< Ezekiel 28 >

1 [Then] Yahweh gave me another message. [He said]:
Neno la Bwana likanijia kusema:
2 “You human, give to the king of Tyre this message from [me], Yahweh the Lord: ‘You have very proudly claimed, “I am a god! I sit on a throne of a god [in a city on an island] in the sea!” You boast that you are a god; but you are only a man, not a god.
“Mwanadamu, mwambie mfalme wa Tiro, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “‘Kwa sababu moyo wako umejivuna na umesema, “Mimi ni mungu; nami ninaketi katika kiti cha enzi cha mungu katika moyo wa bahari.” Lakini wewe ni mwanadamu, wala si mungu, ingawa unafikiri kuwa una hekima kama mungu.
3 [You think that] you are wiser than Daniel was, [and you think that] you can understand every secret.
Je, wewe una hekima kuliko Danieli? Je, hakuna siri iliyofichika kwako?
4 By being wise and understanding [a lot], you have become [very] rich; you have acquired much gold and silver for your treasuries.
Kwa hekima yako na ufahamu wako, umejipatia utajiri, nawe umejikusanyia dhahabu na fedha katika hazina zako.
5 [Yes, it is true that] by trading wisely, you have been enabled to become very rich, and because you are rich, you have become very proud.
Kwa werevu wako mwingi katika biashara, umeongeza utajiri wako na kwa sababu ya utajiri wako moyo wako umekuwa na kiburi.
6 Therefore, this is what Yahweh the Lord says: “Because you think that you are as wise as a god,
“‘Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “‘Kwa sababu unafikiri una hekima, mwenye hekima kama mungu,
7 I will [now] bring a foreign [army] to attack your [country], an army that causes other nations to be terrified. They will pull out their swords to strike you, [you who think that] [IRO] you have marvelous/great wisdom, and they will destroy all your beautiful things.
mimi nitawaleta wageni dhidi yako, taifa katili kuliko yote; watafuta panga zao dhidi ya uzuri wa hekima yako, na kuchafua fahari yako inayongʼaa.
8 They will bring you down to your grave; you will die violently like [MET] those who died in the sea.
Watakushusha chini shimoni, nawe utakufa kifo cha kikatili katika moyo wa bahari.
9 Then you will certainly not [RHQ] say to those who are killing you, 'I am a god!' [because they will know that] you are not a god; you are only a man.
Je, wakati huo utasema, “Mimi ni mungu,” mbele ya wale wanaokuua? Utakuwa mwanadamu tu, wala si mungu, mikononi mwa hao wanaokuua.
10 You will die like other people who are unacceptable to me die, killed by foreigners.” [That will surely happen because] I, Yahweh, have said it.’”
Utakufa kifo cha wasiotahiriwa kwa mkono wa wageni. Kwa kuwa mimi nimenena, asema Bwana Mwenyezi.’”
11 Yahweh also gave me this message:
Neno la Bwana likanijia kusema:
12 “You human, sing a sad/funeral song about the king of Tyre. Say to him, ‘This is what Yahweh the Lord says: [“You thought that] [IRO] you were completely perfect, extremely wise and handsome.
“Mwanadamu, mfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, nawe umwambie: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “‘Ulikuwa kipeo cha ukamilifu, ukiwa umejaa hekima na mkamilifu katika uzuri.
13 You [had a wonderful life, as though] you were in my [beautiful] garden in Eden. Your [clothes] were decorated with many [HYP] kinds of very valuable stones— ruby, topaz, emerald, chrysolite, onyx, jasper, turquoise, and beryl [stones]. Those stones were set/placed in gold [mountings]. They were prepared for you on the day that you were born.
Ulikuwa ndani ya Edeni, bustani ya Mungu; kila kito cha thamani kilikupamba: akiki nyekundu, yakuti manjano na zumaridi, krisolitho, shohamu na yaspi, yakuti samawi, almasi na zabarajadi. Kuwekwa kwa hayo mapambo na kushikizwa kwake kulifanywa kwa dhahabu; siku ile ulipoumbwa yaliandaliwa tayari.
14 I appointed [DOU] you to be like [MET] a strong angel to guard the people. [It was as though I put] you on my holy mountain, and you walked among fiery stones.
Ulitiwa mafuta kuwa kerubi mlinzi, kwa kuwa hivyo ndivyo nilivyokuweka wakfu. Ulikuwa kwenye mlima mtakatifu wa Mungu; ulitembea katikati ya vito vya moto.
15 You were completely good in all that you did, from the day that you were created/born, until you [started to] do wicked things.
Ulikuwa mnyofu katika njia zako tangu siku ile ya kuumbwa kwako, hadi uovu ulipoonekana ndani yako.
16 [Then] you became busy trading things, and you started to act violently, and you sinned. So I caused you to be disgraced; and the angel who was guarding you forced you to leave my holy mountain, forced you to leave your place among those fiery stones.
Kutokana na biashara yako iliyoenea, ulijazwa na dhuluma, nawe ukatenda dhambi. Hivyo nilikuondoa kwa aibu kutoka mlima wa Mungu, nami nikakufukuza, ee kerubi mlinzi, kutoka katikati ya vito vya moto.
17 You were extremely proud because you were very handsome. Because you loved beautiful things, you did things that wise people do not do. [So] I threw you to the ground, and allowed [other] kings who saw you to laugh at you.
Moyo wako ukawa na kiburi kwa ajili ya uzuri wako, nawe ukaiharibu hekima yako kwa sababu ya fahari yako. Kwa hiyo nikakutupa chini; nimekufanya kioja mbele ya wafalme.
18 By committing many sins and by trading things dishonestly, you caused your places of worship to become unacceptable to me. So I caused a fire [to burn down your city]. [Your city] was burned completely; the people who were watching it saw that only ashes remained on the ground.
Kwa dhambi zako nyingi na biashara yako ya dhuluma, umenajisi mahali pako patakatifu. Kwa hiyo nilifanya moto utoke ndani yako, nao ukakuteketeza, nami nikakufanya majivu juu ya nchi, machoni pa wote waliokuwa wakitazama.
19 All the people who knew what your [city was like previously] were appalled. Now [your city] has disappeared, and it will not exist any more.”’”
Mataifa yote yaliyokujua yanakustajabia; umefikia mwisho wa kutisha na hutakuwepo tena milele.’”
20 [Then] Yahweh gave me another message. [He said],
Neno la Bwana likanijia kusema:
21 “You human, turn toward Sidon [city], and declare the terrible things that will happen to it.
“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Sidoni, ukatabiri dhidi yake,
22 Give [the people of Sidon] this message from [me], Yahweh the Lord: ‘I am your enemy, [you people of] Sidon, and by what I do to you, I will reveal that I am very great/glorious. When I punish you and reveal that I am holy, everyone who is watching that will know that it is I, Yahweh, [who have the power to do what I say that I will do].
nawe useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “‘Mimi ni kinyume chako, ee Sidoni, nami nitapata utukufu ndani yako. Nao watajua kwamba Mimi ndimi Bwana, nitakapotekeleza hukumu zangu na kuonyesha utakatifu wangu ndani yake.
23 I will send a plague upon you, and I will send [enemies to come and] kill [MTY] you in your streets. They will attack you from every direction, and your people will be slaughtered inside the walls of your city. Then everyone will know that I, Yahweh, [have the power to do what I say that I will do].'
Nitapeleka tauni ndani yake na kufanya damu itiririke katika barabara zake. Waliochinjwa wataanguka ndani yake, kwa upanga dhidi yake kila upande. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana.
24 No longer will those who live near you people of Israel [hurt you] like [MET] painful briers and sharp thorns [hurt people]. And then the Israeli people will know that I, Yahweh, [have the power to do what I say that I will do].”
“‘Nyumba ya Israeli hawatakuwa tena na majirani wenye nia ya kuwadhuru wanaoumiza kama michongoma na miiba mikali. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana Mwenyezi.
25 And this is [also] what Yahweh the Lord says: “Some day the people of Israel will live in their own land [again], the land that I gave to Jacob, who [also] served me. I will gather them from [distant] countries where I have scattered them. And I will reveal to the nations that I am holy among my people.
“‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitakapoikusanya nyumba ya Israeli kutoka mataifa ambako wametawanyika, nitajionyesha kuwa mtakatifu miongoni mwao machoni pa mataifa. Ndipo watakapoishi katika nchi yao wenyewe, niliyompa mtumishi wangu Yakobo.
26 My people will live safely in Israel; they will build houses and plant vineyards. And when I punish the nearby nations that despised them, they will know that it is I, Yahweh their God, [who has done it].”
Wataishi humo kwa salama na watajenga nyumba na kupanda mashamba ya mizabibu, wataishi kwa salama nitakapowaadhibu majirani zao wote ambao waliwafanyia uovu. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana, Mungu wao.’”

< Ezekiel 28 >