< 1 Wakorintho 10 >

1 Ndugu, nataka mjue kwamba babu zetu wote walikuwa chini ya ulinzi wa lile wingu, na kwamba wote walivuka salama ile bahari.
Now I do not want you to be ignorant, brothers, that our fathers were all under the cloud and all passed through the sea
2 Wote walibatizwa katika umoja na Mose kwa lile wingu na ile bahari.
—all were baptized into Moses by the cloud and by the sea—
3 Wote walikula chakula kilekile cha kiroho,
and all ate the same spiritual food
4 wakanywa pia kinywaji kilekile cha kiroho, maana walikunywa kutoka ule mwamba wa kiroho uliowafuata; mwamba huo ulikuwa Kristo mwenyewe.
and drank the same spiritual drink; because they kept drinking from a spiritual rock that accompanied them, and that Rock was the Christ.
5 Hata hivyo, wengi wao hawakumpendeza Mungu, na maiti zao zilisambazwa jangwani.
For all that, God was not pleased with most of them—their carcasses were scattered around the desert!
6 Sasa, mambo hayo yote ni mfano tu kwetu; yanatuonya sisi tusitamani ubaya kama wao walivyotamani.
Now these things became examples for us, to the intent that we should not lust after evil things as they also lusted.
7 Msiwe waabudu sanamu kama baadhi yao walivyokuwa; kama yasemavyo Maandiko: “Watu waliketi kula na kunywa, wakasimama kucheza.”
And do not become idolaters, just like some of them; as it is written: “The people sat down to eat and drink, and got up to amuse themselves.”
8 Wala tusizini kama baadhi yao walivyozini, wakaangamia siku moja watu ishirini na tatu elfu.
And let us not fornicate, just as some of them did—and in one day twenty-three thousand died!
9 Tusimjaribu Bwana kama baadhi yao walivyomjaribu, wakauawa na nyoka.
Neither let us test the Christ, just as also some of them did—and were destroyed by the snakes!
10 Wala msinung'unike kama baadhi yao walivyonung'unika, wakaangamizwa na Mwangamizi!
And do not grumble, just as also some of them did—and were executed by the destroyer!
11 Basi, mambo hayo yaliyowapata wao ni kielelezo kwa wengine, na yaliandikwa ili kutuonya sisi, ambao mwisho wa nyakati unatukabili. (aiōn g165)
Now all these things happened to them as examples and were written for our admonition, upon whom the ends of the ages have come. (aiōn g165)
12 Anayedhani amesimama imara ajihadhari asianguke.
So then, let him who thinks he stands be careful that he does not fall!
13 Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu, naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama.
No testing has overtaken you except what is common to man, and God is competent, who will not allow you to be tested beyond what you can stand, but with the testing will also provide the way out, that you may be able to endure it.
14 Kwa hiyo, wapenzi wangu, epeni ibada za sanamu.
Therefore, my beloved, flee from idolatry!
15 Naongea nanyi, watu wenye busara; jiamulieni wenyewe hayo nisemayo.
I speak as to wise men; judge for yourselves what I say.
16 Tunapomshukuru Mungu kwa kikombe kile cha baraka, je, huwa hatushiriki damu ya Kristo? Na tunapoumega mkate, je, huwa hatushiriki mwili wa Kristo?
The cup of blessing that we bless, is it not a sharing of the blood of Christ? The bread that we break, is it not a sharing of the body of Christ?
17 Kwa kuwa mkate huo ni mmoja, sisi, ingawa ni wengi, tu mwili mmoja; maana sote twashiriki mkate huohuo.
Since the loaf is one, we, the many, are one body, because we all partake of that single loaf.
18 Chukueni, kwa mfano, Wayahudi wenyewe: kwao, wenye kula vilivyotambikiwa madhabahuni waliungana na hiyo madhabahu.
Consider the physical Israel: are not those who eat the sacrifices partakers of the altar?
19 Nataka kusema nini, basi? Kwamba chakula kilichotambikiwa sanamu ni kitu zaidi ya chakula? Na hizo sanamu, je, ni kitu kweli zaidi ya sanamu?
So what am I getting at? That an idol is anything, or what is offered to idols is anything?
20 Hata kidogo! Ninachosema ni kwamba tambiko wanazotoa watu wasiomjua Mungu wanawatolea pepo, sio Mungu. Sipendi kamwe ninyi muwe na ushirika na pepo.
Rather, that the things pagans sacrifice they sacrifice to demons and not to God. I do not want you to become participants with the demons.
21 Hamwezi kunywa kikombe cha Bwana na kikombe cha pepo; hamwezi kushiriki katika meza ya Bwana na katika meza ya pepo.
You cannot drink the cup of the Lord and the cup of demons; you cannot partake of the Lord's table and of the table of demons.
22 Au je, tunataka kumfanya Bwana awe na wivu? Mnadhani tuna nguvu zaidi kuliko yeye?
Are we going to provoke the Lord's jealousy? Are we stronger than He?
23 Vitu vyote ni halali, lakini si vyote vinafaa. Vitu vyote ni halali lakini si vyote vinajenga.
All things are ‘permissible’ for me, but not all things are expedient. All things are ‘permissible’ for me, but not all things edify.
24 Mtu asitafute faida yake mwenyewe, ila faida ya mwenzake.
Let no one seek his own, but each one the other's well-being.
25 Kuleni chochote kile kiuzwacho sokoni bila ya kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu;
Eat whatever is being sold in the meat market, asking no question for the sake of conscience;
26 maana Maandiko yasema: “Dunia na vyote vilivyomo ni mali ya Bwana.”
since “the earth is the Lord's, and all its fullness.”
27 Kama mtu ambaye si muumini akiwaalikeni nanyi mkakubali kwenda, basi, kuleni vyote atakavyowaandalieni bila kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu.
If some unbeliever invites you and you decide to go, eat whatever is set before you, asking no questions for the sake of conscience.
28 Lakini mtu akiwaambieni: “Chakula hiki kimetambikiwa sanamu,” basi, kwa ajili ya huyo aliyewaambieni hivyo na kwa ajili ya dhamiri, msile.
But if anyone says, “This was offered to idols,” do not eat it for the sake of the speaker and of the conscience; since “the earth is the Lord's, and all its fullness.”
29 Nasema, “kwa ajili ya dhamiri,” si dhamiri yenu, bali dhamiri yake huyo aliyewaambieni. Mtaniuliza: “Kwa nini uhuru wangu utegemee dhamiri ya mtu mwingine?
‘Conscience’ I say, not your own but that of the other. Now just why should my freedom be judged by another's conscience?
30 Ikiwa mimi nashiriki chakula hicho huku namshukuru Mungu, kwa nini nilaumiwe kwa chakula ambacho kwa ajili yake nimemshukuru Mungu?”
If I partake with thanks, why be slandered over something I give thanks for?
31 Basi, chochote mfanyacho iwe ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
Therefore, whether you eat or you drink, or whatever you do, do all to the glory of God.
32 Msiwe kikwazo kwa Wayahudi au kwa Wagiriki au kwa kanisa la Mungu.
Give no offense, either to Jews or to Greeks or to the Church of God
33 Muwe kama mimi; najaribu kuwapendeza wote kwa kila njia, bila kutafuta faida yangu mwenyewe ila faida ya wote, wapate kuokolewa.
—even as I try to please everyone in every way, not seeking my own profit but that of the many, that they may be saved.

< 1 Wakorintho 10 >