< Psalmorum 146 >

1 Alleluia, Aggæi, et Zachariæ.
Msifu Yahwe. Msifu Yahwe, ee nafsi yangu.
2 Lauda anima mea Dominum, laudabo Dominum in vita mea: psallam Deo meo quamdiu fuero. Nolite confidere in principibus:
Ninamsifu Mungu maisha yangu yote; nitamuimbia sifa Mungu wangu ni ngali ni hai.
3 in filiis hominum, in quibus non est salus.
Msiweke imani katika wakuu au wanadamu, ambaye katika yeye hamna wokovu.
4 Exibit spiritus eius, et revertetur in terram suam: in illa die peribunt omnes cogitationes eorum.
Wakati uhai wa pumzi ya mtu unapokoma, hurudi aridhini; siku hiyo mipango yake hufikia mwisho.
5 Beatus, cuius Deus Iacob adiutor eius, spes eius in Domino Deo ipsius:
Amebarikiwa yule ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, ambaye tumaini lake liko katika Yahwe Mungu wake.
6 qui fecit cælum et terram, mare, et omnia, quæ in eis sunt.
Yahwe aliumba mbingu na nchi, bahari, na vyote vilivyomo; huitazama kweli milele.
7 Qui custodit veritatem in sæculum, facit iudicium iniuriam patientibus: dat escam esurientibus. Dominus solvit compeditos:
Yeye hutekeleza hukumu kwa ajili ya walioonewa na huwapa chakula wenye njaa. Yahwe huwafungua waliofungwa;
8 Dominus illuminat cæcos. Dominus erigit elisos, Dominus diligit iustos.
Yahwe huyafungua macho ya kipofu; Yahwe huwainua walioinama; Yahwe huwapenda watu wenye haki.
9 Dominus custodit advenas, pupillum et viduam suscipiet: et vias peccatorum disperdet.
Yahwe huwalinda wageni katika nchi; huwainua yatima na wajane, bali huipinga njia ya wasio haki.
10 Regnabit Dominus in sæcula, Deus tuus Sion, in generationem et generationem.
Yahwe atatawala milele, Mungu wako, Sayuni, kwa vizazi vyote. Msifuni Yahwe.

< Psalmorum 146 >