< Colossenes 4 >

1 Domini, quod iustum est et æquum, servis præstate: scientes quod et vos Dominum habetis in cælo.
Mabwana, toeni kwa watumwa mambo yaliyo haki na ya adili. Mnajua pia kwamba mnaye Bwana mbinguni.
2 Orationi instate, vigilantes in ea in gratiarum actione:
Endeleeni kuwa thabiti katika maombi. Kaeni macho katika hilo kwa shukrani.
3 orantes simul et pro nobis, ut Deus aperiat nobis ostium sermonis ad loquendum mysterium Christi (propter quod etiam vinctus sum)
Ombeni pamoja kwa ajili yetu pia, ili kwamba Mungu afungue mlango kwa ajili ya neno, kunena siri ya ukweli ya Kristo. Kwa sababu ya hili nimefungwa minyororo.
4 ut manifestem illud ita ut oportet me loqui.
Na ombeni kwamba niweze kuliweka wazi, kama inavyonipasa kusema.
5 In sapientia ambulate ad eos, qui foris sunt: tempus redimentes.
Enenda kwa hekima kwa wale walioko nje, na muukomboe wakati.
6 Sermo vester semper in gratia sale sit conditus, ut sciatis quomodo oporteat vos unicuique respondere.
Maneno yenu na yawe na neema wakati wote, na yakolee chumvi majira yote, ili kwamba mweze kujua jinsi inavyowapasa kumjibu kila mtu.
7 Quæ circa me sunt, omnia vobis nota faciet Tychicus charissimus frater, et fidelis minister, et conservus in Domino:
Kwa mambo yanayonihusu mimi, Tikiko atayafanya yajulikane kwenu. Yeye ni ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, na mtumwa mwenzetu katika Bwana.
8 quem misi ad vos ad hoc ipsum ut cognoscat, quæ circa vos sunt, et consoletur corda vestra,
Namtuma kwenu kwa ajili ya hili, kwamba mweze kujua mambo kuhusu sisi na pia kwamba aweze kuwatia moyo.
9 cum Onesimo charissimo, et fideli fratre, qui ex vobis est. Omnia, quæ hic aguntur, nota facient vobis.
Namtuma pamoja na Onesimo, ndugu yetu mpendwa mwaminifu, na mmoja wenu. Watawaambia kila kitu kilichotokea hapa.
10 Salutat vos Aristarchus concaptivus meus, et Marcus consobrinus Barnabæ, de quo accepistis mandata: si venerit ad vos, excipite illum:
Aristarko, mfungwa mwenzangu, anawasalimu, pia na Marko binamu yake na Barnaba mliyepokea utaratibu kutoka kwake, “kama akija kwenu, mpokeeni,”
11 et Iesus, qui dicitur Iustus: qui sunt ex circumcisione: hi soli sunt adiutores mei in regno Dei, qui mihi fuerunt solatio.
Na pia Yesu aitwaye Yusto. Hawa peke yao wa tohara ni watendakazi wenzangu kwa jili ya ufalme wa Mungu. Wamekuwa ni faraja kwangu.
12 Salutat vos Epaphras, qui ex vobis est, servus Christi Iesu, semper solicitus pro vobis in orationibus, ut stetis perfecti, et pleni in omni voluntate Dei.
Epafra anawasalimu. Yeye ni mmoja wenu na mtumwa wa Kristo Yesu. Yeye hufanya bidii katika maombi kwa ajili, ili kwamba mweze kusimama kwa ukamilifu na kuhakishwa kikamilifu katika mapenzi yote ya Mungu.
13 Testimonium enim illi perhibeo quod habet multum laborem pro vobis, et pro iis, qui sunt Laodiciæ, et qui Hierapoli.
Kwa kuwa ninamshuhudia, kwamba anafanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, kwa hao walioko Laodekia, na kwa hao walioko Hierapoli.
14 Salutat vos Lucas medicus charissimus, et Demas.
Luka yule tabibu mpendwa, na Dema wanawasalimu.
15 Salutate fratres, qui sunt Laodiciæ, et Nympham, et quæ in domo eius est, ecclesiam.
Wasalimu ndugu zangu walioko Laodekia, na Nimfa, na kanisa lile lililoko nyumbani kwake.
16 Et cum lecta fuerit apud vos epistola hæc, facite ut et in Laodicensium Ecclesia legatur: et eam, quæ Laodicensium est, vos legatis.
Barua hii itakapokuwa imesomwa miongoni mwenu, isomwe pia kwa kanisa la walaodekia, nanyi pia hakikisheni mnaisoma ile barua kutoka Laodekia.
17 Et dicite Archippo: Vide ministerium, quod accepisti in Domino, ut illud impleas.
Sema kwa Arkipo, ''Angalia ile huduma ambayo umeipokea katika Bwana, kwamba unapaswa kuitimiza.”
18 Salutatio, mea manu Pauli. Memores estote vinculorum meorum. Gratia vobiscum. Amen.
Salamu hii ni kwa mkono wangu mwenyewe - Paulo. Ikuumbukeni minyororo yangu. Neema na iwe nanyi.

< Colossenes 4 >