< マタイの福音書 25 >

1 其時天國は、十人の處女面々燈を執りて新郎と新婦とを迎へに出たる如くならん。
Ndipo ufalme wa mbinguni utafananishwa na wanawali kumi waliochukua taa zao na kuondoka kwenda kumpokea bwana harusi.
2 其中五人は愚にして五人は賢し、
Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano wengine walikuwa werevu.
3 愚なる五人は燈を執りて油を携へざるに、
Wanawali wapumbavu walipochukua taa zao, hawakuchukua mafuta yoyote.
4 賢きは燈と共に油を器に携へたり。
Bali wanawali welevu walichukua vyombo vyenye mafuta pamoja na taa zao.
5 新郎遅かりければ、皆假寝して眠りたりしが、
Sasa wakati bwana harusi amechelewa kufika, wote walishikwa usingizi na wakalala.
6 夜中に「すわ新郎來たるぞ、出迎へよ」との聲ありしかば、
Lakini wakati wa usiku wa manane kulikuwa na yowe, 'Tazama, bwana harusi! Tokeni nje mkampokee.'
7 處女皆起きて其燈を整へたり。
Ndipo hao wanawali waliamka wote na kuwasha taa zao.
8 愚なるが賢きに云ひけるは、汝等の油を我等に分て、我等の燈滅ゆ、と。
Wale wapumbavu waliwaambia wale welevu, 'Mtupatie sehemu ya mafuta yenu kwa sababu taa zetu zinazimika.'
9 賢きが答へて云ひけるは、恐らくは我等と汝等とに足らじ、寧売者に往きて自の為に買へ、と。
Lakini wale welevu waliwajibu na kuwaambia, 'Kwa kuwa hayatatutosha sisi na ninyi, badala yake nendeni kwa wanaouza mjinunulie kiasi kwa ajili yenu.'
10 彼等が買はんとて往ける間に、新郎來りしかば、用意してありし者等は、彼と共に婚筵に入り、然て門は鎖されたり。
Wakati wameenda huko kununua, Bwana harusi alifika, na wote waliokuwa tayari walienda naye kwenye sherehe ya harusi, na mlango ulifungwa.
11 軈て他の處女等も來りて、主よ主よ、我等に開き給へ、と云ひ居れども、
Baadaye wale wanawali wengine pia walifika na kusema, 'Bwana, bwana, tufungulie.'
12 彼答へて、我誠に汝等に告ぐ、我は汝等を知らず、と云へり。
Lakini alijibu na kusema, 'Kweli nawaambia, Mimi siwajui.'
13 然れば警戒せよ、汝等は其日其時を知らざればなり
Kwa hiyo angalieni, kwa kuwa hamjui siku au saa.
14 [天國は]即或人遠く旅立たんとして、其僕等を召び、是に我所有を渡せるが如し。
Kwa kuwa ni sawa na mtu alipotaka kusafiri kwenda nchi nyingine. Aliwaita watumwa wake na kuwakabidhi utajiri wake.
15 一人には五タレント、一人に二タレント、一人には一タレントを、各其器量に應じて渡し、然て直に出立せしが、
Mmoja wao alimpatia talanta tano, mwingine alimpa mbili, na yule mwingine alimpa talanta moja. Kila mmoja alipokea kiasi kulingana na uwezo wake, na yule mtu alisafari kwenda zake.
16 五タレントを受けし者は、往きて之を以て取引して、外に五タレントを贏け、
Mapema yule aliyepokea talanta tano alienda kuziwekeza, na kuzalisha talanta zingine tano.
17 二タレントを受けし者も同じ様にして、外に二タレントを贏けしに、
Vilevile yule aliyepokea talanta mbili, alizalisha zingine mbili.
18 一タレントを受けし者は、往きて地を掘り主人の金を蔵し置けり。
Lakini mtumwa aliyepokea talanta moja, alienda zake, akachimba shimo ardhini, na kuificha fedha ya bwana wake.
19 久しうして後、此僕等の主人來りて彼等と計算せしが、
Na baada ya muda mrefu, bwana wa watumwa hao alirudi na kutengeneza mahesabu nao.
20 五タレントを受けし者近づきて、別に五タレントを差出して云ひけるは、主君よ、我に五タレントを渡し給ひしが、看よ別に又五タレントを贏けたり、と。
Yule mtumwa aliyepokea talanta tano alikuja na kuleta talanta zingine tano, akasema, 'Bwana, ulinipa talanta tano. Tazama, nimepata faida ya talanta zingine tano.'
21 主人云ひけるは、宜し、善にして忠なる僕よ、汝些少なる物に忠なりしにより、我汝に多くの物を宰らしめん、汝の主人の喜に入れよ、と。
Bwana wake alimwambia, 'Hongera, mtumwa mzuri na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vidogo. Nitakupa madaraka juu ya vitu vingi. Ingia katika furaha ya bwana wako.'
22 二タレントを受けし者も亦近づきて云ひけるは、主君よ、我に二タレントを渡し給ひしが、看よ別に又二タレントを贏けたり、と。
Mtumwa aliyepokea talanta mbili alikuja na kusema, 'Bwana, ulinipa talanta mbili. Tazama, nimepata faida ya talanta zingine mbili,'
23 主人云ひけるは、宜し善にして忠なる僕よ、汝些少なる物に忠なりしにより、我汝に多くの物を宰らしめん、汝の主人の喜に入れよ、と。
Bwana wake alimwambia, 'Hongera, mtumwa mzuri na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache. Nitakupa madaraka juu ya vitu vingi. Ingia katika furaha ya bwana wako.'
24 一タレントを受けし者も亦近づきて云ひけるは、主君よ、我汝の厳しき人にして、播かざる處より穫り、散らさざる處より聚むるを知り、
Baadaye mtumwa aliyepokea talanta moja alikuja na kusema, 'Bwana, najua kuwa wewe ni mtu mkali. Unachuma mahali ambapo hukupanda, na unavuna mahali ambapo hukusia.
25 懼れて、往きて汝のタレントを地に蔵し置けり、看よ汝己が物を有す、と。
Mimi niliogopa, nikaenda zangu na kuificha talanta yako katika udongo. Tazama, unayo hapa ile iliyo yako.'
26 主人答へて云ひけるは、惡くして懶惰なる僕よ、汝我播かざる處より穫り、散らさざる處より聚むるを知りたれば、
Lakini bwana wake alijibu na kusema, 'Wewe mtumwa mwovu na mzembe, ulijua kwamba ninachuma mahali ambapo sijapanda na kuvuna mahali ambapo sikusia.
27 我金を兩替屋に預くべかりき、然らば我來りて、我有を利子と共に受けしならん。
Kwahiyo ulipaswa kuwapa fedha yangu watu wa benki, na wakati wa kurudi kwangu ningeipokea ile yangu pamoja na faida.
28 然れば汝等。此者より其タレントを取りて、十タレントを有てる者に與へよ、
Kwa hiyo mnyang'anyeni hiyo talanta na mpeni yule mtumwa aliye na talanta kumi.
29 蓋総て有てる人は與へられて裕ならん、然れど有たぬ人は、其有てりと思はるる所までも奪はれん、
Kila mtu aliye nacho, ataongezewa zaidi-hata kwa kuzidishiwa sana. Lakini kwa yeyote asiye na kitu, hata alicho nacho atanyang'anywa.
30 無益なる僕を外の暗に投出せ、其處には痛哭と切歯と在らん、と。
Mtupeni nje gizani huyo mtumwa asiyefaa, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.'
31 人の子己が威光を以て諸の[天]使を從へて來らん時、其威光の座に坐せん。
Wakati Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake, na malaika wote pamoja naye, ndipo atakapokaa juu ya kiti chake cha utukufu.
32 斯て萬民を其前に集め、彼等を別つこと、恰牧者が羊と牡山羊とを別つが如く、
Mataifa yote yatakusanyika mbele zake, naye atawatenganisha watu, kama vile mchungaji anavyowatenganisha kondoo na mbuzi.
33 羊を右に、牡山羊を左に置かん。
Atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, bali mbuzi atawaweka mkono wa kushoto.
34 時に王は其右に居る者に云はん、來れ、我父に祝せられたる者よ、世界開闢より汝等の為に備へられたる國を得よ。
Kisha mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kulia, 'Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu.
35 其は我が飢ゑしに汝等は食せしめ、我が渇きしに汝等飲ましめ、我が旅人なりしに汝等宿らせ、
Kwa kuwa nilikuwa na njaa na mlinipa chakula; Nilikuwa mgeni na mlinikaribisha;
36 裸なりしに着せ、病みたりしに訪ひ、監獄に在りしに來りたればなり、と。
Nilikuwa uchi, na mlinivika nguo; Nilikuwa mgonjwa na mkanitunza; Nilikuwa kifungoni na mkaniijia.'
37 此時義人等彼に答へて云はん、主よ、我等何時飢ゑ給ふを見て主に食せしめ、渇き給ふを[見て]主に飲ましめ、
Ndipo wenye haki watamjibu na kumwambia, 'Bwana, lini tulikuona ukiwa na njaa, na kukulisha? Au una kiu na tukakupa maji?
38 何時旅人に在せるを見て主を宿らせ、又裸に在るを[見て]主に着せしぞ、と。
Na lini tulikuona ukiwa mgeni, na tukakukaribisha? Au ukiwa uchi na tukakuvisha nguo?
39 又何時病み給ひ或は監獄に居給ふを見て主に至りしぞ、と。
Na lini tulikuona ukiwa mgonjwa, au katika kifungo, na tukakujia?
40 王答へて彼等に云はん、我誠に汝等に告ぐ、汝等が我此最小き兄弟の一人に為したる所は、事毎に即我に為ししなり、と。
Na mfalme atawajibu na kuwaambia, 'Kweli nawaambia, mlichotenda hapa kwa mmoja wa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.'
41 斯て左に居る者にも亦云はん、詛はれたる者よ、我を離れて、惡魔と其使等との為に備へられたる永遠の火に[入れ]。 (aiōnios g166)
Ndipo atawaambia hao walio mkono wake wa kushoto, 'Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, nendeni katika moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya shetani na malaika zake, (aiōnios g166)
42 其は我が飢ゑしに汝等は食せしめず、我が渇きしに汝等飲ましめず、
kwa sababu nilikuwa na njaa lakini hamkunipa chakula; Nilikuwa na kiu lakini hamkunipa maji;
43 我が旅人なりしに汝等宿らせず、裸なりしに汝等着せず、病み又監獄に在りしに汝等訪はざりし故なり、と。
Nilikuwa mgeni lakini hamkunikaribisha; nikiwa uchi lakini hamkunipa mavazi; nikiwa mgonjwa na nikiwa kifungoni, lakini hamkunitunza.'
44 此時彼等も王に答へて云はん、主よ、我等何時主の飢ゑ、或は渇き、或は旅人たり、或は裸なり、或は病み、或は監獄に居給ふを見て主に事へざりしぞ、と。
Ndipo wao pia watamjibu na kusema, 'Bwana, lini tulikuona ukiwa na njaa, au una kiu, au u mgeni, au ukiwa uchi, au ukiwa mgonjwa, au ukiwa mfungwa, na hatukukuhudumia?
45 此時王彼等に答へて云はん、我誠に汝等に告ぐ、汝等が此最小き者の一人に為さざりし所は、事毎に即我に為さざりしなり、と。
Kisha atawajibu na kusema, 'Kweli nawaambia, kile ambacho hamkutenda kwa mmoja wa hawa wadogo, hamkunitendea mimi.'
46 斯て是等の人は永遠の刑罰に入り、義人は永遠の生命に入るべし、と。 (aiōnios g166)
Hawa watakwenda katika adhabu ya milele bali wenye haki katika uzima wa milele.” (aiōnios g166)

< マタイの福音書 25 >