< Zekaria 12 >

1 Hili ni tamko la neno la Yahwe kwa Israeli - Bwana asema, azitandaye mbingu na kuweka msingi wa dunia, aiumbaye roho ya mtu ndani yake, 2 “Tazama, nitaifanya Yerusalemu kuwa kikombe kiwafadhaishacho watu wote wamzungukao. Itakuwa hivyo hivyo pia kwa Yuda wakati wa kuhusuriwa kwa Yerusalemu. 3 Katika siku hiyo, nitaifanya Yerusalemu kuwa jiwe zito kwa watu wa jamaa zote. Kila atakayejaribu kuliinua jiwe hilo atajihumiza sana, na mataifa yote ya dunia yatakusanyika kinyume cha mji huo. 4 Katika siku hiyo asema Yahwe - nitampiga kila farasi kwa ushangao na kila mpanda farasi kwa wendawazimu. Nitaiangalia nyumba ya Yuda kwa upendeleo na nami nitawapiga kwa upofu farasi wa majeshi. 5 Ndipo watawala wa Yuda watakapojisemea mioyoni mwao, 'Wakaao Yerusalemu ndio nguvu yetu kwa sababu ya Yahwe wa majeshi, Mungu wao.' 6 Katika siku hiyo nitawafanya watawala wa Yuda kuwa kama mitungi ya moto katika miti na kama miali ya moto kati ya nafaka isimamayo, kwani utateketeza watu wote walio karibu upande wao wa kulia na kushoto. Yerusalemu atakaa mahali pake tena. 7 Yahwe ataziokoa hema za Yuda kwanza, ili kwamba utukufu ya nyumba ya Daudi na utukufu wa wale waishio Yerusalemu hautazidi sehemu iliyosalia ya Yuda. 8 Katika siku hiyo Yahwe atakuwa mtetezi wa wakao Yerusalemu, na siku hiyo waliodhaifu miongoni mwao watakuwa kama Daudi, wakati nyumba ya Daudi watakuwa kama Mungu, kama malaika wa Yahwe mbele yao. 9 “Itakuwa kwamba katika siku hiyo nitaanza kuyaharibu mataifa yote yajayo kinyume cha Yerusalemu. 10 Lakini nitamwaga roho ya huruma na kuiombea nyumba ya Daudi na wakao Yerusalemu, hivyo wataniangalia mimi, waliomchoma kwa mkuki. Wataniombolezea, kama amwombolezeaye mwana wa pekee; watamwombolezea kwa uchungu sana kama aombolezaye kifo cha mzaliwa wa kwanza. 11 Katika siku hiyo maombolezo huko Yerusalemu yatakuwa kama maombolezo ya Hadadi Rimoni katika tambarare za Megido. 12 Nchi itaomboleza, kila ukoo peke yao. Ukoo wa nyumba ya Daudi utakuwa peke yake na wake zao watakuwa peke yao mbali na wanaume. Ukoo wa nyumba ya Nathani utakuwa peke yao na wake zao watakuwa peke yao mbali na waume. 13 Ukoo wa nyumba ya Lawi utakuwa peke yao na wake zao watakuwa peke yao mbali na waume. Ukoo wa Washimei utakuwa peke yao na wake zao watakuwa peke yao mbali na waume. 14 Kila ukoo uliosalia - kila mmoja utakuwa peke yake na wake watakuwa pekee mbali na waume.

< Zekaria 12 >