wa kushoto.
Tu watumishi wake katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu. Tuna silaha ya haki kwa ajili ya mkono wa kuuume na wa kushoto.
8 Twapanga kazi katika hekima na dharauliwa, katika kashfa na sifa. Twatituhumiwa kuwa abocho na wakati tubile wakweli.
Tunafanya kazi katika heshima na kudharauliwa, katika kashfa na sifa. Tunatuhumiwa kuwa wadanganyifu na wakati tu wakweli.
9 Tunapanga kazi napanga twajulikana kwaa na bado twayowanika vizuri. Twapanga kazi kati batiwaa na -Linga!-bado twatama. Twaipanga kazi kati twaazibiwa kwa ajili ya matendo yitu lakini kati kwaa yaabahukumilwe hata waa,
Tunafanya kazi kana kwamba hatujulikani na bado tunajulikana vizuri. Tunafanya kazi kama wanaokufa na -Tazama! - bado tunaishi. Tunafanya kazi kama tunaoadhibiwa kwa ajili ya matendo yetu lakini sio kama waliohukumiwa hata kufa.
10 Twaipanga kazi kati wenye masikitiko, lakini masoba gote twabile na furaha. Twaipanga kazi kati maskini, lakini twajihatarisha baingi. Twaipanga kazi kati panga twapata kwaa kilebe kati twatemiliki kila kilebe.
Tunafanya kazi kama wenye masikitiko, lakini siku zote tuna furaha. Tunafanya kazi kama maskini, lakini tunatajirisha wengi. Tunafanya kazi kana kwamba hatupati kitu bali kama tunaomiliki kila kitu.
11 Twabaya ukweli wote kwinu, Akorintho, na mioyo yitu yatifunguka kwa upana.
Tumezungumza ukweli wote kwenu, Wakorintho, na mioyo yetu imefunguka kwa upana.
12 Mioyo yinu izuiliwa kwaa na twenga, ila mwatizuiliwa na hisia yinu wene.
mioyo yenu haizuiliwi na sisi, bali mnazuiliwa na hisia zenu wenyewe.
13 Nambeambe katika badilishana kwa haki nalongela kati kwa bana-muipungue mioyo yinu kwa upana.
Sasa katika kubadilishana kwa haki - ninaongea kama kwa watoto - fungueni mioyo yenu kwa upana.
14 Kana mupungamanishe pamope ni baaminiya kwaa. Kwa mana kwabile ni uhusiano gani kati ya haki ni uasi? Ni kwabile ni ushirika gani kati ya bweya ya libendo?
Msifungamanishwe pamoja na wasioamini. Kwa kuwa kuna uhusiano gani kati ya haki na uasi? Na kuna ushirika gani kati ya nuru na giza?
15 Ni makubaliano gani Kristo aweza kuwa nayo na Beliari? Au ywembe ywaamiye abile sehemu gani pamope ni ywaaminiya kwaa?
Ni makubaliano gani Kristo anaweza kuwa nayo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na asiyeamini?
16 Na kwabile na kakubaliano gani yabile kati ya hekalu lya Nnongo na lisanamu? Kwa mana twanga ni lihekale lya Nnongo ywabile nkoto, kati ambavyo Nnongo abayite: “Nalowa tama kati yabembe ni ktyanga kati ya bembe. Nalowa pangika Nnongo wa bembe, na bembe bapangika kuwa bandu bango.”
Na kuna makubaliano gani yapo kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi ni hekalu la Mungu aliye hai, kama ambavyo Mungu alisema: “Nitakaa kati yao na kutembea kati yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”
17 Kwa eyo, “Muboke kati yabembe, mkatengwe nabo,” abaya Ngwana.”Kana mukamwe kilebe kichafu na nalowa kubakaribisha mwenga.
Kwa hiyo, “Tokeni kati yao, na mkatengwe nao,” asema Bwana. “Msiguse kitu kichafu, na nitawakaribisha ninyi.
18 Nalowa pangika kuwa Tate kwinu, ni mwenga mwalowa pangika bana bango analome na anwawa, “abaya Ngwana Mwenyezi.
Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa wanangu wa kiume na wa kike,” asema Bwana Mwenyezi.

< 2 Akoritho 6 >