< Mathayo 16 >

1 Mafarisayo na Masadukayo walimwendea Yesu, na kwa kumjaribu, wakamwomba afanye ishara itokayo mbinguni.
And the Pharisees and Sadducees who came, testing, demanded him to exhibit to them a sign from the sky.
2 Lakini Yesu akawajibu, “Wakati wa jioni ukifika ninyi husema: Hali ya hewa itakuwa nzuri kwa maana anga ni jekundu!
But having answered, he said to them, When it becomes evening, ye say, Fair weather, for the sky is red.
3 Na alfajiri mwasema: Leo hali ya hewa itakuwa ya dhoruba, maana anga ni jekundu na tena mawingu yametanda! Basi, ninyi mnajua sana kusoma majira kwa kuangalia anga, lakini kutambua dalili za nyakati hizi hamjui.
And at morning, Bad weather today, for the sky is red, being gloomy. Hypocrites! Ye indeed know how to discern the face of the sky, but the signs of the times ye are not able.
4 Kizazi kiovu kisicho na uaminifu! Mnataka ishara, lakini hamtapewa ishara yoyote isipokuwa tu ile ya Yona.” Basi, akawaacha, akaenda zake.
An evil and adulterous generation seeks after a sign, and no sign will be given to it, except the sign of Jonah the prophet. And having left them behind, he departed.
5 Wanafunzi wake walipokwisha vukia upande wa pili wa ziwa, walijikuta wamesahau kuchukua mikate.
And his disciples having come to the other side, they forgot to take loaves.
6 Yesu akawaambia, “Muwe macho na mjihadhari na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo!”
And Jesus said to them, Watch and beware of the leaven of the Pharisees and Sadducees.
7 Lakini wao wakawa wanajadiliana: “Anasema hivyo kwa kuwa hatukuchukua mikate.”
And they deliberated among themselves, saying, We took no loaves.
8 Yesu alijua mawazo yao, akawaambia, “Enyi watu wenye imani haba! Mbona mnajadiliana juu ya kutokuwa na mikate?
And having known it, Jesus said to them, O ye of little faith, why do ye deliberate among yourselves because ye brought no loaves?
9 Je, hamjaelewa bado? Je, hamkumbuki nilipoimega ile mikate mitano kwa ajili ya wale watu elfu tano? Je, mlijaza vikapu vingapi vya makombo?
Do ye not yet understand, nor remember the five loaves of the five thousand, and how many baskets ye took up,
10 Au, ile mikate saba waliyogawiwa wale watu elfu nne, je, mlikusanya vikapu vingapi vya mabaki?
nor the seven loaves of the four thousand, and how many hampers ye took up?
11 Inawezekanaje hamwelewi ya kwamba sikuwa nikisema juu ya mikate? Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo!”
How do ye not understand that I spoke to you not about bread, to beware of the leaven of the Pharisees and Sadducees?
12 Hapo wanafunzi wakafahamu kwamba aliwaambia wajihadhari siyo na chachu ya mikate, bali na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.
Then they understood that he said not to beware of the leaven of bread, but of the teaching of the Pharisees and Sadducees.
13 Yesu alipofika pande za Kaisarea Filipi, aliwauliza wanafunzi wake, “Watu wanasema Mwana wa Mtu kuwa ni nani?”
Now when Jesus came into the regions of Caesarea Philippi, he asked his disciples, saying, Who do men say I, the Son of man, am?
14 Wakamjibu, “Wengine wanasema kuwa ni Yohane mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.”
And they said, Some, John the immerser, others, Elijah, but others, Jeremiah, or one of the prophets.
15 Yesu akawauliza, “Na ninyi je, mwasema mimi ni nani?”
He says to them, But who say ye, I am?
16 Simoni Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”
And Simon Peter having answered, said, Thou are the Christ, the Son of the living God.
17 Yesu akasema, “Heri wewe Simoni mwana wa Yona, kwa maana si binadamu aliyekufunulia ukweli huu, ila Baba yangu aliye mbinguni.
And having answered, Jesus said to him, Blessed are thou, Simon Bar-jonah, because flesh and blood has not revealed it to thee, but my Father in the heavens.
18 Nami nakwambia: wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala kifo chenyewe hakitaweza kulishinda. (Hadēs g86)
And I also say to thee, that thou are Peter, and upon this rock I will build my church, and the gates of Hades will not prevail against it. (Hadēs g86)
19 Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni; kila utakachofunga duniani, kitafungwa pia mbinguni; kila utakachofungua duniani, kitafunguliwa pia mbinguni.”
And I will give to thee the keys of the kingdom of the heavens, and whatever thou may bind on earth will be what is bound in the heavens, and whatever thou may loose on the earth will be what is loosed in the heavens.
20 Kisha akawaonya wanafunzi wasimwambie mtu yeyote kwamba yeye ndiye Kristo.
Then he commanded his disciples that they should tell no man that he is Jesus, the Christ.
21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwajulisha waziwazi wanafunzi wake: “Ni lazima mimi niende Yerusalemu, na huko nikapate mateso mengi yatakayosababishwa na wazee, makuhani wakuu na walimu wa Sheria. Nitauawa, na siku ya tatu nitafufuliwa.”
From that time Jesus began to show his disciples that he must go to Jerusalem, and suffer many things from the elders, and chief priests, and scholars, and be killed, and the third day be raised up.
22 Hapo Petro akamchukua kando, akaanza kumkemea: “Isiwe hivyo Bwana! Jambo hili halitakupata!”
And having taken him aside, Peter began to rebuke him, saying, Be merciful to thee, Lord. This will, no, not be to thee.
23 Lakini Yesu akageuka, akamwambia Petro, “Ondoka mbele yangu Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Mawazo yako si ya mungu bali ni ya kibinadamu!”
But having turned around, he said to Peter, Go thee behind me, Satan. Thou are my stumbling-block, because thou regard not the things of God, but the things of men.
24 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kama mtu yeyote anataka kuwa mfuasi wangu, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate.
Then Jesus said to his disciples, If any man wants to come behind me, let him deny himself, and take up his cross, and follow me.
25 Maana, mtu anayetaka kuyaokoa maisha yake mwenyewe, atayapoteza;
For whoever wants save his life will lose it, and whoever will lose his life for my sake will find it.
26 lakini mtu anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayapata. Je, mtu atafaidi nini akiupata utajiri wote wa ulimwengu na hali amepoteza maisha yake? Au, mtu atatoa kitu gani kiwe badala ya maisha yake?
For what does it profit a man, if he should gain the whole world, and lose his soul? Or what will a man give in exchange for his soul?
27 Maana, Mwana wa Mtu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika wake, na hapo ndipo atakapomlipa kila mtu kadiri ya matendo yake.
For the Son of man is going to come in the glory of his Father with his agents, and then he will reward each man according to his actions.
28 Kweli nawaambieni, wako wengine papahapa ambao hawatakufa kabla ya kumwona Mwana wa Mtu akija katika Ufalme wake.”
Truly I say to you, there are some of those who stand here, who will, no, not taste of death, until they see the Son of man coming in his kingdom.

< Mathayo 16 >