< Yohana 10 >

1 Yesu alisema “Kweli nawaambieni, yeyote yule asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni, bali hupenya na kuingia kwa njia nyingine, huyo ni mwizi na mnyang'anyi.
“Os aseguro que el que no entra por la puerta en el redil de las ovejas, sino que sube por otro camino, es un ladrón y un salteador.
2 Lakini anayeingia kwa kupitia mlangoni, huyo ndiye mchungaji wa kondoo.
Pero el que entra por la puerta es el pastor de las ovejas.
3 Mngoja mlango wa zizi humfungulia, na kondoo husikia sauti yake, naye huwaita kondoo wake kila mmoja kwa jina lake na kuwaongoza nje.
El guardián le abre la puerta, y las ovejas escuchan su voz. Llama a sus ovejas por su nombre y las saca.
4 Akisha watoa nje huwatangulia mbele nao kondoo humfuata, kwani wanaijua sauti yake.
Cada vez que saca a sus ovejas, va delante de ellas; y las ovejas le siguen, porque conocen su voz.
5 Kondoo hao hawawezi kumfuata mgeni, bali watamkimbia kwa sababu hawaijui sauti yake.”
No seguirán en absoluto a un extraño, sino que huirán de él, porque no conocen la voz de los extraños.”
6 Yesu aliwaambia mfano huo, lakini wao hawakuelewa alichotaka kuwaambia.
Jesús les dijo esta parábola, pero no entendieron lo que les decía.
7 Basi, akasema tena, “Kweli nawaambieni, mimi ni mlango wa kondoo.
Por eso Jesús les volvió a decir: “Os aseguro que yo soy la puerta de las ovejas.
8 Wale wengine wote waliokuja kabla yangu ni wezi na wanyang'anyi, nao kondoo hawakuwasikiliza.
Todos los que vinieron antes que yo son ladrones y salteadores, pero las ovejas no les hicieron caso.
9 Mimi ni mlango. Anayeingia kwa kupitia kwangu ataokolewa; ataingia na kutoka, na kupata malisho.
Yo soy la puerta. Si alguien entra por mí, se salvará, y entrará y saldrá y hallará pastos.
10 Mwizi huja kwa shabaha ya kuiba, kuua na kuharibu. Mimi nimekuja mpate kuwa na uzima—uzima kamili.
El ladrón sólo viene a robar, matar y destruir. Yo he venido para que tengan vida y la tengan en abundancia.
11 “Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo wake.
“Yo soy el buen pastor. El buen pastor da su vida por las ovejas.
12 Mtu wa kuajiriwa ambaye si mchungaji, na wala kondoo si mali yake, anapoona mbwa mwitu anakuja, huwaacha kondoo na kukimbia. Kisha mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya.
El que es asalariado y no pastor, que no es dueño de las ovejas, ve venir al lobo, deja las ovejas y huye. El lobo arrebata las ovejas y las dispersa.
13 Yeye hajali kitu juu ya kondoo kwa sababu yeye ni mtu wa mshahara tu.
El jornalero huye porque es jornalero y no cuida de las ovejas.
14 Mimi ni mchungaji mwema. Nawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi,
Yo soy el buen pastor. Conozco a las mías, y soy conocido por las mías;
15 kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Mimi nayatoa maisha yangu kwa ajili yao.
así como el Padre me conoce, y yo conozco al Padre. Yo doy mi vida por las ovejas.
16 Tena ninao kondoo wengine ambao hawamo zizini humu. Inanibidi kuwaleta hao pia, nao wataisikia sauti yangu, na kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.
Tengo otras ovejas que no son de este redil. Debo traerlas también, y oirán mi voz. Serán un solo rebaño con un solo pastor.
17 “Baba ananipenda kwani nautoa uhai wangu ili nipate kuupokea tena.
Por eso el Padre me ama, porque doy mi vida para volver a tomarla.
18 Hakuna mtu anayeninyang'anya uhai wangu; mimi na nautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa na uwezo wa kuuchukua tena. Hivi ndivyo Baba alivyoniamuru nifanye.”
Nadie me la quita, sino que yo mismo la pongo. Tengo poder para ponerla, y tengo poder para volver a tomarla. Este mandamiento lo recibí de mi Padre”.
19 Kukawa tena na mafarakano kati ya Wayahudi kwa sababu ya maneno haya.
Por eso volvió a surgir una división entre los judíos a causa de estas palabras.
20 Wengi wao wakasema, “Ana pepo; tena ni mwendawazimu! Ya nini kumsikiliza?”
Muchos de ellos decían: “¡Tiene un demonio y está loco! ¿Por qué le escucháis?”
21 Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mwenye pepo. Je, pepo anaweza kuyafumbua macho ya vipofu?”
Otros decían: “Estos no son los dichos de un poseído por un demonio. No es posible que un demonio abra los ojos de los ciegos, ¿verdad?”
22 Huko Yerusalemu kulikuwa na sikukuu ya Kutabaruku. Wakati huo ulikuwa wa baridi.
Era la fiesta de la Dedicación en Jerusalén.
23 Naye Yesu akawa anatembea Hekaluni katika ukumbi wa Solomoni.
Era invierno, y Jesús andaba por el templo, en el pórtico de Salomón.
24 Basi, Wayahudi wakamzunguka, wakamwuliza, “Utatuacha katika mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo, basi, tuambie wazi.”
Los judíos se acercaron a él y le dijeron: “¿Hasta cuándo nos vas a tener en suspenso? Si eres el Cristo, dínoslo claramente”.
25 Yesu akawajibu, “Nimewaambieni, lakini hamsadiki. Kazi ninazozifanya mimi kwa jina la Baba yangu zinanishuhudia.
Jesús les respondió: “Os lo he dicho, y no creéis. Las obras que hago en nombre de mi Padre, éstas dan testimonio de mí.
26 Lakini ninyi hamsadiki kwa sababu ninyi si kondoo wangu.
Pero vosotros no creéis, porque no sois de mis ovejas, como os he dicho.
27 Kondoo wangu huisikia sauti yangu; mimi nawajua, nao hunifuata.
Mis ovejas oyen mi voz, y yo las conozco, y me siguen.
28 Mimi nawapa uzima wa milele; nao hawatapotea milele, wala hakuna mtu atakayeweza kuwatoa mkononi mwangu. (aiōn g165, aiōnios g166)
Yo les doy vida eterna. Nunca perecerán, y nadie las arrebatará de mi mano. (aiōn g165, aiōnios g166)
29 Baba yangu ambaye ndiye aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote, wale hakuna awezaye kuwatoa mikononi mwake Baba.
Mi Padre, que me las ha dado, es más grande que todos. Nadie puede arrebatarlos de la mano de mi Padre.
30 Mimi na Baba, tu mmoja.”
Yo y el Padre somos uno”.
31 Basi, Wayahudi wakachukua mawe ili wamtupie.
Por eso los judíos volvieron a tomar piedras para apedrearlo.
32 Yesu akawaambia, “Nimewaonyesheni kazi nyingi kutoka kwa Baba. Ni ipi kati ya hizo inayowafanya mnipige mawe?”
Jesús les respondió: “Os he mostrado muchas obras buenas de mi Padre. ¿Por cuál de esas obras me apedreáis?”
33 Wayahudi wakamjibu, “Hatukupigi mawe kwa ajili ya tendo jema, ila kwa sababu ya kukufuru! Maana wajifanya kuwa Mungu hali wewe ni binadamu tu.”
Los judíos le respondieron: “No te apedreamos por una obra buena, sino por blasfemia, porque tú, siendo hombre, te haces Dios”.
34 Yesu akawajibu, “Je, haikuandikwa katika Sheria yenu: Mimi nimesema, ninyi ni miungu?
Jesús les contestó: “¿No está escrito en vuestra ley: “Yo dije que sois dioses”?
35 Mungu aliwaita miungu wale waliopewa neno lake; nasi twajua kwamba Maandiko Matakatifu yasema ukweli daima.
Si los llamó dioses, a los que vino la palabra de Dios (y la Escritura no puede ser quebrantada),
36 Je, yeye ambaye Baba alimweka wakfu na kumtuma ulimwenguni, mnamwambia: Unakufuru, eti kwa sababu nilisema: Mimi ni Mwana wa Mungu?
¿decís de aquel a quien el Padre santificó y envió al mundo: “Tú blasfemas”, porque yo dije: “Yo soy el Hijo de Dios”?
37 Kama sifanyi kazi za Baba yangu msiniamini.
Si no hago las obras de mi Padre, no me creáis.
38 Lakini ikiwa ninazifanya, hata kama hamniamini, walau ziaminini hizo kazi mpate kujua na kutambua kwamba Baba yuko ndani yangu, nami niko ndani yake.”
Pero si las hago, aunque no me creáis, creed en las obras, para que sepáis y creáis que el Padre está en mí, y yo en el Padre.”
39 Wakajaribu tena kumkamata lakini akachopoka mikononi mwao.
Volvieron a buscarlo para apresarlo, pero se les escapó de las manos.
40 Yesu akaenda tena ng'ambo ya mto Yordani, mahali Yohane alipokuwa akibatiza, akakaa huko.
Volvió a pasar el Jordán, al lugar donde Juan bautizaba al principio, y se quedó allí.
41 Watu wengi walimwendea wakasema, “Yohane hakufanya ishara yoyote. Lakini yale yote Yohane aliyosema juu ya mtu huyu ni kweli kabisa.”
Muchos se acercaron a él. Decían: “Ciertamente Juan no hizo ninguna señal, pero todo lo que Juan dijo de este hombre es verdad”.
42 Watu wengi mahali hapo wakamwamini.
Muchos creyeron allí en él.

< Yohana 10 >