< 1 Corinthians 8 >

1 To speake of thinges dedicate vnto ydols we are sure that we all have knowledge. knowledge maketh a man swell: bnt love edifieth.
Yahusu sasa vyakula vilivyotambikiwa sanamu: Tunajua kwamba sisi sote tuna ujuzi, lakini ujuzi huo huwafanya watu wawe na majivuno; lakini mapendo hujenga.
2 If eny man thinke that he knoweth eny thinge he knoweth nothynge yet as he ought to knowe.
Anayefikiri kwamba anajua kitu, kwa kweli hajui chochote kama inavyompasa.
3 But yf eny man love god the same is knowen of him.
Lakini anayempenda Mungu huyo anajulikana naye.
4 To speake of meate dedicat vnto ydols we are sure that ther is none ydoll in the worlde and that ther is none other god but one.
Kwa hiyo, kuhusu vyakula vilivyotambikiwa sanamu, twajua kwamba sanamu si kitu duniani; twajua kwamba Mungu ni mmoja tu.
5 And though ther be yt are called goddes whether in heven other in erth (as ther be goddes many and lordes many)
Hata kama viko vitu viitwavyo miungu duniani au mbinguni, na hata kama wako miungu na mabwana wengi,
6 yet vnto vs is there but one god which is the father of whom are all thinges and we in him: and one lorde Iesus Christ by whom are all thinges and we by him.
hata hivyo, kwetu sisi yuko Mungu mmoja tu: Baba, Muumba wa vyote, ambaye kwa ajili yake sisi tuko. Pia yuko Bwana mmoja tu, Yesu Kristo, ambaye kwa njia yake vitu vyote viliumbwa, na sisi twaishi kwa njia yake.
7 But every man hath not knowledge. For some suppose that ther is an ydoll vntyll this houre and eate as of a thinge offered vnto ye ydole and so their consciences beynge yet weake are defyled.
Lakini, si kila mtu anao ujuzi huu. Maana wako watu wengine waliokwisha zoea sanamu, watu ambao mpaka hivi sasa wanapokula vyakula huviona bado kama vyakula vilivyotambikiwa sanamu. Na kwa vile dhamiri zao ni dhaifu, hutiwa unajisi.
8 Meate maketh vs not acceptable to god. Nether yf we eate are we ye better. Nether yf we eate not are we the worsse.
Lakini chakula hakiwezi kutupeleka karibu zaidi na Mungu. Tukiacha kukila hatupungukiwi kitu, tukikila hatuongezewi kitu.
9 But take hede that youre libertie cause not ye weake to faule.
Lakini, jihadharini: huu uhuru wenu usiwafanye walio na imani dhaifu waanguke katika dhambi.
10 For yf some man se ye which hast knowledge sit at meate in the ydoles teple shall not the conscience of hym which is weake be boldened to eate those thinges which are offered vnto ye ydole?
Maana, mtu ambaye dhamiri yake ni dhaifu, akikuona wewe mwenye ujuzi unakula vyakula hivyo ndani ya hekalu la sanamu, je, hatatiwa moyo wa kula vyakula vilivyotambikiwa sanamu?
11 And so thorow thy knowledge shall ye weake brother perisshe for whom christ dyed.
Hivyo, huyo ndugu yako dhaifu ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake, atapotea kwa sababu ya ujuzi wako.
12 Whe ye synne so agaynst the brethren and wounde their weake consciences ye synne agaynst Christ.
Kama mkiwakosesha ndugu zenu jinsi hiyo na kuzijeruhi dhamiri zao dhaifu, mtakuwa mmemkosea Kristo.
13 Wherfore yf meate hurt my brother I will eate no flesshe whill the worlde stondeth because I will not hurte my brother. (aiōn g165)
Kwa hiyo, ikiwa chakula husababisha kuanguka kwa ndugu yangu, sitakula nyama kamwe, nisije nikamfanya ndugu yangu aanguke katika dhambi. (aiōn g165)

< 1 Corinthians 8 >