< Marko 16 >

1 Baada ya siku ya Sabato, Maria Magdalene, Salome na Maria mama yake Yakobo walinunua manukato ili wakaupake mwili wa Yesu.
And when the sabbath was past, Mary Magdalene, and Mary the mother of James, and Salome, bought spices, so that having come, they might anoint him.
2 Basi, alfajiri na mapema siku ya Jumapili, jua lilipoanza kuchomoza, walienda kaburini.
And very much early morning on the first day of the week, they come near to the sepulcher when the sun was risen.
3 Nao wakawa wanaambiana, “Nani atakayetuondolea lile jiwe mlangoni mwa kaburi?”
And they said to themselves, Who will roll away the stone for us from the door of the sepulcher?
4 Lakini walipotazama, waliona jiwe limekwisha ondolewa. (Nalo lilikuwa kubwa mno.)
And having looked, they see that the stone has been rolled back, for it was very large.
5 Walipoingia kaburini, walimwona kijana mmoja aliyevaa vazi jeupe, ameketi upande wa kulia; wakashangaa sana.
And having entered into the sepulcher, they saw a young man sitting on the right side, clothed in a white robe, and they were alarmed.
6 Lakini huyo kijana akawaambia, “Msishangae. Mnamtafuta Yesu wa Nazareti aliyesulubiwa. Amefufuka, hayumo hapa. Tazameni mahali walipokuwa wamemlaza.
And he says to them, Be not alarmed. Ye seek Jesus, the man of Nazareth who was crucified. He was raised. He is not here. Behold, the place where they laid him.
7 Nendeni mkawaambie wanafunzi wake pamoja na Petro ya kwamba anawatangulieni kule Galilaya. Huko mtamwona kama alivyowaambieni.”
But go, tell his disciples and Peter, that he goes before you into Galilee. Ye will see him there, just as he said to you.
8 Basi, wakatoka pale kaburini mbio, maana walitetemeka kwa hofu na kushangaa. Hawakumwambia mtu yeyote kitu, kwa sababu waliogopa mno.
And having come out, they fled from the sepulcher, and trembling and astonishment seized them. And they said nothing to any man, for they were afraid.
9 (note: The most reliable and earliest manuscripts do not include Mark 16:9-20.) Yesu alipofufuka mapema Jumapili, alijionyesha kwanza kwa Maria Magdalene, ambaye Yesu alikuwa amemtoa pepo saba.
(note: The most reliable and earliest manuscripts do not include Mark 16:9-20.) Now having risen early morning on the first day of the week, he appeared first to Mary Magdalene, from whom he had cast out seven demons.
10 Maria Magdalene akaenda, akawajulisha wale waliokuwa pamoja na Yesu, na wakati huo walikuwa wanaomboleza na kulia.
That woman, having gone, informed those who became with him, as they mourned and wept.
11 Lakini waliposikia ya kwamba Yesu yu hai na kwamba Maria Magdalene amemwona, hawakuamini.
And those men, when they heard that he is alive, and was seen by her, did not believe.
12 Baadaye Yesu aliwatokea wanafunzi wawili akiwa na sura nyingine. Wanafunzi hao walikuwa wanakwenda shambani.
And after these things he appeared in a different form to two of them as they walked going into the countryside.
13 Nao pia wakaenda wakawaambia wenzao. Hata hivyo hawakuamini.
And those men having departed, they reported to the others. Neither did they believe those men.
14 Mwishowe, Yesu aliwatokea wanafunzi kumi na mmoja walipokuwa pamoja mezani. Akawakemea sana kwa sababu ya kutoamini kwao na ukaidi wao, maana hawakuwaamini wale waliokuwa wamemwona baada ya kufufuka.
Afterward he became visible to them, to the eleven, who were relaxing. And he upbraided their unbelief and hard heart, because they did not believe those who saw him after he was raised.
15 Basi, akawaambia, “Nendeni ulimwenguni kote mkahubiri Habari Njema kwa kila mtu.
And he said to them, Having gone into all the world, preach ye the good news to the whole creation.
16 Anayeamini na kubatizwa ataokolewa; asiyeamini atahukumiwa.
He who believes and is immersed will be saved, but he who does not believe will be damned.
17 Na ishara hizi zitaandamana na wale wanaoamini: kwa jina langu watatoa pepo na watasema kwa lugha mpya.
And these signs will accompany those who believe: In my name they will cast out demons. They will speak in new tongues.
18 Wakishika nyoka au wakinywa kitu chochote chenye sumu, hakitawadhuru. Watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona.”
They will take up serpents, and if they drink anything deadly, it will, no, not harm them. They will lay hands on the feeble, and they will fare well.
19 Basi, Bwana Yesu alipokwisha sema nao, akachukuliwa mbinguni, akaketi upande wa kulia wa Mungu.
Therefore indeed, the Lord, after he spoke to them, was taken up into heaven, and sat down at the right hand of God.
20 Wanafunzi wakaenda wakihubiri kila mahali. Bwana akafanya kazi pamoja nao na kuimarisha ujumbe huo kwa ishara zilizoandamana nao.
And those men, having gone forth, they preached everywhere, the Lord working jointly, and confirming the word by the signs that followed. Truly.

< Marko 16 >