< Yakobo 5 >

1 Na sasa sikilizeni enyi matajiri! Lieni na kuomboleza kwa sababu ya taabu zitakazowajieni.
Go now, ye rich, weep, howling for your miseries that are approaching.
2 Mali zenu zimeoza, na nguo zenu zimeliwa na nondo.
Your wealth has decayed, and your garments have become moth-eaten.
3 Dhahabu yenu na fedha vimeota kutu, na kutu hiyo itakuwa ushahidi dhidi yenu, nayo itakula miili yenu kama vile moto. Ninyi mmejilundikia mali katika siku hizi za mwisho!
Your gold and your silver have cankered, and their corrosion will be testimony against you, and will eat your flesh like fire. Ye have hoarded in the last days.
4 Hamkuwalipa mishahara watumishi waliofanya kazi katika mashamba yenu. Sikilizeni malalamiko yao! Kilio cha hao wanaovuna mashamba yenu kimefika masikioni mwa Bwana, Mwenye Nguvu.
Behold the wage of the workmen who reaped your fields. The man who was defrauded by you cries out. And the outcries of those who reaped have entered into the ears of the Lord of hosts.
5 Mmeishi duniani maisha ya kujifurahisha na ya anasa. Mmejinenepesha tayari kwa siku ya kuchinjwa.
Ye have lived in luxury on the earth, and were self-indulgent. Ye have nourished your hearts as in a day of slaughter.
6 Mmemhukumu na kumwua mtu asiye na hatia, naye hakuwapigeni.
Ye have condemned, ye have murdered the righteous man. He is not hostile to you.
7 Basi, ndugu zangu, muwe na subira mpaka Bwana atakapokuja. Tazameni mkulima anavyongoja kwa subira mimea yake itoe mavuno mazuri. Yeye hungojea kwa subira mvua za masika na za vuli.
Be patient therefore, brothers, until the coming of the Lord. Behold, the farmer waits for the precious fruit of the earth, being patient for it, until it receives the early and latter rain.
8 Nanyi pia mnapaswa kuwa na subira; imarisheni mioyo yenu, maana siku ya kuja kwake Bwana inakaribia.
Be ye also patient. Establish your hearts, because the coming of the Lord has approached.
9 Ndugu zangu, msinung'unikiane ninyi kwa ninyi msije mkahukumiwa na Mungu. Hakimu yu karibu, tayari kuingia.
Do not grumble, brothers, against each other, so that ye not be judged. Behold, the judge stands before the doors.
10 Ndugu, mkitaka kuona mfano wa subira na uvumilivu katika mateso, fikirini juu ya manabii ambao walinena kwa jina la Bwana.
Take an example, my brothers, of evil-suffering and longsuffering, the prophets who spoke in the name of the Lord.
11 Tunawaita hao wenye heri kwa sababu walivumilia. Mmesikia habari za uvumilivu wa Yobu, na mnajua jinsi Bwana alivyomtendea mwishoni. Maana Bwana amejaa huruma na rehema.
Behold, we regard those who endured, blessed. Ye have heard of the fortitude of Job, and have seen the outcome of the Lord, that he is very compassionate and merciful.
12 Zaidi ya hayo yote, ndugu zangu, msiape kwa mbingu, wala kwa dunia, wala kwa kitu kingine chochote. Semeni “Ndiyo” kama maana yenu ni ndiyo, na “La” kama maana yenu ni la, na hapo hamtahukumiwa na Mungu.
But above all things, my brothers, swear not. Neither by the heaven, nor the earth, nor any other oath, but let your yes be yes, and the no, no, so that ye may not fall into hypocrisy.
13 Je, pana mtu yeyote miongoni mwenu aliye na shida? Anapaswa kusali. Je, yuko mwenye furaha? Anapaswa kuimba nyimbo za sifa.
Is any man among you afflicted? Let him pray. Is any cheerful? Let him sing praise.
14 Je, yuko mgonjwa kati yenu? Anapaswa kuwaita wazee wa kanisa, nao watamwombea na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.
Is any man weak among you? Let him summon the elders of the congregation, and let them pray near him, having anointed him with olive oil in the name of the Lord.
15 Wakiomba kwa imani mgonjwa ataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu, na dhambi alizotenda zitaondolewa.
And the prayer of faith will rescue him who is depressed, and the Lord will rouse him. And if he should be a man who has committed sins, they will be forgiven him.
16 Basi, ungamanianeni dhambi zenu, na ombeaneni, ili mpate kuponywa. Sala ya mtu mwema ina nguvu ya kutenda mengi.
Confess ye the trespasses to each other, and pray for each other so that ye may be healed. A working supplication of a righteous man is very powerful.
17 Eliya alikuwa binadamu kama sisi. Aliomba kwa moyo mvua isinyeshe, nayo haikunyesha nchini kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita.
Elijah was a man of the same nature as we. And by prayer, he asked for it not to rain, and it did not rain on the earth for three years and six months.
18 Kisha akaomba tena, mvua ikanyesha kutoka angani na nchi ikatoa mazao yake.
And he prayed again, and the heaven gave rain, and the earth produced its fruit.
19 Ndugu zangu, mmoja wenu akipotoka kuhusu ukweli, na mwingine akamrudisha,
Brothers, if any man among you may be led astray from the truth, and some man converts him,
20 fahamuni kwamba, huyo anayemrudisha mwenye dhambi kutoka njia yake ya upotovu, ataiokoa roho yake kutoka kifo, na dhambi nyingi zitaondolewa.
let him know that he who converts a sinful man from his wandering way, will save a soul from death, and will hide a multitude of sins.

< Yakobo 5 >