< Luka 9 >

1 Yesu aliwaita wale kumi na wawili, akawapa uwezo juu ya pepo wote, na uwezo wa kuponya wagonjwa.
He called the twelve together, and gave them power and authority over all demons and to cure diseases.
2 Halafu akawatuma waende kuhubiri Ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.
He sent them forth to proclaim the Kingdom of God, and to heal the sick.
3 Akawaambia, “Mnaposafiri msichukue chochote: msichukue fimbo, wala mkoba, wala chakula, wala fedha, wala hata koti la ziada.
And he said to them, "Take nothing for your journey—neither staff, nor pack, nor bread, nor money; neither have two tunics.
4 Nyumba yoyote mtakayoingia na kukaribishwa, kaeni humo mpaka mtakapoondoka katika kijiji hicho.
Into whatever house you enter, stay there, and depart from there.
5 Watu wakikataa kuwakaribisha, tokeni katika mji huo, nanyi mnapotoka kung'uteni mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.”
As many as do not receive you, when you depart from that city, shake off even the dust from your feet for a testimony against them."
6 Basi, wakaanza safari, wakapitia vijijini wakihubiri Habari Njema na kuponya wagonjwa kila mahali.
They departed, and went throughout the villages, preaching the Good News, and healing everywhere.
7 Sasa, mtawala Herode, alipata habari za mambo yote yaliyokuwa yanatendeka, akawa na wasiwasi kwa vile walikuwa wakisema: “Yohane amefufuka kutoka wafu!”
Now Herod the tetrarch heard of all that was done; and he was very perplexed, because it was said by some that Yukhanan had risen from the dead,
8 Wengine walisema kwamba Eliya ametokea, na wengine walisema kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amerudi duniani.
and by some that Eliya had appeared, and by others that one of the old prophets had risen again.
9 Lakini Herode akasema, “Huyo Yohane nilimkata kichwa; sasa ni nani huyu ninayesikia habari zake?” Akawa na hamu ya kumwona.
Herod said, "Yukhanan I beheaded, but who is this, about whom I hear such things?" He sought to see him.
10 Wale mitume waliporudi, walimweleza yote waliyoyafanya. Yesu akawachukua, wakaenda peke yao mjini Bethsaida.
The apostles, when they had returned, told him what things they had done. He took them, and withdrew apart to a city called Beth-Sayada.
11 Lakini wale watu walipojua alikokwenda, walimfuata. Yesu akawakaribisha akawazungumzia juu ya Ufalme wa Mungu, akawaponya wale waliohitaji kuponywa.
But the crowds, perceiving it, followed him. He welcomed them, and spoke to them of the Kingdom of God, and he cured those who needed healing.
12 Jua lilipokuwa linaanza kutua, wale kumi na wawili walimwendea wakamwambia, “Waage watu waende kwenye vijiji na mashamba ya karibu, wakajipatie chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tulipo ni nyikani.”
The day began to wear away; and the twelve came, and said to him, "Send the crowd away, that they may go into the surrounding villages and farms, and lodge, and get food, for we are here in a deserted place."
13 Lakini Yesu akawaambia, “Wapeni ninyi chakula.” Wakamjibu, “Hatuna chochote ila mikate mitano na samaki wawili. Labda twende wenyewe tukawanunulie chakula watu wote hawa!”
But he said to them, "You give them something to eat." They said, "We have no more than five loaves and two fish, unless we should go and buy food for all these people."
14 (Walikuwepo pale wanaume wapatao elfu tano.) Basi, Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Waambieni watu waketi katika makundi ya watu hamsinihamsini.”
For they were about five thousand men. He said to his disciples, "Make them sit down in groups of about fifty each."
15 Wanafunzi wakafanya walivyoambiwa, wakawaketisha wote.
They did so, and made them all sit down.
16 Kisha Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akamshukuru Mungu, akavimega, akawapa wanafunzi wake wawagawie watu.
He took the five loaves and the two fish, and looking up to the sky, he blessed them, and broke them, and gave them to the disciples to set before the crowd.
17 Wakala wote, wakashiba; wakakusanya makombo ya chakula, wakajaza vikapu kumi na viwili.
They ate, and were all filled. They gathered up twelve baskets of broken pieces that were left over.
18 Siku moja, Yesu alikuwa anasali peke yake, na wanafunzi wake walikuwa karibu. Basi, akawauliza, “Eti watu wanasema mimi ni nani?”
It happened, as he was praying alone, that the disciples were with him, and he asked them, "Who do the crowds say that I am?"
19 Nao wakamjibu, “Wengine wanasema kuwa wewe ni Yohane mbatizaji, wengine wanasema wewe ni Eliya, hali wengine wanasema kuwa wewe ni mmoja wa manabii wa kale ambaye amefufuka.”
They answered, "'Yukhanan the Baptist,' but others say, 'Eliya,' and others, that one of the old prophets is risen again."
20 Hapo akawauliza, “Na ninyi je, mwasema mimi ni nani?” Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo wa Mungu.”
He said to them, "But who do you say that I am?" Kipha answered, "The Meshikha of God."
21 Halafu Yesu akawaamuru wasimwambie mtu yeyote habari hiyo.
But he warned them, and commanded them to tell this to no one,
22 Akaendelea kusema: “Ni lazima Mwana wa Mtu apate mateso mengi na kukataliwa na wazee na makuhani wakuu na walimu wa Sheria; atauawa, lakini siku ya tatu atafufuliwa.”
saying, "The Son of Man must suffer many things, and be rejected by the elders, chief priests, and scribes, and be killed, and the third day be raised up."
23 Kisha akawaambia watu wote, “Mtu yeyote akitaka kuwa mfuasi wangu, ni lazima ajikane nafsi yake, auchukue msalaba wake kila siku, anifuate.
He said to all, "If anyone desires to come after me, let him deny himself, take up his cross daily, and follow me.
24 Maana, mtu anayetaka kuyaokoa maisha yake mwenyewe, atayapoteza; lakini atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayaokoa.
For whoever desires to save his life will lose it, but whoever will lose his life for my sake, the same will save it.
25 Je, kuna faida gani mtu kuupata utajiri wote wa dunia kwa kujipoteza au kujiangamiza yeye mwenyewe?
For what does it profit a person if he gains the whole world, and loses or forfeits his own self?
26 Mtu akinionea aibu mimi na mafundisho yangu, Mwana wa Mtu atamwonea aibu mtu huyo wakati atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu.
For whoever will be ashamed of me and of my words, of him will the Son of Man be ashamed, when he comes in his glory, and the glory of the Father, and of the holy angels.
27 Nawaambieni kweli, kuna wengine papa hapa ambao hawatakufa kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu.”
But I tell you the truth: There are some of those who stand here, who will in no way taste of death, until they see the Kingdom of God."
28 Yapata siku nane baada ya kusema hayo, Yesu aliwachukua Petro, Yohane na Yakobo, akaenda nao mlimani kusali.
It happened about eight days after these sayings, that he took with him Kipha, Yukhanan, and Yaquv, and went up onto the mountain to pray.
29 Alipokuwa akisali, sura yake ilibadilika, mavazi yake yakawa meupe na kung'aa sana.
As he was praying, the appearance of his face was altered, and his clothing became white and dazzling.
30 Na watu wawili wakaonekana wakizungumza naye, nao ni Mose na Eliya,
And look, two men were talking with him, who were Mushe and Eliya,
31 ambao walitokea wakiwa wenye utukufu, wakazungumza naye juu ya kifo chake ambacho angekikamilisha huko Yerusalemu.
who appeared in glory, and spoke of his departure, which he was about to accomplish at Urishlim.
32 Petro na wenzake walikuwa wamelemewa na usingizi mzito, hata hivyo waliamka, wakauona utukufu wake, wakawaona na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye.
Now Kipha and those who were with him were heavy with sleep, but when they were fully awake, they saw his glory, and the two men who stood with him.
33 Basi, watu hao wawili walipokuwa wakiondoka, Petro alimwambia Yesu, “Bwana, ni vizuri kwamba tupo hapa: basi, tujenge vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Eliya.” —Kwa kweli hakujua anasema nini.
It happened, as they were parting from him, that Kipha said to Yeshua, "Master, it is good for us to be here. Let us make three tents: one for you, and one for Mushe, and one for Eliya," not knowing what he said.
34 Petro alipokuwa akisema hayo, mara wingu likatokea na kuwafunika; na wingu hilo lilipowajia, wale wanafunzi waliogopa sana.
While he said these things, a cloud came and overshadowed them, and they were afraid as they entered into the cloud.
35 Sauti ikasikika kutoka katika hilo wingu: “Huyu ndiye Mwanangu niliyemchagua, msikilizeni.”
A voice came out of the cloud, saying, "This is my Son, my Chosen One. Listen to him."
36 Baada ya hiyo sauti kusikika, Yesu alionekana akiwa peke yake. Wanafunzi walikaa kimya juu ya tukio hilo, na wakati ule hawakumwambia mtu yeyote mambo hayo waliyoyaona.
When the voice came, Yeshua was found alone. They were silent, and told no one in those days any of the things which they had seen.
37 Kesho yake walipokuwa wakishuka kutoka kule mlimani, kundi kubwa la watu lilikutana na Yesu.
It happened on the next day, when they had come down from the mountain, that a large crowd met him.
38 Hapo, mtu mmoja katika lile kundi akapaaza sauti, akasema, “Mwalimu! Ninakusihi umwangalie mwanangu—mwanangu wa pekee!
And look, a man from the crowd called out, saying, "Teacher, I beg you to look at my son, for he is my only child.
39 Pepo huwa anamshambulia, na mara humfanya apige kelele; humtia kifafa, na povu likamtoka kinywani. Huendelea kumtesa sana, asimwache upesi.
And look, a spirit seizes him, and all at once he cries out, and it convulses him so that he foams, and it hardly departs from him, bruising him severely.
40 Niliwaomba wanafunzi wako wamfukuze, lakini hawakuweza.”
I begged your disciples to cast it out, and they could not."
41 Yesu akasema, “Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka! Nitakaa nanyi na kuwavumilia mpaka lini?” Kisha akamwambia huyo mtu, “Mlete mtoto wako hapa.”
Yeshua answered, "Faithless and perverse generation, how long must I be with you and put up with you? Bring your son here."
42 Wakati mtoto huyo alipokuwa anamjia Yesu, yule pepo alimwangusha chini na kumtia kifafa. Lakini Yesu akamkemea yule pepo mchafu akamponya mtoto na kumkabidhi kwa baba yake.
While he was still coming, the demon threw him down and convulsed him violently. But Yeshua rebuked the unclean spirit, and healed the boy, and gave him back to his father.
43 Watu wote wakashangazwa na uwezo mkuu wa Mungu. Wale watu walipokuwa bado wanashangaa juu ya mambo yote aliyofanya, Yesu aliwaambia wanafunzi wake,
They were all astonished at the majesty of God. But while all were marveling at all the things which Yeshua did, he said to his disciples,
44 “Tegeni masikio, myasikie mambo haya: Mwana wa Mtu anakwenda kutiwa mikononi mwa watu.”
"Let these words sink into your ears, for the Son of Man will be delivered up into the hands of men."
45 Lakini wao hawakuelewa maana ya usemi huo. Jambo hilo lilikuwa limefichwa kwao ili wasitambue; nao wakaogopa kumwuliza juu ya msemo huo.
But they did not understand this saying. It was concealed from them, that they should not perceive it, and they were afraid to ask him about this saying.
46 Kukatokea majadiliano kati ya wale wanafunzi kuhusu nani kati yao aliyekuwa mkuu zaidi.
There arose an argument among them about which of them was the greatest.
47 Yesu aliyajua mawazo yaliyokuwa mioyoni mwao; basi akamchukua mtoto mdogo akamweka karibu naye,
Yeshua, knowing the reasoning of their hearts, took a little child, and set him by his side,
48 akawaambia, “Mtu yeyote anayempokea mtoto huyu mdogo kwa jina langu, ananipokea mimi; na yeyote anayenipokea mimi, anampokea yule aliyenituma. Maana yule aliye mdogo kuliko wote kati yenu ndiye aliye mkubwa kuliko wote.”
and said to them, "Whoever receives this little child in my name receives me. Whoever receives me receives him who sent me. For whoever is least among you all, this one is great."
49 Yohane alidakia na kusema, “Bwana, tumemwona mtu mmoja akitoa pepo kwa kulitumia jina lako nasi tukajaribu kumkataza kwa kuwa yeye si mmoja wetu.”
Yukhanan answered, "Master, we saw someone casting out demons in your name, and we forbade him, because he does not follow with us."
50 Lakini Yesu akamwambia, “Msimkataze; kwani asiyepingana nanyi yuko upande wenu.”
Yeshua said to him, "Do not forbid him, for he who is not against you is for you."
51 Wakati ulipokaribia ambapo Yesu angechukuliwa juu mbinguni, yeye alikata shauri kwenda Yerusalemu.
It came to pass, when the days were near that he should be taken up, he intently set his face to go to Urishlim,
52 Basi, akawatuma wajumbe wamtangulie, nao wakaenda wakaingia kijiji kimoja cha Wasamaria ili wamtayarishie mahali.
and sent messengers before his face. They went, and entered into a village of the Samaritans, so as to prepare for him.
53 Lakini wenyeji wa hapo hawakutaka kumpokea kwa sababu alikuwa anaelekea Yerusalemu.
But they did not receive him, because he was traveling with his face set towards Urishlim.
54 Basi, wanafunzi wake, kina Yohane na Yakobo, walipoona hayo, wakasema, “Bwana, wataka tuamuru moto ushuke kutoka mbinguni uwateketeze?”
When his disciples, Yaquv and Yukhanan, saw this, they said, "Lord, do you want us to command fire to come down from the sky, and consume them?"
55 Lakini yeye akawageukia, akawakemea akasema, “Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo;
And he turned and rebuked them, and said, "You do not realize what kind of Rukha you belong to.
56 kwa maana Mwana wa Mtu hakuja kuyaangamiza maisha ya watu, bali kuyaokoa.” Wakatoka, wakaenda kijiji kingine.
For the Son of Man did not come to destroy people's lives, but to save them." And they went to another village.
57 Walipokuwa wakisafiri njiani, mtu mmoja akamwambia Yesu, “Nitakufuata kokote utakakokwenda.”
As they went on the way, a certain man said to him, "I want to follow you wherever you go."
58 Yesu akasema, “Mbweha wana mapango, na ndege wana viota; lakini Mwana wa Mtu hana mahali pa kupumzikia.”
And Yeshua said to him, "The foxes have holes, and the birds of the sky have nests, but the Son of Man has no place to lay his head."
59 Kisha akamwambia mtu mwingine, “Nifuate.” Lakini huyo akasema, “Bwana, niruhusu kwanza niende kumzika baba yangu.”
He said to another, "Follow me." But he said, "Lord, allow me first to go and bury my father."
60 Yesu akamwambia, “Waache wafu wazike wafu wao; bali wewe nenda ukatangaze Ufalme wa Mungu.”
But Yeshua said to him, "Leave the dead to bury their own dead, but you go and announce the Kingdom of God."
61 Na mtu mwingine akamwambia, “Nitakufuata, lakini niruhusu kwanza nikawaage wale walio nyumbani kwangu.”
Another also said, "I want to follow you, Lord, but first allow me to bid farewell to those who are at my house."
62 Yesu akamwambia, “Yeyote anayeshika jembe tayari kulima na huku anaangalia nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu.”
But Yeshua said to him, "No one, having put his hand to the plow, and looking back, is fit for the Kingdom of God."

< Luka 9 >