< Luka 3 >

1 Mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alikuwa anatawala mkoa wa Yudea. Herode alikuwa mkuu wa mkoa wa Galilaya, na Filipo, ndugu yake, alikuwa mkuu wa mikoa ya Iturea na Trakoniti. Lusania alikuwa mkuu wa mkoa wa Abilene,
Sasa, katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberia, wakati Pontio Pilato alikuwa gavana wa Uyahudi, Herode alikuwa mkuu wa mkoa wa Galilaya, na Filipo ndugu yake alikuwa mkuu wa mkoa wa Iturea na Trakoniti, na Lisania alikuwa mkuu wa mkoa wa Abilene,
2 na Anasi na Kayafa walikuwa makuhani wakuu mjini Yerusalem. Wakati huo ndipo neno la Mungu lilipomjia Yohane, mwana wa Zakariya, kule jangwani.
na wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa, Neno la Mungu lilimjia Yohana mwana wa Zakaria, jangwani.
3 Basi, Yohane akaenda katika sehemu zote zilizopakana na mto Yordani, akihubiri watu watubu na kubatizwa ili Mungu awaondolee dhambi.
Alisafiri katika mkoa wote kuzunguka Mto Yordani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi
4 Ndivyo ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Sauti ya mtu imesikika jangwani: Mtayarishieni Bwana njia yake; nyosheni mapito yake.
Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha maneno ya Isaya nabii, “sauti ya mtu aliaye nyikani, “Itengenezeni tayari njia ya Bwana, yatengenezeni mapito yake yaliyoonyoka.
5 Kila bonde litafukiwa, kila mlima na kilima vitasawazishwa; palipopindika patanyooshwa, njia mbaya zitatengenezwa.
Kila bonde litajazwa, kila mlima na kilima vitasawazishwa, barabara zilizopinda zitanyoshwa, na njia zilizoparaza zitalainishwa.
6 Na, watu wote watauona wokovu utokao kwa Mungu.”
Watu wote watauona wokovu wa Mungu.”
7 Basi, Yohane akawa anawaambia watu wengi waliofika ili awabatize: “Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea kwamba mngeweza kuiepuka ghadhabu inayokuja?
Hivyo, Yohana akawaambia makutano makubwa ya watu waliomjia wapate kubatizwa na yeye, “Ninyi uzao wa nyoka wenye sumu, nani aliwaonya kuikimbia gadhabu inayokuja?
8 Basi, onyesheni kwa matendo kwamba mmetubu. Msianze sasa kusema: Sisi ni watoto wa Abrahamu. Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyageuza mawe haya yawe watoto wa Abrahamu!
Zaeni matunda yanayoedana na toba, na msianze kusema ndani yenu, “Tunaye Ibarahimu ambaye ni baba yetu; kwa sababu nawaambia ya kwamba, Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto hata kutokana na mawe haya.
9 Lakini, sasa hivi shoka limewekwa tayari kukata mizizi ya miti. Kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni.”
Tayari shoka limeshawekwa kwenye mzizi wa miti. Hivyo, kila mti usiozaa matunda mema, hukatwa na kutupwa motoni.
10 Umati wa watu ukamwuliza, “Tufanye nini basi?”
Kisha watu katika makutano walimuuliza wakisema, “Sasa tunatakiwa tufanyeje?”
11 Akawajibu, “Aliye na nguo mbili amgawie yule asiye na nguo; aliye na chakula afanye vivyo hivyo.”
Alijibu na kuwaambia, “kama mtu ana kanzu mbili anatakiwa atoe kanzu moja kwa mwingine ambaye hana kabisa, na ambaye ana chakula na afanye vivyo hivyo.”
12 Nao watoza ushuru wakaja pia ili wabatizwe, wakamwuliza, “Mwalimu, tufanye nini?”
Kisha baadhi ya watoza ushuru walikuja pia kubatizwa, na wakamwambia, “Mwalimu, tunatakiwa kufanya nini?
13 Naye akawaambia, “Msitoze ushuru zaidi ya kima kilichowekwa.”
Akawaambia, “Msikusanye fedha zaidi kuliko mnachotakiwa kukusanya.”
14 Nao askari wakamwuliza, “Na sisi tufanye nini?” Naye akawajibu, “Msichukue vitu vya mtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyote kwa uongo. Toshekeni na mishahara yenu.”
Baadhi ya maaskari pia wakamuuliza wakisema, “Na sisi je? Tunatakiwa tufanye nini?” Akawambia, “Msichukue fedha kwa mtu yeyote kwa nguvu, na msimtuhumu mtu yeyote kwa uongo. Ridhikeni na mishahara yenu.”
15 Wote walikuwa wanatazamia kitu fulani; basi, wakaanza kujiuliza mioyoni mwao kuhusu Yohane: kuwa labda yeye ndiye Kristo.
Sasa, kwa kuwa watu walikuwa na shauku ya kumngojea Kristo atakaye kuja, kila mmoja alikuwa anawaza moyoni mwake kuhusu Yohana kama yeye ndiye Kristo.
16 Hapo Yohane akawaambia wote, “Mimi ninawabatiza kwa maji, lakini anakuja mwenye uwezo zaidi kuliko mimi ambaye sistahili hata kumfungulia kamba za viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
Yohana akajibu kwa kuwaambia wote, “Mimi nawabatiza ninyi kwa maji, lakini kuna mmoja ajaye ambaye ana nguvu kuliko mimi, na sisitahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Atawabatiza ninyi kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
17 Yeye ni kama mtu anayeshika mikononi mwake chombo cha kupuria nafaka, aipure nafaka yake, akusanye ngano ghalani mwake, na makapi ayachome kwa moto usiozimika.”
Pepeto lake liko mkononi mwake ili kusafisha vizuri uwanda wake wa kupepetea ngano na kuikusanya ngano ghalani mwake. Lakini, atayateketeza makapi kwa moto ambao hauwezi kuzimika.
18 Hivyo, pamoja na mawaidha mengine mengi, Yohane aliwahimiza watu akiwahubiria Habari Njema.
Kwa maonyo mengine mengi pia, alihubiri habari njema kwa watu.
19 Lakini Yohane alimgombeza Herode, mkuu wa mkoa, kwa sababu alikuwa amemchukua Herodia, mke wa ndugu yake, na kumfanya mke wake; na pia kwa ajili ya mabaya yote aliyokuwa amefanya.
Yohana alimkemea pia Herode mkuu wa mkoa kwa kumuoa Herodia, mke wa ndugu yake na kwa maovu mengine mengi ambayo Herode alikuwa ameyatenda.
20 Kisha Herode akazidisha ubaya wake kwa kumtia Yohane gerezani.
Lakini baadaye Herode alifanya uovu mwingine mbaya sana. Alimfunga Yohana gerezani.
21 Watu wote walipokuwa wamekwisha batizwa, Yesu naye alibatizwa. Na alipokuwa akisali, mbingu zilifunguka,
Kisha ilitokea kwamba, wakati watu wote walipokuwa wakibatizwa na Yohana, naye Yesu alibatizwa pia. Wakati alipokuwa akiomba, mbingu zikafunguka.
22 na Roho Mtakatifu akamshukia akiwa na umbo kama la njiwa. Sauti ikasikika kutoka mbinguni: “Wewe ndiwe Mwanangu mpendwa, nimependezwa nawe.”
Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili kama njiwa, wakati huo huo sauti ikaja kutoka mbinguni ikisema, “Wewe ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa sana na wewe.”
23 Yesu alipoanza kazi yake hadharani, alikuwa na umri upatao miaka thelathini, na watu walidhani yeye ni mwana wa Yosefu, mwana wa Heli.
Sasa Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa na umri upatao miaka thelathini. Alikuwa ni mwana (kama ilivyotadhaniwa) wa Yusufu, mwana wa Eli,
24 Heli alikuwa mwana wa Mathati, mwana wa Lawi, mwana wa Melki, mwana wa Yanai, mwana wa Yosefu,
mwana wa Mathati, mwana wa Lawi, mwana wa Melki, mwana wa Yana, mwana wa Yusufu,
25 mwana wa Matathia, mwana wa Amosi, mwana wa Nahumu, mwana wa Hesli, mwana wa Nagai,
mwana wa Matathia, mwana wa Amosi, mwana wa Nahumu, mwana wa Esli, mwana wa Nagai,
26 mwana wa Maathi, mwana wa Matathia, mwana wa Shemeni, mwana wa Yoseki, mwana wa Yuda,
mwana wa Maati, mwana wa Matathia, mwana wa Semeini, mwana wa Yusufu, mwana wa Yuda,
27 mwana wa Yohanani, mwana wa Resa, mwana wa Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mwana wa Neri,
mwana wa Yoanani, mwana wa Resa, mwana wa Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mwana wa Neri,
28 mwana wa Melki, mwana wa Adi, mwana wa Kosamu, mwana wa Elmadamu, mwana wa Eri,
mwana wa Melki, mwana wa Adi, mwana wa Kosamu, mwana wa Elmadamu, mwana wa Eri,
29 mwana wa Yoshua, mwana wa Eliezeri, mwana wa Yorimu, mwana wa Mathati, mwana wa Lawi,
mwana wa Yoshua, mwana wa Eliezeri, mwana wa Yorimu, mwana wa Matathi, mwana wa Lawi,
30 mwana wa Simeoni, mwana wa Yuda, mwana wa Yosefu, mwana wa Yonamu, mwana wa Eliakimu,
mwana wa Simeoni, mwana wa Yuda, mwana wa Yusufu, mwana wa Yonamu, mwana wa Eliyakimu,
31 mwana wa Melea, mwana wa Mena, mwana wa Matatha, mwana wa Nathani, mwana wa Daudi,
mwana wa Melea, mwana wa Mena, mwana wa Matatha, mwana wa Nathani, mwana wa Daudi,
32 mwana wa Yese, mwana wa Obedi, mwana wa Boazi, mwana wa Salmoni, mwana wa Nashoni,
mwana wa Yese, mwana wa Obedi, mwana wa Boazi, mwana wa Salmoni, mwana wa Nashoni,
33 mwana wa Aminadabu, mwana wa Admini, mwana wa Arni, mwana wa Hesroni, mwana wa Feresi, mwana wa Yuda,
mwana wa Abinadabu, mwana wa Aramu, mwana wa Hesroni, mwana wa Peresi, mwana wa Yuda,
34 mwana wa Yakobo, mwana wa Isaka, mwana wa Abrahamu, mwana wa Tera, mwana wa Nahori,
mwana wa Yakobo, mwana wa Isaka, mwana wa Ibrahimu, mwana wa Tera, mwana wa Nahori,
35 mwana wa Serugi, mwana wa Reu, mwana wa Pelegi, mwana wa Eberi, mwana wa Sala,
mwana wa Seruig, mwana wa Ragau, mwana wa Pelegi, mwana wa Eberi, mwana wa Sala,
36 mwana wa Kainani, mwana wa Arfaksadi, mwana wa Shemu, mwana wa Noa, mwana wa Lameki,
mwana wa Kenani, mwana wa Arfaksadi, mwana wa Shemu, mwana wa Nuhu, mwana wa Lameki,
37 mwana wa Mathusala, mwana wa Henoki, mwana wa Yaredi, mwana wa Mahalaleli, mwana wa Kenani,
mwana wa Methusela, mwana wa Henoko, mwana wa Yaredi, mwana Mahalalei, mwana wa Kenani,
38 mwana wa Enosi, mwana wa Sethi, mwana wa Adamu, aliyekuwa wa Mungu.
mwana wa Enoshi, mwana wa Sethi, mwana wa Adamu, mwana wa Mungu.

< Luka 3 >