< דברי הימים א 3 >

ואלה היו בני דויד אשר נולד לו בחברון הבכור אמנן לאחינעם היזרעאלית שני דניאל לאביגיל הכרמלית 1
Hawa ndio waliokuwa wana wa Daudi waliozaliwa huko Hebroni: Mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni ambaye mama yake aliitwa Ahinoamu wa Yezreeli; wa pili, Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili wa Karmeli;
השלשי לאבשלום בן מעכה בת תלמי מלך גשור הרביעי אדניה בן חגית 2
wa tatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa Maaka, binti Talmai mfalme wa Geshuri; wa nne, Adoniya, ambaye mama yake alikuwa Hagithi;
החמישי שפטיה לאביטל הששי יתרעם לעגלה אשתו 3
wa tano alikuwa Shefatia ambaye mama yake alikuwa Abitali; wa sita alikuwa Ithreamu, aliyezaliwa na mke wake Egla.
ששה נולד לו בחברון וימלך שם שבע שנים וששה חדשים ושלשים ושלוש שנה מלך בירושלם 4
Hawa sita walizaliwa huko Hebroni ambako Daudi alitawala kwa miaka saba na miezi sita. Daudi alitawala Yerusalemu kwa miaka thelathini na mitatu,
ואלה נולדו לו בירושלים שמעא ושובב ונתן ושלמה ארבעה לבת שוע בת עמיאל 5
nao hawa ndio watoto wa Daudi waliozaliwa huko Yerusalemu: mkewe Bathsheba, binti Amieli, alimzalia Shamua, Shobabu, Nathani na Solomoni.
ויבחר ואלישמע ואליפלט 6
Pia kulikuwa na wana wengine: Ibihari, Elishua, Elifeleti,
ונגה ונפג ויפיע 7
Noga, Nefegi, Yafia,
ואלישמע ואלידע ואליפלט תשעה 8
Elishama, Eliada na Elifeleti; wote walikuwa tisa.
כל בני דויד--מלבד בני פילגשים ותמר אחותם 9
Hawa wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wale wana waliozaliwa na masuria. Naye Tamari alikuwa dada yao.
ובן שלמה רחבעם אביה בנו אסא בנו יהושפט בנו 10
Mwana wa Solomoni alikuwa Rehoboamu, mwanawe huyo alikuwa Abiya, mwanawe huyo alikuwa Yehoshafati, mwanawe huyo alikuwa Asa,
יורם בנו אחזיהו בנו יואש בנו 11
mwanawe huyo alikuwa Yehoramu, mwanawe huyo alikuwa Ahazia, mwanawe huyo alikuwa Yoashi,
אמציהו בנו עזריה בנו יותם בנו 12
mwanawe huyo alikuwa Amazia, mwanawe huyo alikuwa Azaria, mwanawe huyo alikuwa Yothamu,
אחז בנו חזקיהו בנו מנשה בנו 13
mwanawe huyo alikuwa Ahazi, mwanawe huyo alikuwa Hezekia, mwanawe huyo alikuwa Manase,
אמון בנו יאשיהו בנו 14
mwanawe huyo alikuwa Amoni na mwanawe huyo alikuwa Yosia.
ובני יאשיהו--הבכור יוחנן השני יהויקים השלשי צדקיהו הרביעי שלום 15
Wana wa Yosia walikuwa: Yohanani mzaliwa wake wa kwanza, Yehoyakimu mwanawe wa pili, wa tatu Sedekia, wa nne Shalumu.
ובני יהויקים--יכניה בנו צדקיה בנו 16
Walioingia mahali pa Yehoyakimu kama wafalme ni: Yekonia mwanawe, na Sedekia.
ובני יכניה אסר שאלתיאל בנו 17
Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yekonia aliyekuwa mateka: Shealtieli mwanawe,
ומלכירם ופדיה ושנאצר יקמיה הושמע ונדביה 18
Malkiramu, Pedaya, Shenasari, Yekamia, Hoshama na Nedabia.
ובני פדיה זרבבל ושמעי ובן זרבבל משלם וחנניה ושלמית אחותם 19
Wana wa Pedaya walikuwa: Zerubabeli na Shimei. Wana wa Zerubabeli walikuwa: Meshulamu na Hanania. Shelomithi alikuwa dada yao.
וחשבה ואהל וברכיה וחסדיה יושב חסד--חמש 20
Pia walikuwepo wengine watano: Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia na Yushab-Hesedi.
ובן חנניה פלטיה וישעיה בני רפיה בני ארנן בני עבדיה בני שכניה 21
Wazao wa Hanania walikuwa: Pelatia na Yeshaya, na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.
ובני שכניה שמעיה ובני שמעיה חטוש ויגאל ובריח ונעריה ושפט--ששה 22
Wazao wa Shekania: Shemaya na wanawe: Hatushi, Igali, Baria, Nearia na Shafati; jumla yao walikuwa sita.
ובן נעריה אליועיני וחזקיה ועזריקם--שלשה 23
Wana wa Nearia walikuwa: Elioenai, Hizkia na Azrikamu; jumla yao watatu.
ובני אליועיני הודיוהו (הודויהו) ואלישיב ופליה ועקוב ויוחנן ודליה וענני--שבעה 24
Wana wa Elioenai walikuwa: Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohanani, Delaya na Anani; jumla yao wote saba.

< דברי הימים א 3 >