< Thessalonicenses I 1 >

1 Paulus, et Silvanus, et Timotheus Ecclesiæ Thessalonicensium in Deo Patre, et Domino Iesu Christo.
Paulo, Silwano na Timotheo kwa kanisa la Wathesalonike katika Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo. Neema na amani iwe nanyi.
2 Gratia vobis, et pax. Gratias agimus Deo semper pro omnibus vobis, memoriam vestri facientes in orationibus nostris sine intermissione,
Tunatoa shukrani kwa Mungu kila mara kwa ajili yenu nyote, wakati tunapowataja katika maombi yetu.
3 memores operis fidei vestræ, et laboris, et charitatis, et sustinentiæ spei Domini nostri Iesu Christi, ante Deum et Patrem nostrum:
Tunaikumbuka bila kukoma mbele ya Mungu na baba yetu kazi yenu ya imani, juhudi ya upendo, na uvumilivu wenye ujasiri kwa ajili ya baadaye katika Bwana Yesu Kristo.
4 scientes fratres, dilecti a Deo, electionem vestram:
Ndugu Mnaopendwa na Mungu, tunajua wito wenu.
5 quia Evangelium nostrum non fuit ad vos in sermone tantum, sed et in virtute, et in Spiritu Sancto, et in plenitudine multa, sicut scitis quales fuerimus in vobis propter vos.
Na jinsi injili yetu ilivyokuja kwenu si kwa neno tu, bali pia katika nguvu, katika Roho Mtakatifu, na katika uhakika. Kwa namna hiyo, mnajua pia sisi tulikuwa watu wa namna gani miongoni mwenu kwa ajili yenu.
6 Et vos imitatores nostri facti estis, et Domini, excipientes Verbum in tribulatione multa, cum gaudio Spiritus Sancti:
Mlikuwa watu wa kutuiga sisi na Bwana, kama mlivyopokea neno katika taabu kwa furaha itokayo kwa Roho Mtakatifu.
7 ita ut facti sitis forma omnibus credentibus in Macedonia, et in Achaia.
Na matokeo yake, mkawa mfano kwa wote katika Makedonia na Akaiya ambao wanaamini.
8 A vobis enim diffamatus est sermo Domini, non solum in Macedonia, et in Achaia, sed et in omni loco fides vestra, quæ est ad Deum, profecta est, ita ut non sit nobis necesse quidquam loqui.
Kwa kuwa kutoka kwenu neno la Mungu limeenea kote, na si kwa Mekadonia na Akaiya peke yake. Badala yake, kwa kila mahali imani yenu katika Mungu imeenea kote. Na matokeo yake, hatuhitaji kusema chochote.
9 Ipsi enim de nobis annunciant qualem introitum habuerimus ad vos: et quomodo conversi estis ad Deum a simulacris, servire Deo vivo, et vero,
Kwa kuwa wao wenyewe wanaarifu ujio wetu ulikuwa wa namna gani kati yenu. Wanasimulia jinsi mulivyomgeukia Mungu kutoka katika sanamu na kumtumikia Mungu aliye hai na wa kweli.
10 et expectare Filium eius de cælis (quem suscitavit a mortuis) Iesum, qui eripuit nos ab ira ventura.
Walitoa habari kuwa mnamsubiri Mwana wake kutoka mbinguni, aliyefufuliwa kutoka kwa wafu. Na huyu ni Yesu, anayetuweka huru kutoka kwenye ghadhabu ijayo.

< Thessalonicenses I 1 >