< 2 Wathesalonike 1 >

1 Mimi Paulo, Silwano na Timotheo tunawaandikia ninyi jumuiya ya kanisa la Thesalonike, ambao ni watu wake Mungu Baba yetu na wa Bwana Yesu Kristo.
Pavel in Silvan in Timotej občini Tesaloničanov v Bogu očetu našem in Gospodu Jezusu Kristusu:
2 Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
Milost vam in mir od Boga očeta našega in Gospoda Jezusa Kristusa.
3 Ndugu, tunapaswa kushukuru Mungu daima kwa ajili yenu. Inafaa kwetu kufanya hivyo kwani imani yenu inakua sana na kupendana kwenu kunaongezeka sana.
Zahvaljevati se dolžni smo Bogu vedno za vas, bratje, kakor je spodobno, ker se močno množi vera vaša, in raste ljubezen vsakega izmed vas vseh med seboj;
4 Ndio maana sisi tunajivunia ninyi katika makanisa ya Mungu. Tunaona fahari juu ya jinsi mnavyoendelea kuamini na kustahimili katika udhalimu wote na mateso mnayopata.
Tako da se mi sami hvalimo za vas v občinah Božjih, zaradi stanovitnosti vaše in vere v vseh preganjanjih vaših in stiskah, katere prebivate;
5 Hayo yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na matokeo yake ninyi mtastahili Utawala wake ambao kwa ajili yake mnateseka.
Znamenje pravične sodbe Božje, da se za vredne spoznate kraljestva Božjega, za katero tudi trpite:
6 Mungu atafanya jambo la haki: atawalipa mateso wale wanaowatesa ninyi,
Če je res pravično pri Bogu vračati stisko njim, ki vas stiskajo,
7 na kuwapeni nafuu ninyi mnaoteseka, na sisi pia. Atafanya jambo hilo wakati Bwana atakapotokea kutoka mbinguni pamoja na malaika wake na wakuu
In vam stiskanim počitek z nami, v razodenji Gospoda Jezusa z neba z angeli moči njegove,
8 na miali ya moto, kuwaadhibu wale wanaomkataa Mungu na wale wasiotii Habari Njema ya Bwana wetu Yesu.
V ognji plamena, kaznujočega njé, ki ne poznajo Boga, in ne slušajo evangelja Gospoda našega Jezusa Kristusa,
9 Adhabu yao itakuwa kuangamizwa milele na kutengwa mbali na utukufu wake mkuu, (aiōnios g166)
Kateri bodo za kazen trpeli večno pogubo izpred obličja Gospodovega in izpred slave moči negove, (aiōnios g166)
10 wakati atakapokuja Siku ile kupokea utukufu kutoka kwa watu wake na heshima kutoka kwa wote wanaoamini. Ninyi pia mtakuwa miongoni mwao, kwani mmeuamini ule ujumbe tuliowaletea.
Kader bode prišel, da se oslavi v svetih svojih, in da se mu čudijo vsi verujoči (ker se je verovalo pričanje naše pri vas) tisti dan.
11 Ndiyo maana tunawaombeeni daima. Tunamwomba Mungu wetu awawezeshe muyastahili maisha aliyowaitia myaishi. Tunamwomba, kwa uwezo wake, atimize nia yenu ya kutenda mema na kukamilisha kazi yenu ya imani.
Za kar tudi vedno molimo za vas, da vas vredne spozna poklica naš Bog, in napolni vse dopadajenje dobrote in delo vere v moči,
12 Kwa namna hiyo, jina la Bwana wetu Yesu litapata utukufu kutoka kwenu, nanyi mtapata utukufu kutoka kwake kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo.
Da se oslavi ime Gospoda našega Jezusa Kristusa v vas, in vi v njem, po milosti Boga našega in Gospoda Jezusa Kristusa.

< 2 Wathesalonike 1 >